Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 81
Bible en Swahili de l’est


1 Mwimbieni Mungu, nguvu zetu, nyimbo za furaha, Mshangilieni Mungu wa Yakobo. Psaumes 66.1 Jérémie 31.7 Psaumes 8.1 Psaumes 46.1-46.7 Psaumes 46.11
2 Pazeni zaburi, pigeni matari, Kinubi chenye sauti nzuri, na kinanda. Psaumes 92.3 Exode 15.20 Psaumes 149.1-149.3 Marc 14.26 Psaumes 95.1-95.2
3 Pigeni panda mwandamo wa mwezi, Wakati wa mbalamwezi, sikukuu yetu. 2 Chroniques 8.13 Nombres 15.3 Colossiens 2.16 Deutéronome 16.15 Nombres 10.1-10.10
4 Kwa maana ni sheria kwa Israeli, Ni hukumu ya Mungu wa Yakobo. 5 Aliamuru iwe ushuhuda katika Yusufu, Alipoondoka juu ya nchi ya Misri; Maneno yake nisiyemjua naliyasikia. Psaumes 114.1 Jérémie 5.15 Deutéronome 28.49 Psaumes 77.15 1 Corinthiens 14.21-14.22
6 Nimelitenga bega lake na mzigo, Mikono yake ikaachana na kikapu. Esaïe 9.4 Esaïe 10.27 Exode 6.6 Exode 1.14 Psaumes 68.13
7 Katika shida uliniita nikakuokoa; Nalikuitikia katika sitara ya radi; Nalikujaribu penye maji ya Meriba. Psaumes 50.15 Nombres 20.13 Exode 19.19 Exode 2.23 Exode 14.10
8 Enyi watu wangu, sikieni, nami nitawaonya, Ee Israeli, kama ukitaka kunisikiliza; Psaumes 50.7 Psaumes 81.13 Jean 3.11 Deutéronome 32.46 Deutéronome 5.27
9 Usiwe na mungu mgeni ndani yako; Wala usimsujudie mungu mwingine. Esaïe 43.12 Deutéronome 32.12 Malachie 2.11 Exode 20.3-20.5 1 Corinthiens 8.5-8.6
10 Mimi ndimi Bwana, Mungu wako, Niliyekupandisha toka nchi ya Misri; Fumbua sana kinywa chako nami nitakijaza. Exode 20.2 Psaumes 37.3-37.4 Apocalypse 22.17 Jérémie 11.4 Jean 16.23
11 Lakini watu wangu hawakuisikiliza sauti yangu, Wala Israeli hawakunitaka. Exode 32.1 Deutéronome 32.15 Jérémie 2.11-2.13 Proverbes 1.30 Jérémie 7.23-7.24
12 Nikawaacha wakaenda kwa ukaidi wa mioyo yao, Waenende katika mashauri yao. Romains 1.24 Jérémie 7.24 Actes 7.42 Esaïe 30.1 Romains 1.26-1.27
13 Laiti watu wangu wangenisikiliza, Na Israeli angeenenda katika njia zangu; Deutéronome 5.29 Esaïe 48.18 Matthieu 23.37 Luc 19.41-19.42 Deutéronome 10.12-10.13
14 Ningewadhili adui zao kwa upesi, Na juu ya watesi wao ningegeuza mkono wangu; Amos 1.8 Zacharie 13.7 Nombres 14.45 Josué 23.13 Juges 2.20-2.23
15 Wamchukiao Bwana wangenyenyekea mbele zake, Bali wakati wao ungedumu milele. Romains 1.30 Psaumes 83.2-83.18 Jean 15.22-15.23 Psaumes 63.3 Deutéronome 7.10
16 Naam, ningewalisha kwa unono wa ngano, Ningewashibisha kwa asali itokayo mwambani. Psaumes 147.14 Deutéronome 32.13-32.14 Job 29.6 Juges 14.18 1 Samuel 14.25-14.26

Cette Bible est dans le domaine public.