Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 29.24
Bible en Swahili de l’est


1 Ole wa Arieli, Arieli, mji ambao Daudi alifanya kituo chake ndani yake; ongezeni mwaka baada ya mwaka; sikukuu na zirudi wakati wake,2 Samuel 5.9 Hébreux 10.1 Ezéchiel 43.15-43.16 Amos 4.4-4.5 Osée 5.6
2 ndipo nitamwudhi Arieli; kutakuwapo maombolezo na kilio; naye atakuwa kwangu kama Arieli.Esaïe 5.25-5.30 Esaïe 17.14 Ezéchiel 39.17 Esaïe 34.6 Apocalypse 19.17-19.18
3 Nami nitapiga kimo juu yako pande zote, nitakuhusuru kwa ngome, nami nitajenga maboma yakuzunguke.Luc 19.43-19.44 Ezéchiel 21.22 2 Rois 19.32 2 Rois 18.17 2 Rois 24.11-24.12
4 Nawe utashushwa, nawe utanena toka chini ya nchi, na maneno yako yatakuwa chini toka mavumbini; na sauti yako itakuwa kama sauti ya mtu mwenye pepo, ikitoka katika nchi, na matamko yako yatanong’ona toka mavumbini.Esaïe 8.19 Esaïe 2.11-2.21 Lamentations 1.9 Esaïe 3.8 Esaïe 51.23
5 Lakini wingi wa adui zako utakuwa kama mavumbi membamba, na wingi wao watishao utakuwa kama makapi yapitayo; naam, itakuwa mara na kwa ghafula.1 Thessaloniciens 5.3 Esaïe 30.13 Esaïe 17.13-17.14 Esaïe 37.36 Esaïe 10.16-10.19
6 Naye atajiliwa na Bwana wa majeshi kwa ngurumo, na tetemeko la nchi, na sauti kuu, na chamchela, na tufani, na mwali wa moto uteketezao.Marc 13.8 Luc 21.11 Matthieu 24.7 Apocalypse 11.19 1 Samuel 2.10
7 Na wingi wa mataifa wapiganao na Arieli, wote wapiganao naye na ngome yake, nao wamwudhio, watakuwa kama ndoto, na maono ya usiku.Job 20.8 Psaumes 73.20 Zacharie 12.9 Michée 4.11-4.12 Jérémie 25.31-25.33
8 Tena itakuwa kama mtu mwenye njaa aotapo, kumbe, anakula; lakini aamkapo, nafsi yake haina kitu; na kama mtu mwenye kiu aotapo, kumbe, anakunywa; lakini aamkapo, kumbe, anazimia, na nafsi yake inatamani; hivyo ndivyo utakavyokuwa huo wingi wa mataifa waletao vita juu ya mlima Sayuni.2 Chroniques 32.21 Psaumes 73.20 Esaïe 44.12 Esaïe 10.7-10.16
9 Ngojeni mstaajabu; fanyeni anasa zenu na kuwa vipofu; wamelewa wala si kwa mvinyo; wamewaya-waya wala si kwa sababu ya kileo.Esaïe 51.21-51.22 Esaïe 19.14 Esaïe 33.13-33.14 Marc 14.41 Esaïe 49.26
10 Kwa maana Bwana amewamwagieni roho ya usingizi, amefumba macho yenu, yaani, manabii; amefunika vichwa vyenu, yaani, waonaji.Romains 11.8 Esaïe 44.18 Michée 3.6 Esaïe 6.9-6.10 Psaumes 69.23
11 Na maono yote yamekuwa kwenu kama maneno ya chuo kilichotiwa muhuri, ambacho watu humpa mtu aliye na maarifa, wakisema, Tafadhali ukisome hiki; akasema, Siwezi, kwa kuwa kimetiwa muhuri;Esaïe 8.16 Daniel 12.4 Matthieu 13.11 Daniel 12.9 Matthieu 16.17
12 kisha chuo hiki apewa mtu asiye na maarifa, akaambiwa, Kisome hicho tafadhali, akasema, Sina maarifa mimi.Jean 7.15-7.16 Jérémie 5.4 Esaïe 28.12-28.13 Esaïe 29.18 Osée 4.6
13 Bwana akanena, Kwa kuwa watu hawa hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao, bali mioyo yao wamefarakana nami, na kicho chao walicho nacho kwangu ni maagizo ya wanadamu waliyofundishwa;Marc 7.2-7.13 Jérémie 12.2 Matthieu 15.2-15.9 Jérémie 3.10 Ezéchiel 33.31-33.33
14 kwa sababu hiyo mimi nitafanya tena kazi ya ajabu kati ya watu hawa, kazi ya ajabu na mwujiza; na akili za watu wao wenye akili zitapotea, na ufahamu wa wenye busara wao utafichwa.Habakuk 1.5 Jérémie 49.7 Esaïe 28.21 Esaïe 6.9-6.10 1 Corinthiens 1.19-1.24
15 Ole wao wanaojitahidi kumficha Bwana mashauri yao, na matendo yao yamo gizani, nao husema, Ni nani atuonaye? Nani atujuaye?Ezéchiel 8.12 Esaïe 30.1 Esaïe 47.10 Psaumes 10.11-10.13 Esaïe 28.15
16 Ninyi mnapindua mambo; Je! Mfinyanzi ahesabiwe kuwa kama udongo; kitu kilichofinyangwa kimnene yeye aliyekifinyanga, Hakunifinyanga huyu; au kitu kilichoumbwa kimnene yeye aliyekiumba, Yeye hana ufahamu?Romains 9.19-9.21 Psaumes 94.8-94.9 Esaïe 45.9-45.11 Actes 17.6 Jérémie 18.1-18.10
17 Je! Si muda mdogo uliobaki, na Lebanoni itageuzwa kuwa shamba lizaalo sana, na lile shamba lizaalo sana litahesabiwa kuwa msitu?Esaïe 32.15 Esaïe 65.12-65.16 Osée 3.4 Esaïe 41.19 Habakuk 2.3
18 Na katika siku hiyo viziwi watasikia maneno ya hicho chuo, na macho ya vipofu yataona katika upofu na katika giza.Esaïe 35.5 Matthieu 11.5 Marc 7.37 Psaumes 119.18 Ephésiens 1.17-1.19
19 Wanyenyekevu nao wataongeza furaha yao katika Bwana, na maskini katika wanadamu watafurahi katika Mtakatifu wa Israeli.Jacques 2.5 Esaïe 61.1 Matthieu 11.29 Matthieu 11.5 Psaumes 25.9
20 Kwa maana mwenye kutisha ameangamizwa, naye mwenye dharau amekoma, nao wote watazamiao uovu wamekatiliwa mbali;Michée 2.1 Luc 16.14 Esaïe 29.5 Esaïe 13.3 Esaïe 28.14-28.22
21 hao wamfanyao mtu kuwa amekosa katika neno, na kumtegea mtego yeye aonyaye langoni, na kumgeuza mwenye haki kwa kitu kisichofaa.Amos 5.10-5.12 Michée 2.6-2.7 Actes 3.14 Jérémie 26.2-26.8 Jérémie 20.7-20.10
22 Basi, Bwana aliyemkomboa Ibrahimu asema hivi, katika habari za nyumba ya Yakobo; Yakobo hatatahayarika sasa, wala uso wake hautabadilika rangi yake.Esaïe 51.2 Esaïe 54.4 Esaïe 45.17 Jérémie 30.5-30.7 Apocalypse 5.9
23 Bali atakapowaona watoto wake, walio kazi ya mikono yangu, katikati yake, wao watalitakasa jina langu; naam, watamtakasa Mtakatifu wa Yakobo, nao watamcha Mungu wa Israeli.Esaïe 8.13 Esaïe 19.25 Esaïe 45.11 Esaïe 5.16 Esaïe 60.21
24 Hao nao wakosao rohoni mwao watapata kufahamu, na hao wanung’unikao watajifunza elimu.Esaïe 28.7 Luc 15.17-15.19 Apocalypse 20.2-20.3 Esaïe 41.20 Esaïe 60.16

Cette Bible est dans le domaine public.