Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Amos 4.12
Bible en Swahili de l’est


1 Lisikieni neno hili, enyi ng’ombe wa Bashani, mnaokaa juu ya mlima wa Samaria, mnaowaonea maskini, na kuwaponda wahitaji; mnaowaambia bwana zao, Haya! Leteni, tunywe.Psaumes 22.12 Amos 6.1 Ezéchiel 39.18 Amos 5.11 Amos 8.4-8.6
2 Bwana MUNGU ameapa kwa utakatifu wake, ya kuwa, tazama, siku zitawajilia, watakapowaondoa ninyi kwa kulabu, na mabaki yenu kwa ndoana.Psaumes 89.35 Jérémie 16.16 Amos 6.8 Habakuk 1.15-1.16 Esaïe 37.29
3 Nanyi mtatoka kwenye mahali palipobomolewa, kila mwanamke moja kwa moja mbele yake; nanyi mtajitupa katika Harmoni, asema Bwana.Ezéchiel 12.5 Ezéchiel 12.12 2 Rois 25.4 Esaïe 2.20 Matthieu 16.26
4 Njoni Betheli, mkakose; njoni Gilgali, mkaongeze makosa; kaleteni dhabihu zenu kila asubuhi, na zaka zenu kila siku ya tatu;Osée 4.15 Ezéchiel 20.39 Matthieu 23.32 Osée 12.11 Nombres 28.3-28.4
5 mkachome sadaka ya shukrani, ya kitu kilichotiwa chachu; mkatangaze sadaka mtoazo kwa hiari na kuzihubiri habari zake; kwa maana ndivyo viwapendezavyo ninyi, enyi wana wa Israeli, asema Bwana MUNGU.Lévitique 22.18-22.21 Psaumes 81.12 Osée 9.10 Lévitique 7.12-7.13 Osée 9.1
6 Mimi nami nimewapa usafi wa meno katika miji yenu yote, na kutindikiwa na mkate mahali penu pote; lakini hamkunirudia mimi, asema Bwana.Aggée 2.17 Jérémie 5.3 Esaïe 9.13 Lévitique 26.26 1 Rois 17.1
7 Tena nimeizuia mvua msiipate, ilipobaki miezi mitatu kabla ya mavuno; nami nimenyesha mvua juu ya mji mmoja, nikaizuia mvua isinyeshe juu ya mji mwingine; sehemu moja ilipata mvua, na sehemu isiyopata mvua ilikatika.Exode 9.26 Jérémie 3.3 Esaïe 5.6 Exode 10.23 Exode 9.4
8 Basi kutoka miji miwili mitatu walitanga-tanga kuendea mji mwingine wapate kunywa maji, wasipate ya kuwatosha; lakini hamkunirudia mimi, asema Bwana.Amos 4.6 Aggée 1.6 1 Rois 18.5 Jérémie 14.3-14.4 Ezéchiel 4.16-4.17
9 Nami nimewapiga kwa ukavu na koga; wingi wa bustani zenu na mashamba yenu ya mizabibu, na mitini yenu na mizeituni yenu imeliwa na tunutu; Lakini hamkunirudia mimi, asema Bwana.Deutéronome 28.22 Aggée 2.17 Joël 1.4 Amos 7.1-7.2 Amos 4.6
10 Nimewapelekea tauni, kama tauni ya Misri; vijana wenu nimewaua kwa upanga, na farasi wenu nimewachukulia mbali; nami nimeupandisha uvundo wa matuo yenu na kuuingiza katika mianzi ya pua zenu; lakini hamkunirudia mimi, asema Bwana.Joël 2.20 Lévitique 26.25 Deutéronome 28.60 2 Rois 13.7 Jérémie 18.21
11 Baadhi yenu nimewaangamiza, kama hapo Mungu alipoiangamiza Sodoma na Gomora, nanyi mkawa kama kinga kilichonyakuliwa motoni; lakini hamkunirudia mimi, asema Bwana.Esaïe 13.19 Zacharie 3.2 Genèse 19.24-19.25 Jude 1.23 Amos 4.6
12 Basi nitakutenda hivi, Ee Israeli, na kwa sababu nitakutenda hivi, ujiweke tayari kuonana na Mungu wako, Ee Israeli.1 Thessaloniciens 5.2-5.4 Jacques 4.1-4.10 Matthieu 24.44-25.13 Esaïe 47.3 Luc 21.3-21.36
13 Kwa maana, angalia, yeye aifanyizaye milima, na kuuumba upepo, na kumwambia mwanadamu mawazo yake, afanyaye asubuhi kuwa giza, na kupakanyaga mahali pa dunia palipoinuka; Bwana, Mungu wa majeshi, ndilo jina lake.Amos 5.8 Michée 1.3 Amos 9.6 Daniel 2.28 Esaïe 47.4

Cette Bible est dans le domaine public.