Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

1 Thessaloniciens 3.7
Bible en Swahili de l’est


1 Basi kwa hiyo, tulipokuwa hatuwezi kuvumilia zaidi, tuliona vema kuachwa Athene peke yetu.Actes 17.15 1 Thessaloniciens 3.5 1 Thessaloniciens 2.17 Jérémie 20.9 2 Corinthiens 2.13
2 Tukamtuma Timotheo ndugu yetu, mtumishi wa Mungu katika Injili ya Kristo, ili kuwafanya ninyi imara na kuwafariji kwa habari ya imani yenu;Actes 14.22-14.23 Ephésiens 6.21-6.22 Philippiens 1.25 Actes 17.14-17.15 2 Corinthiens 1.19
3 mtu asifadhaishwe na dhiki hizi; maana ninyi wenyewe mnajua ya kuwa twawekewa hizo.Actes 14.22 Actes 9.16 Actes 21.13 Matthieu 24.9-24.10 1 Corinthiens 15.58
4 Kwa kuwa tulipokuwapo kwenu tulitangulia kuwaambia kwamba tutapata dhiki, kama ilivyotukia, nanyi mwajua.1 Thessaloniciens 2.14 1 Thessaloniciens 2.2 Actes 20.24 2 Thessaloniciens 1.4-1.6 Jean 16.1-16.3
5 Kwa hiyo mimi nami nilipokuwa siwezi kuvumilia tena, nalituma mtu ili niijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, na taabu yetu ikawa haina faida.Matthieu 4.3 Philippiens 2.16 Jacques 1.13-1.14 1 Corinthiens 7.5 Ephésiens 4.14
6 Lakini Timotheo alipotujia hivi sasa kutoka kwenu, alituletea habari njema za imani yenu na upendo wenu, na ya kwamba mnatukumbuka vema siku zote; mkitamani kutuona sisi vile vile kama sisi kuwaona ninyi.1 Corinthiens 11.2 Proverbes 25.25 Actes 18.5 1 Thessaloniciens 1.3 Esaïe 52.7
7 Kwa sababu hiyo, ndugu, tulifarijiwa kwa habari zenu, katika msiba na dhiki yetu yote, kwa imani yenu.2 Corinthiens 1.4 Actes 17.4-17.10 1 Thessaloniciens 3.8-3.9 2 Timothée 3.10-3.12 2 Corinthiens 7.13
8 Kwa kuwa sasa twaishi, ikiwa ninyi mnasimama imara katika Bwana.1 Corinthiens 16.13 Colossiens 1.23 Ephésiens 3.17 Actes 11.23 Hébreux 10.23
9 Maana ni shukrani gani tuwezayo kumlipa Mungu kwa ajili yenu, kwa furaha ile yote tunayoifurahia, kwa sababu yenu mbele za Mungu wetu;2 Corinthiens 9.15 Deutéronome 12.18 2 Samuel 6.21 Psaumes 96.12-96.13 Néhémie 9.5
10 usiku na mchana tunapoomba kwa juhudi tupate kuwaona nyuso zenu, na kuyatengeneza mapungufu ya imani yenu?2 Timothée 1.3 2 Corinthiens 13.9 Romains 1.10-1.12 2 Corinthiens 1.24 Apocalypse 4.8
11 Basi Mungu mwenyewe, Baba yetu, na Bwana wetu Yesu, atuongoze njia yetu tufike kwenu.2 Thessaloniciens 2.16 Proverbes 3.5-3.6 1 Thessaloniciens 3.13 2 Thessaloniciens 3.5 Matthieu 6.26
12 Bwana na awaongeze na kuwazidisha katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile sisi nasi tulivyo kwenu;Philippiens 1.9 2 Thessaloniciens 1.3 1 Thessaloniciens 4.9-4.10 1 Thessaloniciens 5.15 Matthieu 22.39
13 apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.1 Thessaloniciens 5.23 1 Thessaloniciens 2.19 Colossiens 1.22 Ephésiens 5.27 Jude 1.14

Cette Bible est dans le domaine public.