Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Tite 3
Bible en Swahili de l’est


1 Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa kila kazi njema; Romains 13.1-13.7 Ecclésiaste 10.4 2 Timothée 2.21 1 Pierre 2.13-2.17 Matthieu 22.21
2 wasimtukane mtu ye yote, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote. 2 Timothée 2.24-2.25 1 Timothée 3.3 Ephésiens 4.31 Matthieu 11.29 Colossiens 3.12-3.13
3 Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana. Colossiens 3.7 Ephésiens 2.1-2.3 Colossiens 1.21 Romains 3.9-3.20 2 Timothée 3.2-3.3
4 Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa; Tite 2.10-2.11 Hébreux 9.26 Ephésiens 2.4-2.10 Romains 2.4 1 Timothée 2.3
5 si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu; Ephésiens 2.8-2.9 1 Corinthiens 6.11 1 Pierre 3.21 Romains 12.2 Ephésiens 2.4
6 ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu; Romains 5.5 Joël 2.28 Actes 2.33 Actes 10.45 Proverbes 1.23
7 ili tukihesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu. Romains 8.17 Tite 1.2 Romains 3.24 Tite 2.11 1 Corinthiens 6.11
8 Ni neno la kuaminiwa; na mambo hayo nataka uyanene kwa nguvu, ili wale waliomwamini Mungu wakumbuke kudumu katika matendo mema. Hayo ni mazuri, tena yana faida kwa wanadamu. Tite 3.14 Tite 2.14 1 Timothée 1.15 Psaumes 16.2-16.3 Romains 4.5
9 Lakini maswali ya upuzi ujiepushe nayo, na nasaba, na magomvi, na mashindano ya sheria. Kwa kuwa hayana faida, tena hayana maana. 2 Timothée 2.14 2 Timothée 2.23 Tite 1.14 1 Timothée 4.7 Job 15.3
10 Mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, mkatae; Romains 16.17 2 Jean 1.10 2 Timothée 3.5 2 Thessaloniciens 3.14 Galates 5.20
11 ukijua ya kuwa mtu kama huyo amepotoka, tena atenda dhambi, maana amejihukumu hatia yeye mwenyewe. 1 Timothée 1.19-1.20 2 Timothée 2.14 Luc 7.30 Actes 15.24 Hébreux 10.26
12 Wakati nitakapomtuma Artema kwako au Tikiko, jitahidi kuja kwangu huku Nikopoli; kwa maana huku nimekusudia kukaa wakati wa baridi. Actes 20.4 2 Timothée 4.9 2 Timothée 4.21 2 Timothée 4.12 1 Corinthiens 16.8-16.9
13 Zena, yule mwana-sheria, na Apolo, uwasafirishe kwa bidii, wasipungukiwe na cho chote. Actes 18.24 Matthieu 22.35 Actes 28.10 Luc 14.3 Luc 11.45
14 Watu wetu nao wajifunze kudumu katika matendo mema, kwa matumizi yaliyo lazima, ili wasiwe hawana matunda. Colossiens 1.10 Philippiens 1.11 Philippiens 4.17 Tite 3.8 Matthieu 7.19
15 Watu wote walio pamoja nami wakusalimu. Tusalimie wale watupendao katika imani. Neema na iwe pamoja nanyi nyote. Colossiens 4.18 Galates 5.6 2 Jean 1.1-1.2 Hébreux 13.25 3 Jean 1.1

Cette Bible est dans le domaine public.