Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Apocalypse 11
Bible en Swahili de l’est


1 Nikapewa mwanzi kama fimbo; na mmoja akaniambia, Inuka, ukalipime hekalu la Mungu, na madhabahu, na hao wasujuduo humo. Apocalypse 21.15 Ezéchiel 42.15-42.20 Zacharie 2.1-2.2 Ephésiens 2.20-2.22 1 Pierre 2.5
2 Na behewa iliyo nje ya hekalu uiache nje wala usiipime, kwa maana Mataifa wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arobaini na miwili. Apocalypse 12.6 Luc 21.24 Daniel 7.25 Daniel 12.7 Apocalypse 11.3
3 Nami nitawaruhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini, hali wamevikwa magunia. Apocalypse 11.2 Apocalypse 12.6 2 Corinthiens 13.1 Deutéronome 19.15 Genèse 37.34
4 Hao ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili visimamavyo mbele za Bwana wa nchi. Jérémie 11.16 Psaumes 52.8 Zacharie 4.11-4.14 Zacharie 4.2-4.3 Luc 11.33
5 Na mtu akitaka kuwadhuru, moto hutoka katika vinywa vyao na kuwala adui zao. Na mtu akitaka kuwadhuru, hivyo ndivyo impasavyo kuuawa. Jérémie 5.14 2 Rois 1.10-1.12 Zacharie 2.8 Actes 9.4-9.5 Psaumes 18.8
6 Hao wana amri ya kuzifunga mbingu, ili mvua isinyeshe katika siku za unabii wao. Nao wana amri juu ya maji kuyageuza kuwa damu, na kuipiga nchi kwa kila pigo, kila watakapo. 1 Rois 17.1 Luc 4.25 1 Samuel 4.8 Jacques 5.16-5.18 Exode 7.17-7.25
7 Hata watakapoumaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika kuzimu atafanya vita nao, naye atawashinda na kuwaua. Apocalypse 13.7 Daniel 8.23-8.24 Daniel 7.25 Luc 13.32 Apocalypse 13.11
8 Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule mkuu, uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wao aliposulibiwa. Apocalypse 18.10 Apocalypse 18.18 Apocalypse 18.21 Apocalypse 18.2 Apocalypse 16.19
9 Na watu wa hao jamaa na kabila na lugha na taifa waitazama mizoga yao siku tatu u nusu, wala hawaiachi mizoga yao kuwekwa kaburini. Psaumes 79.2-79.3 Apocalypse 10.11 Apocalypse 11.11 Ecclésiaste 6.3 Apocalypse 11.2-11.3
10 Nao wakaao juu ya nchi wafurahi juu yao na kushangilia. Nao watapelekeana zawadi wao kwa wao, kwa kuwa manabii hao wawili waliwatesa wao wakaao juu ya nchi. Apocalypse 3.10 Jean 16.20 1 Rois 18.17 Néhémie 8.10-8.12 Actes 7.54-7.57
11 Na baada ya siku hizo tatu u nusu, roho ya uhai itokayo kwa Mungu ikawaingia, wakasimama juu ya miguu yao; na hofu kuu ikawaangukia watu waliowatazama. Genèse 2.7 Apocalypse 11.9 Jérémie 33.9 Ezéchiel 37.5-37.14 Apocalypse 11.13
12 Wakasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, Pandeni hata huku. Wakapanda mbinguni katika wingu, adui zao wakiwatazama. Actes 1.9 Apocalypse 4.1 2 Rois 2.11 1 Thessaloniciens 4.17 Apocalypse 12.5
13 Na katika saa ile palikuwa na tetemeko kuu la nchi, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka; wanadamu elfu saba wakauawa katika tetemeko lile. Na waliosalia wakaingiwa na hofu, wakamtukuza Mungu wa mbingu. Apocalypse 14.7 Apocalypse 6.12 Josué 7.19 Apocalypse 16.18-16.19 Apocalypse 11.19
14 Ole wa pili umekwisha pita, tazama ole wa tatu unakuja upesi. Apocalypse 8.13 Apocalypse 9.12 Apocalypse 15.1 Apocalypse 16.1-16.21
15 Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele. Apocalypse 12.10 Daniel 7.27 Daniel 7.14 Apocalypse 10.7 Apocalypse 16.17
16 Na wale wazee ishirini na wanne waketio mbele za Mungu katika viti vya enzi vyao wakaanguka kifulifuli, wakamsujudia Mungu Apocalypse 4.4 Apocalypse 4.10 Apocalypse 19.4 Apocalypse 7.11 Apocalypse 5.14
17 wakisema, Tunakushukuru wewe, Bwana Mungu Mwenyezi, uliyeko na uliyekuwako, kwa sababu umeutwaa uweza wako ulio mkuu, na kumiliki. Apocalypse 1.8 Apocalypse 19.6 Apocalypse 16.5 Apocalypse 1.4 Apocalypse 19.11-20.3
18 Na mataifa walikasirika, hasira yako nayo ikaja, na wakati ukaja wa kuhukumiwa waliokufa, na wa kuwapa thawabu yao watumwa wako manabii na watakatifu, na hao walichao jina lako, wadogo kwa wakubwa, na wa kuwaharibu hao waiharibuo nchi. Apocalypse 19.5 Apocalypse 20.12 Apocalypse 6.10-6.11 2 Thessaloniciens 1.5-1.7 Apocalypse 11.2
19 Kisha Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua ya mawe nyingi sana. Apocalypse 16.21 Apocalypse 8.5 Exode 25.21-25.22 Apocalypse 4.5 Apocalypse 14.15-14.17

Cette Bible est dans le domaine public.