Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Genèse 12
Bible en Swahili de l’est


1 Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; Hébreux 11.8 Luc 14.26-14.33 Esaïe 41.9 Genèse 15.7 Apocalypse 18.4
2 nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; Genèse 18.18 Galates 3.14 Genèse 17.4-17.6 Genèse 46.3 Deutéronome 26.5
3 nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa. Genèse 22.18 Genèse 26.4 Genèse 27.29 Galates 3.8 Genèse 28.14
4 Basi Abramu akaenda, kama Bwana alivyomwamuru; Lutu akaenda pamoja naye. Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka sabini na mitano alipotoka Harani. Genèse 11.27 Genèse 11.31 Hébreux 11.8
5 Abramu akamchukua Sarai mkewe, na Lutu mwana wa nduguye, na vitu vyao vyote walivyokuwa wamejipatia na hao watu waliowapata huko Harani, wakatoka ili kwenda nchi ya Kanaani; nao wakaingia katika nchi ya Kanaani. Genèse 14.14 Genèse 11.31 Genèse 10.19 Actes 7.4 Hébreux 11.8-11.9
6 Abramu akapita katikati ya nchi mpaka mahali patakatifu pa Shekemu; mpaka mwaloni wa More. Na Wakanaani siku zile walikaa katika nchi hiyo. Deutéronome 11.30 Genèse 35.4 Hébreux 11.9 Juges 7.1 Genèse 13.7
7 Bwana akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye huko akamjengea madhabahu Bwana aliyemtokea. Genèse 17.8 Genèse 13.15 Genèse 18.1 Genèse 17.1 Galates 3.16
8 Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; alikuwa na Betheli upande wa magharibi, na Ai upande wa mashariki, akamjengea Bwana madhabahu huko, akaliitia jina la Bwana. Néhémie 11.31 Genèse 4.26 Genèse 21.33 Genèse 28.19 Romains 10.12-10.14
9 Naye Abramu akasafiri, akazidi kwenda pande za kusini. Genèse 13.3 Genèse 24.62 Psaumes 105.13 Genèse 13.1 Hébreux 11.13-11.14
10 Basi kulikuwa njaa katika nchi ile; Abramu akashuka Misri, akae huko kwa muda maana njaa ilikuwa nzito katika nchi. Genèse 43.1 2 Samuel 21.1 Jean 16.33 Genèse 26.1-26.3 Genèse 42.5
11 Ikawa alipokuwa karibu kuingia Misri, akamwambia Sarai mkewe, Tazama, najua ya kuwa u mwanamke mzuri wa uso; Genèse 29.17 Genèse 26.7 Genèse 12.14 Cantique 1.14 Genèse 39.6-39.7
12 basi itakuwa, Wamisri watakapokuona watasema, Huyu ni mkewe; kisha wataniua mimi na wewe watakuacha hai. Genèse 20.11 Genèse 26.7 1 Jean 1.8-1.10 Matthieu 10.28 1 Samuel 27.1
13 Tafadhali useme, wewe u ndugu yangu, iwe heri kwangu kwa ajili yako, na nafsi yangu iishi kwa ajili yako. Genèse 26.7 Genèse 20.2 Genèse 20.5 Genèse 20.12-20.13 Genèse 11.29
14 Basi ikawa Abramu alipofika Misri, Wamisri wakamwona huyo mwanamke ya kwamba yeye ni mzuri sana. Genèse 6.2 Matthieu 5.28 Genèse 39.7 Genèse 3.6
15 Wakuu wa Farao wakamwona, nao wakamsifu kwa Farao; basi yule mwanamke akachukuliwa nyumbani mwa Farao. Genèse 20.2 Osée 7.4-7.5 Genèse 41.1 Exode 2.5 Jérémie 25.19
16 Naye akamtendea Abramu mema kwa ajili yake; naye alikuwa na kondoo na ng’ombe, na punda waume, na watumwa, na wajakazi, na punda wake, na ngamia. Genèse 20.14 Genèse 13.2 Genèse 32.13-32.15 Genèse 24.35 Genèse 32.5
17 Lakini Bwana akampiga Farao na nyumba yake mapigo makuu, kwa ajili ya Sarai, mkewe Abramu. 1 Chroniques 16.21 Genèse 20.18 Psaumes 105.14-105.15 Hébreux 13.4 Job 34.19
18 Ndipo Farao akamwita Abramu, akasema, N’nini hili ulilonitendea? Mbona hukuniambia ya kuwa huyo ni mkeo? Genèse 20.9-20.10 Genèse 44.15 Josué 7.19 Genèse 26.9-26.11 Genèse 3.13
19 Mbona ulisema, Huyo ni umbu langu, hata nikamtwaa kuwa mke wangu? Basi sasa, huyo mke wako umchukue, uende zako. 20 Farao akawaagiza watu kwa ajili yake, wakampeleka njiani, na mkewe, na kila alichokuwa nacho. Exode 18.27 Psaumes 105.14-105.15 1 Samuel 29.6-29.11 Proverbes 21.1

Cette Bible est dans le domaine public.