Renouvellement des promesses à Abram
1 Baada ya mambo hayo neno la Bwana likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana.
Genèse 26.24 Esaïe 41.10 Psaumes 119.114 Psaumes 84.11 Lamentations 3.24
2 Abramu akasema, Ee Bwana MUNGU, utanipa nini, nami naenda zangu hali sina mtoto, na atakayeimiliki nyumba yangu ni huyu Eliezeri, Mdameski?
Genèse 25.21 Actes 7.5 Proverbes 17.2 Psaumes 127.3 Genèse 43.19
3 Abramu akasema, Tazama, hukunipa uzao, na mtu aliyezaliwa nyumbani mwangu ndiye mrithi wangu.
Genèse 14.14 Proverbes 29.21 Genèse 12.2 Proverbes 30.23 Jérémie 12.1
4 Nalo neno la Bwana likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali atakayetoka katika viuno vyako ndiye atakayekurithi.
Galates 4.28 Genèse 17.16 Genèse 21.12 Philémon 1.12 2 Samuel 16.11
5 Akamleta nje, akasema, Tazama sasa mbinguni, kazihesabu nyota, kama ukiweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.
Romains 4.18 Deutéronome 1.10 Hébreux 11.12 Genèse 22.17 Exode 32.13
6 Akamwamini Bwana, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki.
Jacques 2.23 Galates 3.6-3.14 Romains 4.9 Romains 4.3-4.6 Romains 4.20-4.25
7 Kisha akamwambia, Mimi ni Bwana, niliyekuleta kutoka Uru wa Wakaldayo nikupe nchi hii ili uirithi.
Psaumes 105.44 Actes 7.2-7.4 Néhémie 9.7-9.8 Genèse 12.1 Psaumes 105.42
8 Akasema, Ee Bwana MUNGU, nipateje kujua ya kwamba nitairithi?
Luc 1.18 Psaumes 86.17 Esaïe 7.11 2 Rois 20.8 Juges 6.36-6.40
9 Akamwambia, Unipatie ndama wa miaka mitatu, na mbuzi mke wa miaka mitatu, na kondoo mume wa miaka mitatu, na hua, na mwana njiwa.
Genèse 22.13 Psaumes 50.5 Lévitique 3.1 Lévitique 1.3 Lévitique 1.10
10 Akampatia hao wote, akawapasua vipande viwili, akaweka kila kipande kuelekea mwenzake, ila ndege hakuwapasua.
Lévitique 1.17 Jérémie 34.18-34.19 2 Timothée 2.15 Genèse 15.17
11 Hata tai walipotua juu ya mizoga Abramu akawafukuza.
Matthieu 13.4 Ezéchiel 17.3 Psaumes 119.13 Ezéchiel 17.7
12 Na jua lilipokuwa likichwa usingizi mzito ulimshika Abramu, hofu ya giza kuu ikamwangukia.
Genèse 2.21 Job 33.15 Daniel 10.8-10.9 Actes 9.8-9.9 Actes 20.9
13 Bwana akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa muda wa miaka mia nne.
Actes 7.6-7.7 Galates 3.17 Lévitique 19.34 Deutéronome 10.19 Actes 7.17
14 Hata na taifa lile, watakaowatumikia, nitawahukumu; baadaye watatoka na mali mengi.
Josué 24.4-24.7 Exode 7.1-7.14 Josué 24.17 Genèse 46.1-46.34 Exode 3.21-3.22
15 Lakini wewe utakwenda kwa baba zako kwa amani, utazikwa katika uzee mwema.
Job 5.26 Genèse 25.7-25.9 Psaumes 37.37 2 Chroniques 34.28 Genèse 23.19
16 Na kizazi cha nne kitarudi hapa, maana haujatimia uovu wa Waamori bado.1 Rois 21.26 Daniel 8.23 1 Thessaloniciens 2.16 Exode 12.40 Matthieu 23.32-23.35
17 Ikawa, jua lilipokuchwa likawa giza, tazama, tanuru ya moshi na mwenge unaowaka ulipita kati ya vile vipande vya nyama.
Jérémie 34.18-34.19 Juges 6.21 1 Chroniques 21.26 2 Samuel 22.9 Exode 3.2-3.3
18 Siku ile Bwana akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,
Genèse 12.7 Néhémie 9.8 Deutéronome 1.7-1.8 Genèse 24.7 Deutéronome 34.4
19 Mkeni, na Mkenizi, na Mkadmoni,
Nombres 24.21-24.22
20 na Mhiti, na Mperizi, na Mrefai,
Genèse 14.5 Esaïe 17.5
21 na Mwamori, na Mkanaani, na Mgirgashi, na Myebusi.
Matthieu 8.28 Exode 23.23-23.28 Genèse 10.15-10.19 Deutéronome 7.1 Exode 33.2