Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 19
Bible en Swahili de l’est


1 Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, Na anga laitangaza kazi ya mikono yake. Romains 1.19-1.20 Psaumes 50.6 Psaumes 8.3 Genèse 1.14-1.15 Psaumes 148.3-148.4
2 Mchana husemezana na mchana, Usiku hutolea usiku maarifa. Psaumes 74.16 Genèse 8.22 Psaumes 136.8-136.9 Psaumes 24.7-24.10 Genèse 1.17-1.18
3 Hakuna lugha wala maneno, Sauti yao haisikilikani. Deutéronome 4.19
4 Sauti yao imeenea duniani mwote, Na maneno yao hata miisho ya ulimwengu. Katika hizo ameliwekea jua hema, Romains 10.18 Psaumes 104.2 Genèse 1.14-1.18 Malachie 4.2 Psaumes 98.3
5 Kama bwana arusi akitoka chumbani mwake, Lafurahi kama mtu aliye hodari Kwenda mbio katika njia yake. Philippiens 3.13-3.14 1 Corinthiens 9.24-9.26 Ecclésiaste 1.5 Hébreux 12.1-12.2 Esaïe 62.5
6 Kutoka kwake lautoka mwisho wa mbingu, Na kuzunguka kwake hata miisho yake, Wala kwa hari yake Hakuna kitu kilichositirika. Ecclésiaste 1.5 Colossiens 1.23 Psaumes 139.9 Job 25.3 Job 22.14
7 Sheria ya Bwana ni kamilifu, Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa Bwana ni amini, Humtia mjinga hekima. Psaumes 111.7 Psaumes 119.130 Psaumes 23.3 Psaumes 93.5 Psaumes 119.105
8 Maagizo ya Bwana ni ya adili, Huufurahisha moyo. Amri ya Bwana ni safi, Huyatia macho nuru. Psaumes 12.6 Psaumes 119.128 Psaumes 119.105 Proverbes 6.23 Romains 3.20
9 Kicho cha Bwana ni kitakatifu, Kinadumu milele. Hukumu za Bwana ni kweli, Zina haki kabisa. Psaumes 119.142 Psaumes 34.11-34.14 Psaumes 119.1 1 Samuel 12.24 Psaumes 72.1-72.2
10 Ni za kutamanika kuliko dhahabu, Kuliko wingi wa dhahabu safi. Nazo ni tamu kuliko asali, Kuliko sega la asali. Psaumes 119.127 Psaumes 119.103 Psaumes 119.72 Proverbes 8.19 Proverbes 3.13-3.15
11 Tena mtumishi wako huonywa kwazo, Katika kuzishika kuna thawabu nyingi. Proverbes 29.18 Psaumes 119.11 Matthieu 6.4 Hébreux 11.6-11.7 2 Jean 1.8
12 Ni nani awezaye kuyatambua makosa yake? Unitakase na mambo ya siri. Psaumes 90.8 Psaumes 139.23-139.24 1 Jean 1.7 Psaumes 40.12 1 Corinthiens 4.4
13 Umzuie mtumishi wako asitende mambo ya kiburi, Yasinitawale mimi. Ndipo nitakapokuwa kamili, Nami nitakuwa safi, sina kosa lililo kubwa. Psaumes 119.133 Psaumes 7.10 Romains 6.12-6.14 Genèse 20.6 Deutéronome 17.12-17.13
14 Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu, na mwokozi wangu. Psaumes 104.34 Psaumes 51.15 Job 19.25 Psaumes 119.108 Psaumes 66.18-66.20

Cette Bible est dans le domaine public.