Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 38
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Bwana, usinilaumu katika ghadhabu yako, Wala usiniadhibu kwa ukali wa hasira yako. Psaumes 6.1 Hébreux 12.5-12.11 Esaïe 54.8 Psaumes 70.1 Habakuk 3.2
2 Kwa maana mishale yako imenichoma, Na mkono wako umenipata. Psaumes 32.4 Job 6.4 Deutéronome 2.15 1 Samuel 5.6 Lamentations 3.12
3 Hamna uzima katika mwili wangu Kwa sababu ya ghadhabu yako. Wala hamna amani mifupani mwangu Kwa sababu ya hatia zangu. Psaumes 51.8 Psaumes 6.2 Lamentations 3.40-3.42 Psaumes 90.7-90.8 Job 2.7-2.8
4 Maana dhambi zangu zimenifunikiza kichwa, Kama mzigo mzito zimenilemea mno. Esdras 9.6 Psaumes 40.12 Lamentations 1.14 1 Pierre 2.24 Lévitique 7.18
5 Jeraha zangu zinanuka, zimeoza, Kwa sababu ya upumbavu wangu. Esaïe 1.5-1.6 Jérémie 8.22 Psaumes 32.3 Psaumes 69.5 Psaumes 38.7
6 Nimepindika na kuinama sana, Mchana kutwa nimekwenda nikihuzunika. Job 30.28 Psaumes 35.14 Psaumes 42.9 Psaumes 43.2 Psaumes 42.5
7 Maana viuno vyangu vimejaa homa, Wala hamna uzima katika mwili wangu. Job 30.18 Job 7.5 Psaumes 102.3 Actes 12.23 Psaumes 41.8
8 Nimedhoofika na kuchubuka sana, Nimeugua kwa fadhaa ya moyo wangu. Job 3.24 Psaumes 32.3 Job 30.28 Psaumes 22.1-22.2 Esaïe 59.11
9 Bwana, haja zangu zote ziko mbele zako, Kuugua kwangu hakukusitirika kwako. Psaumes 102.5 Psaumes 6.6 2 Corinthiens 5.2 Jean 1.48 Romains 8.26-8.27
10 Moyo wangu unapwita-pwita, Nguvu zangu zimeniacha; Nuru ya macho yangu nayo imeniondoka. Psaumes 6.7 Psaumes 69.3 Psaumes 88.9 Esaïe 21.4 Psaumes 119.123
11 Wanipendao na rafiki zangu wanasimama mbali na pigo langu; Naam, karibu zangu wamesimama mbali. Psaumes 31.11 Luc 23.49 Luc 10.31-10.32 Job 19.13-19.17 Luc 22.54
12 Nao wanaoutafuta uhai wangu hutega mitego; Nao wanaotaka kunidhuru hunena mabaya; Na kufikiri hila mchana kutwa. Psaumes 35.20 Psaumes 140.5 Psaumes 35.4 Psaumes 64.2-64.5 2 Samuel 17.1-17.3
13 Lakini kama kiziwi sisikii, Nami ni kama bubu asiyefumbua kinywa chake. Psaumes 39.2 Psaumes 39.9 Esaïe 53.7 1 Pierre 2.23 2 Samuel 16.10-16.12
14 Naam, nimekuwa kama mtu asiyesikia, Ambaye hamna hoja kinywani mwake. Michée 7.5 Jean 8.6 Amos 5.13 Marc 15.3-15.5
15 Kwa kuwa nakungoja Wewe, Bwana, Wewe utajibu, Ee Bwana, Mungu wangu. Psaumes 39.7 Psaumes 17.6 Psaumes 138.3 Psaumes 123.1-123.3
16 Maana nalisema, Wasije wakanifurahia; Mguu wangu ukiteleza wajitukuza juu yangu. Psaumes 94.18 Psaumes 35.24-35.26 Deutéronome 32.35 Psaumes 13.3-13.4
17 Kwa maana mimi ni karibu na kusita, Na maumivu yangu yako mbele yangu daima. Psaumes 35.15 Psaumes 38.6 Michée 4.6-4.7 Psaumes 6.6 Psaumes 77.2-77.3
18 Kwa maana nitaungama uovu wangu, Na kusikitika kwa dhambi zangu. Psaumes 32.5 Proverbes 28.13 Job 33.27 Job 31.33 Psaumes 51.3
19 Lakini adui zangu ni wazima wenye nguvu, Nao wanaonichukia bure wamekuwa wengi. Psaumes 35.19 Matthieu 10.22 Psaumes 56.1-56.2 Jean 15.18-15.25 Psaumes 25.19
20 Naam, wakilipa mabaya kwa mema, Huwa adui zangu kwa kuwa nalifuata lililo jema. Psaumes 35.12 1 Jean 3.12 1 Pierre 3.13 Matthieu 5.10 1 Pierre 3.17-3.18
21 Wewe, Bwana, usiniache, Mungu wangu, usijitenge nami. Psaumes 22.19 Psaumes 35.21-35.22 Psaumes 22.11 Psaumes 22.24 Psaumes 22.1
22 Ufanye haraka kunisaidia, Ee Bwana, wokovu wangu. Psaumes 40.13 Psaumes 27.1 Psaumes 40.17 Psaumes 70.5 Psaumes 70.1

Cette Bible est dans le domaine public.