Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 41
Bible en Swahili de l’est


1 Heri amkumbukaye mnyonge; Bwana atamwokoa siku ya taabu. Proverbes 14.21 Proverbes 19.17 Hébreux 6.10 2 Corinthiens 9.8-9.14 Psaumes 37.19
2 Bwana atamlinda na kumhifadhi hai, Naye atafanikiwa katika nchi; Wala usimtie katika hali wamtakiayo adui zake. Psaumes 27.12 Psaumes 33.19 Psaumes 128.1-128.6 1 Timothée 4.8 Psaumes 37.22
3 Bwana atamtegemeza alipo mgonjwa kitandani. Katika ugonjwa wake umemtandikia. Philippiens 2.26-2.27 2 Rois 20.5-20.6 Psaumes 73.26 2 Rois 1.16 2 Corinthiens 4.16-4.17
4 Nami nalisema, Bwana, unifadhili, Uniponye roho yangu maana nimekutenda dhambi. Psaumes 147.3 Psaumes 103.3 Psaumes 6.2-6.4 2 Chroniques 30.18-30.20 Psaumes 32.5
5 Adui zangu wananitaja kwa maneno mabaya, Atakufa lini, jina lake likapotea? Proverbes 10.7 Psaumes 102.8 Job 20.7 Job 18.17 Psaumes 22.6-22.8
6 Na mmoja wao akija kunitazama asema uongo, Moyo wake hujikusanyia maovu, Naye atokapo nje huyanena. Psaumes 12.2 Proverbes 26.24-26.26 Daniel 11.27 Jérémie 20.10 Luc 11.53-11.54
7 Wote wanaonichukia wananinong’ona, Wananiwazia mabaya. 2 Corinthiens 12.20 Romains 1.29 Matthieu 22.15 Psaumes 31.13 Proverbes 16.28
8 Neno la kisirani limemgandama, Na iwapo amelala hatasimama tena. Psaumes 71.11 Matthieu 27.41-27.46 Luc 13.16 Psaumes 38.3-38.7 Matthieu 27.63-27.64
9 Msiri wangu tena niliyemtumaini, Aliyekula chakula changu, Ameniinulia kisigino chake. Jean 13.18 Job 19.19 2 Samuel 15.12 Jérémie 20.10 Psaumes 55.12-55.14
10 Lakini Wewe, Bwana, unifadhili, Uniinue nipate kuwalipa. Psaumes 18.37-18.42 Psaumes 109.6-109.21 Psaumes 57.1 Psaumes 3.3 Luc 19.27
11 Kwa neno hili nimejua ya kuwa wapendezwa nami, Kwa kuwa adui yangu hasimangi kwa kunishinda. Psaumes 13.4 Psaumes 35.25 Psaumes 86.17 Psaumes 124.6 Colossiens 2.15
12 Nami katika ukamilifu wangu umenitegemeza, Umeniweka mbele za uso wako milele. Job 36.7 Psaumes 37.17 Psaumes 25.21 Jean 17.24 Psaumes 34.15
13 Na atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, Tangu milele hata milele. Amina na Amina. Ephésiens 1.3 Psaumes 106.48 Psaumes 89.52 Psaumes 72.18-72.19 Apocalypse 7.12

Cette Bible est dans le domaine public.