Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 92.8
Bible en Swahili de l’est


1 Ni neno jema kumshukuru Bwana, Na kuliimbia jina lako, Ee Uliye juu.Psaumes 147.1 Psaumes 135.3 Ephésiens 5.19 Psaumes 107.1 Daniel 4.34-4.37
2 Kuzitangaza rehema zako asubuhi, Na uaminifu wako wakati wa usiku.Lamentations 3.22-3.23 Jean 1.17 Psaumes 145.2 Psaumes 77.2 Psaumes 42.8
3 Kwa chombo chenye nyuzi kumi, Na kwa kinanda, Na kwa mlio wa kinubi.Psaumes 33.2 Néhémie 12.27 1 Chroniques 13.8 1 Samuel 10.5 1 Chroniques 15.16
4 Kwa kuwa umenifurahisha, Bwana, Kwa kazi yako; nitashangilia Kwa ajili ya matendo ya mikono yako.Esaïe 65.13-65.14 Psaumes 8.6 Luc 1.47 2 Corinthiens 2.14 Jean 16.22
5 Ee Bwana, jinsi yalivyo makuu matendo yako! Mawazo yako ni mafumbo makubwa.Esaïe 55.8-55.9 Psaumes 40.5 Romains 11.33-11.34 Psaumes 139.17 Psaumes 145.3-145.4
6 Mtu mjinga hayatambui hayo, Wala mpumbavu hayafahamu.Psaumes 73.22 Psaumes 94.8 Psaumes 49.10 1 Corinthiens 2.14 Jérémie 10.14
7 Wasio haki wakichipuka kama majani Na wote watendao maovu wakistawi. Ni kwa kusudi waangamizwe milele;Psaumes 73.18-73.20 Psaumes 37.38 1 Pierre 1.24 Job 12.6 Job 21.7-21.12
8 Bali Wewe, Bwana, U Mtukufu hata milele.Psaumes 83.18 Psaumes 93.4 Daniel 4.34-4.35 Actes 12.22-12.24 Actes 12.1
9 Maana hao adui zako, Ee Bwana, Hao adui zako watapotea, Na watendao maovu watatawanyika wote pia.Psaumes 37.20 Psaumes 89.10 Luc 21.24 Juges 5.31 Psaumes 21.8-21.9
10 Bali pembe yangu umeiinua kama pembe ya nyati, Nimepakwa mafuta mabichi.Psaumes 23.5 Psaumes 45.7 Psaumes 89.17 Nombres 23.22 2 Corinthiens 1.21
11 Na jicho langu limewatazama walioniotea, Sikio langu limesikia habari za waovu walionishambulia.Psaumes 54.7 Psaumes 91.8 Psaumes 37.34 Psaumes 59.10 Psaumes 112.8
12 Mwenye haki atasitawi kama mtende, Atakua kama mwerezi wa Lebanoni.Psaumes 1.3 Psaumes 52.8 Psaumes 104.16 Osée 14.5-14.6 Psaumes 92.7
13 Waliopandwa katika nyumba ya Bwana Watasitawi katika nyua za Mungu wetu.Psaumes 100.4 Ephésiens 3.17 Psaumes 135.2 Esaïe 60.21 Romains 11.17
14 Watazaa matunda hadi wakati wa uzee, Watajaa utomvu, watakuwa na ubichi.Esaïe 46.4 Ezéchiel 47.12 Philippiens 1.11 Jérémie 17.8 Psaumes 71.18
15 Watangaze ya kuwa Bwana ni mwenye adili, Mwamba wangu, ndani yake hamna udhalimu.Psaumes 18.2 Job 34.10 Deutéronome 32.4 Romains 9.14 Psaumes 62.6

Cette Bible est dans le domaine public.