Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 96.1
Bible en Swahili de l’est


1 Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Mwimbieni Bwana, nchi yote.Psaumes 33.3 1 Chroniques 16.23-16.33 Psaumes 98.1 Apocalypse 5.9 Psaumes 149.1
2 Mwimbieni Bwana, libarikini jina lake, Tangazeni wokovu wake siku kwa siku.Psaumes 71.15 Marc 16.15 Psaumes 40.10 Apocalypse 5.13 Romains 10.14-10.18
3 Wahubirini mataifa habari za utukufu wake, Na watu wote habari za maajabu yake.Esaïe 49.6 Luc 24.47 Zacharie 9.10 Apocalypse 14.6-14.7 Daniel 4.1-4.3
4 Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kusifiwa sana. Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote.Psaumes 18.3 Psaumes 89.7 Psaumes 95.3 Psaumes 145.3 Psaumes 66.3
5 Maana miungu yote ya watu si kitu, Lakini Bwana ndiye aliyezifanya mbingu.Psaumes 115.15 Esaïe 42.5 Jérémie 10.11-10.12 Psaumes 135.18 Psaumes 115.3-115.8
6 Heshima na adhama ziko mbele zake, Nguvu na uzuri zimo katika patakatifu pake.Psaumes 104.1 1 Chroniques 16.27 Psaumes 27.4 Psaumes 29.9 Psaumes 93.1
7 Mpeni Bwana, enyi jamaa za watu, Mpeni Bwana utukufu na nguvu.Psaumes 22.27 Psaumes 29.1-29.2 Apocalypse 5.9 Apocalypse 5.13 Apocalypse 19.6
8 Mpeni Bwana utukufu wa jina lake, Leteni sadaka mkaziingie nyua zake.Psaumes 100.4 Psaumes 45.12 Malachie 1.11 Psaumes 108.3-108.5 Hébreux 13.15-13.16
9 Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu, Tetemekeni mbele zake, nchi yote.Psaumes 29.2 Psaumes 33.8 Psaumes 114.7 Psaumes 110.3 Luc 21.5-21.6
10 Semeni katika mataifa, Bwana ametamalaki; Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike, Atawahukumu watu kwa adili.Psaumes 93.1 Psaumes 9.8 Psaumes 67.4 Psaumes 96.13-97.1 Psaumes 46.6
11 Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie, Bahari na ivume na vyote viijazavyo,Psaumes 69.34 Esaïe 49.13 Psaumes 98.7-98.9 Psaumes 97.1 Apocalypse 12.12
12 Mashamba na yashangilie, na vyote vilivyomo, Ndipo miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha;Esaïe 55.12-55.13 Psaumes 65.12-65.13 Esaïe 42.10-42.11 Esaïe 44.23 Esaïe 35.1
13 Mbele za Bwana, kwa maana anakuja, Kwa maana anakuja aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na mataifa kwa uaminifu wake.Apocalypse 19.11 Psaumes 98.9 2 Thessaloniciens 1.10 Malachie 3.1-3.2 Psaumes 96.10

Cette Bible est dans le domaine public.