Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 96
Bible en Swahili de l’est


1 Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Mwimbieni Bwana, nchi yote. Psaumes 98.1 Psaumes 33.3 1 Chroniques 16.23-16.33 Apocalypse 5.9 Psaumes 149.1
2 Mwimbieni Bwana, libarikini jina lake, Tangazeni wokovu wake siku kwa siku. Psaumes 71.15 Marc 16.15 Romains 10.14-10.18 Actes 13.26 Esaïe 52.7-52.8
3 Wahubirini mataifa habari za utukufu wake, Na watu wote habari za maajabu yake. Zacharie 9.10 Apocalypse 14.6-14.7 Daniel 4.1-4.3 Psaumes 117.1-117.2 Matthieu 28.19
4 Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kusifiwa sana. Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote. Psaumes 18.3 Psaumes 89.7 Psaumes 95.3 Psaumes 145.3 Jérémie 10.6-10.7
5 Maana miungu yote ya watu si kitu, Lakini Bwana ndiye aliyezifanya mbingu. Psaumes 115.15 Esaïe 42.5 Jérémie 10.11-10.12 Psaumes 115.3-115.8 Esaïe 44.8-44.28
6 Heshima na adhama ziko mbele zake, Nguvu na uzuri zimo katika patakatifu pake. Psaumes 104.1 Psaumes 29.9 Psaumes 93.1 Psaumes 50.2 Psaumes 8.1
7 Mpeni Bwana, enyi jamaa za watu, Mpeni Bwana utukufu na nguvu. Psaumes 22.27 Psaumes 29.1-29.2 Psaumes 66.1-66.2 Psaumes 67.3-67.4 Matthieu 6.13
8 Mpeni Bwana utukufu wa jina lake, Leteni sadaka mkaziingie nyua zake. Psaumes 100.4 Malachie 1.11 Psaumes 108.3-108.5 Hébreux 13.15-13.16 Psaumes 72.10
9 Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu, Tetemekeni mbele zake, nchi yote. Psaumes 29.2 Psaumes 33.8 Psaumes 110.3 Psaumes 114.7 Daniel 11.45
10 Semeni katika mataifa, Bwana ametamalaki; Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike, Atawahukumu watu kwa adili. Psaumes 93.1 Psaumes 9.8 Psaumes 67.4 Esaïe 11.3-11.5 Psaumes 2.8-2.12
11 Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie, Bahari na ivume na vyote viijazavyo, Psaumes 69.34 Esaïe 49.13 Psaumes 97.1 Psaumes 98.7-98.9 Luc 2.10
12 Mashamba na yashangilie, na vyote vilivyomo, Ndipo miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha; Esaïe 55.12-55.13 Esaïe 44.23 Esaïe 35.1 Psaumes 65.12-65.13 Esaïe 42.10-42.11
13 Mbele za Bwana, kwa maana anakuja, Kwa maana anakuja aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na mataifa kwa uaminifu wake. Apocalypse 19.11 Psaumes 98.9 Psaumes 96.10 2 Timothée 4.8 2 Pierre 3.12-3.14

Cette Bible est dans le domaine public.