7 Kisha, wakuu wote wa majeshi waliokuwa katika bara, wao na watu wao, waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemweka Gedalia, mwana wa Ahikamu, kuwa liwali juu ya nchi, na kwamba amemkabidhi wanaume na wanawake na watoto, na baadhi ya maskini wa nchi wasiochukuliwa mateka Babeli; Jérémie 39.10 2 Rois 25.22-25.26 Ezéchiel 45.16 Jérémie 39.4 Ezéchiel 33.24-33.29 8 ndipo wakamwendea Gedalia huko Mizpa; nao ni hawa, Ishmaeli, mwana wa Nethania, na Yohana na Yonathani, wana wa Karea, na Seraya, mwana wa Tanhumethi, na wana wa Efai, Mnetofa, na Yezania, mwana wa Mmaaka, wao na watu wao. Jérémie 42.1 Deutéronome 3.14 2 Samuel 10.6 Josué 12.5 2 Samuel 10.8 9 Na Gedalia, mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, akawaapia wao na watu wao, akisema, Msiogope kuwatumikia Wakaldayo; kaeni katika nchi, mkamtumikie mfalme wa Babeli; nayo itawafaa. Jérémie 27.11 1 Samuel 20.16-20.17 2 Rois 25.24 Jérémie 38.17-38.20 Genèse 49.15 10 Na mimi, tazama, nitakaa Mizpa, ili nisimame mbele ya Wakaldayo watakaotujilia; lakini ninyi chumeni divai, na matunda ya wakati wa jua, na mafuta, mkaviweke vitu hivyo katika vyombo vyenu, mkakae katika miji yenu mliyoitwaa. Jérémie 40.12 Jérémie 35.19 Jérémie 48.32 Jérémie 39.10 Deutéronome 1.38 11 Kadhalika waliposikia Wayahudi wote, waliokuwa katika Moabu, na kati ya wana wa Amoni, na hao waliokuwa katika Edomu, na hao waliokuwa katika nchi zote, ya kuwa mfalme wa Babeli amewaachia Yuda mabaki, na ya kuwa amemweka Gedalia, mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, juu yao; Esaïe 16.4 Ezéchiel 25.6 Ezéchiel 5.12 Ezéchiel 35.15 1 Samuel 12.12 12 basi, Wayahudi wote wakarudi kutoka kila mahali walikofukuzwa wakaenda mpaka nchi ya Yuda, wakamwendea Gedalia huko Mizpa, wakakusanya divai, na matunda ya wakati wa jua mengi sana. Jérémie 43.5 13 Tena Yohana, mwana wa Karea, na wakuu wote wa majeshi ya barani, wakamwendea Gedalia huko Mizpa, Jérémie 42.1 Jérémie 40.8 14 wakamwambia, Je! Una habari wewe ya kuwa Baalisi, mfalme wa wana wa Amoni, amemtuma Ishmaeli mwana wa Nethania, akuue? Lakini Gedalia, mwana wa Ahikamu, hakusadiki neno hili. Jérémie 41.10 2 Samuel 10.1-10.6 Jérémie 25.21 1 Samuel 11.1-11.3 Jérémie 49.1-49.6 15 Basi, Yohana, mwana wa Karea, akamwambia Gedalia huko Mizpa kwa siri, akisema, Niache niende nikampige Ishmaeli, mwana wa Nethania, wala hapana mtu atakayejua jambo hili; kwani akuue wewe, hata wakatawanyike Wayahudi waliokukusanyikia, na mabaki ya Yuda wakaangamie? 2 Samuel 21.17 1 Samuel 26.8 2 Samuel 18.3 Jérémie 42.2 Jérémie 12.3-12.4 16 Lakini Gedalia, mwana wa Ahikamu, akamwambia Yohana, mwana wa Karea, Usilitende jambo hili, maana unamsingizia Ishmaeli. Matthieu 10.16-10.17 Jérémie 41.2 Romains 3.8