Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Ezéchiel 25
Bible en Swahili de l’est


1 Neno la Bwana likanijia, kusema, 2 Mwanadamu, uwaelekezee wana wa Amoni uso wako, ukatabiri juu yao. Jérémie 49.1-49.6 Amos 1.13-1.15 Ezéchiel 6.2 Genèse 19.38 Jérémie 27.3
3 Uwaambie hao wana wa Amoni, Lisikieni neno la Bwana MUNGU; Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu umesema, Aha! Juu ya patakatifu pangu, palipotiwa unajisi; na juu ya nchi ya Israeli, ilipoharibiwa; na juu ya nyumba ya Israeli, walipokwenda kifungoni; Ezéchiel 36.2 Proverbes 17.5 Psaumes 70.2-70.3 Michée 7.8 Proverbes 24.17-24.18
4 basi, kwa sababu hiyo, nitakutia katika mikono ya wana wa mashariki uwe milki yao, nao wataweka marago yao ndani yako, kufanya maskani zao ndani yako; watakula matunda yako, na kunywa maziwa yako. Deutéronome 28.33 Juges 6.33 Deutéronome 28.51 1 Rois 4.30 Esaïe 1.7
5 Nami nitafanya Raba kuwa banda la ngamia, na wana wa Amoni kuwa mahali pa kulaza makundi; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. Ezéchiel 21.20 2 Samuel 12.26 Esaïe 17.2 Ezéchiel 25.8 Ezéchiel 35.9
6 Maana Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu umepiga makofi, na kupiga mshindo kwa miguu yako, na kufurahi juu ya nchi ya Israeli, jeuri yote ya roho yako; Abdias 1.12 Sophonie 2.8 Sophonie 2.10 Ezéchiel 25.15 Nahum 3.19
7 basi, tazama, nimenyosha mkono wangu juu yako, nami nitakutoa uwe mateka ya mataifa; nami nitakukatilia mbali na kabila za watu, nami nitakuangamiza, usiwe katika nchi hizo; nitakukomesha; nawe utajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. Sophonie 1.4 Ezéchiel 25.16 Ezéchiel 25.13 Jérémie 49.2 Ezéchiel 35.3
8 Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu Moabu na Seiri husema, Tazama, nyumba ya Israeli ni sawasawa na mataifa yote; Jérémie 48.1-48.47 Esaïe 15.1-15.9 Jérémie 25.21 Esaïe 34.1-34.17 Ezéchiel 35.1-35.15
9 basi, tazama, nitawafunulia wana wa mashariki ubavu wa Moabu toka miji yake, toka miji yake iliyo mipakani mwake, utukufu wa nchi hiyo, Beth-yeshimothi, na Baal-meoni, na Kiriathaimu, Josué 13.17 Jérémie 48.23 Nombres 32.37-32.38 Josué 13.19-13.20 Jérémie 48.1
10 pamoja na wana wa Amoni, nami nitawatoa kuwa milki, ili wana wa Amoni wasikumbukwe kati ya mataifa, Ezéchiel 21.32 Esaïe 23.16 Ezéchiel 25.4 Psaumes 83.3-83.6
11 nami nitatoa hukumu juu ya Moabu; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. Ezéchiel 5.10 Ezéchiel 30.19 Jérémie 48.1-48.47 Jérémie 25.21 Jérémie 9.25-9.26
12 Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa Edomu wametenda kinyume cha nyumba ya Yuda, kwa kujilipiza kisasi, nao wamekosa sana, na kujilipiza kisasi juu yao; Psaumes 137.7 Jérémie 49.7-49.22 Abdias 1.10-1.16 Ezéchiel 25.8 Amos 1.11-1.12
13 kwa sababu hiyo, Bwana MUNGU asema hivi; Nitanyosha mkono wangu juu ya Edomu, nitakatilia mbali nayo wanadamu na wanyama; nami nitaifanya kuwa ukiwa toka Temani; na mpaka Dedani wataanguka kwa upanga. Malachie 1.3-1.4 Ezéchiel 29.8 Jérémie 25.23 Jérémie 49.7-49.8 Esaïe 34.1-34.17
14 Nami nitaweka kisasi changu juu ya Edomu, kwa mkono wa watu wangu Israeli; nao watatenda mambo katika Edomu, kwa kadiri ya hasira yangu, na ghadhabu yangu, nao watakijua kisasi changu, asema Bwana MUNGU. Esaïe 11.14 Deutéronome 32.35-32.36 Apocalypse 6.16-6.17 Hébreux 10.30-10.31 Genèse 27.29
15 Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa Wafilisti wametenda mambo kwa kujilipiza kisasi, nao wamejilipiza kisasi kwa jeuri ya roho, ili kupaangamiza kwa uadui wa daima; Esaïe 14.29-14.31 Ezéchiel 25.6 Ezéchiel 25.12 Jérémie 25.20 2 Chroniques 28.18
16 kwa sababu hiyo, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitanyosha mkono wangu juu ya Wafilisti, nami nitawakatilia mbali Wakerethi, na kuwaharibu wabakio pande za pwani. 1 Samuel 30.14 Ezéchiel 25.13 Ezéchiel 25.7 Jérémie 47.1-47.7 2 Samuel 15.18
17 Nami nitajilipiza kisasi kikuu, nikiwakemea kwa ukali; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapojilipiza kisasi juu yao. Ezéchiel 25.11 Ezéchiel 25.14 Psaumes 9.16 Ezéchiel 5.15 Ezéchiel 25.5

Cette Bible est dans le domaine public.