1 Nalimwona Bwana akisimama karibu na madhabahu; akasema, vipigo vichwa vya nguzo, hata vizingiti vitikisike; vivunje vipande vipande juu ya kichwa cha kila mmoja wao; nami nitamwua mtu wa mwisho wao kwa upanga; hapana hata mmoja wao atakayekimbia, wala hataokoka hata mmoja wao.
Psaumes 68.21 Jean 1.18 Esaïe 6.3-6.4 Amos 3.14 Habakuk 3.13
2 Wajapochimba waingie katika kuzimu, mkono wangu utawatoa huko; nao wajapopanda hata mbinguni, nitawatelemsha toka huko.
Abdias 1.4 Jérémie 51.53 Psaumes 139.7-139.10 Luc 10.18 Esaïe 14.13-14.16
3 Nao wajapojificha katika kilele cha Karmeli, nitawatafuta na kuwatoa toka huko; na wajapositirika katika vilindi vya bahari nisiwaone, nitamwagiza joka huko, naye atawauma.
Jérémie 16.16 Esaïe 27.1 Job 34.22 Psaumes 139.9-139.11 Jérémie 23.23-23.24
4 Nao wajapokwenda hali ya kufungwa mbele ya adui zao, nitauagiza upanga huko, nao utawaua; nami nitawaelekezea macho yangu niwatende mabaya, wala si mema.
Jérémie 21.10 Jérémie 44.11 Lévitique 26.33 Ezéchiel 5.12 Lévitique 17.10
5 Kwa maana Bwana, MUNGU wa majeshi, ndiye aigusaye nchi, nayo ikayeyuka, na wote wakaao ndani yake wataomboleza; nayo itainuka yote pia kama Mto, nayo itakupwa tena kama Mto wa Misri.
Amos 8.8 Psaumes 46.6 Psaumes 144.5 Esaïe 64.1 Psaumes 93.3-93.4
6 Yeye ndiye avijengaye vyumba vyake mbinguni, na kuweka misingi ya kuba yake juu ya nchi; yeye ndiye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; Bwana ndilo jina lake.
Amos 5.8 Psaumes 104.3 Amos 4.13 Psaumes 104.13 Jérémie 5.22
7 Je! Ninyi si kama wana wa Wakushi kwangu mimi, enyi wana wa Israeli, asema Bwana? Je! Mimi sikuwapandisha Israeli toka nchi ya Misri, na Wafilisti toka Kaftori, na Washami toka Kiri?
Amos 1.5 Jérémie 47.4 Deutéronome 2.23 2 Rois 16.9 Amos 2.10
8 Angalieni, macho ya Bwana MUNGU yanauangalia ufalme wenye dhambi, nami nitauangamiza utoke juu ya uso wa dunia; lakini sitaiangamiza kabisa nyumba ya Yakobo, asema Bwana.Jérémie 30.11 Jérémie 5.10 Amos 9.4 Jérémie 44.27 Jérémie 31.35-31.36
9 Kwa maana, angalieni, nitatoa amri, nami nitaipepeta nyumba ya Israeli katika mataifa yote, kama vile ngano ipepetwavyo katika ungo lakini hata chembe moja iliyo ndogo haitaanguka chini.
Luc 22.31 Lévitique 26.33 Esaïe 30.28 Deutéronome 28.64
10 Wenye dhambi wote katika watu wangu watakufa kwa upanga, hao wasemao, Mabaya hayatatupata nyuma wala mbele.
Amos 6.3 Esaïe 33.14 Jérémie 18.18 Psaumes 10.11 Zacharie 13.8-13.9
11 Siku hiyo nitaiinua tena maskani ya Daudi iliyoanguka, na kuziba mahali palipobomoka; nami nitayainua magofu yake, na kuyajenga kama siku za kale;
Actes 15.15-15.17 Psaumes 80.12 Esaïe 16.5 Jérémie 46.26 Job 1.10
12 wapate kuyamiliki mabaki ya Edomu, na mataifa yote yaitwayo kwa jina langu, asema Bwana, afanyaye hayo.
Esaïe 43.7 Esaïe 11.14 Esaïe 14.1-14.2 Malachie 1.4 Genèse 27.29
13 Angalieni, siku zinakuja, asema Bwana, ambazo huyo alimaye atamfikilia avunaye, na yeye akanyagaye zabibu atamfikilia apandaye mbegu; nayo milima itadondoza divai tamu, na vilima vyote vitayeyuka.
Joël 3.18 Lévitique 26.5 Jean 4.35 Joël 3.20 Juges 5.5
14 Nami nitawarejeza tena watu wangu Israeli waliohamishwa, nao wataijenga miji iliyoachwa maganjo, na kukaa ndani yake; nao watapanda mizabibu katika mashamba, na kunywa divai yake; nao watafanyiza bustani, na kula matunda yake.
Jérémie 30.18 Esaïe 61.4 Jérémie 30.3 Esaïe 65.21 Jérémie 31.28
15 Nami nitawapanda katika nchi yao, wala hawatang’olewa tena watoke katika nchi yao niliyowapa, asema Bwana, Mungu wako.
Jérémie 24.6 Ezéchiel 34.28 Ezéchiel 37.25 Esaïe 60.21 Joël 3.20