Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Nahum 2
Bible en Swahili de l’est


1 Yeye asetaye vipande vipande amepanda juu mbele ya uso wako; zishike silaha, ilinde njia, vitie nguvu viuno vyako, uongeze uwezo wako sana. Jérémie 51.20-51.23 Jérémie 46.3-46.10 Nahum 3.14-3.15 Jérémie 25.9 Esaïe 14.6
2 Kwa maana Bwana anairudisha fahari ya Yakobo, kama fahari ya Israeli; maana watekao nyara wamewateka, na kuyaharibu matawi ya mizabibu yao. Psaumes 80.12-80.13 Sophonie 3.11 Osée 10.1 Jérémie 25.29 Genèse 49.22-49.23
3 Ngao ya mashujaa wake imefanywa kuwa nyekundu, watu walio hodari wa vita wamevaa nguo nyekundu sana; magari ya vita yametameta kwa chuma cha pua siku ya kujitengeza kwake, na mikuki inatikiswa kwa namna ya kutisha. Ezéchiel 23.14-23.15 Esaïe 63.1-63.3 Apocalypse 6.4 Esaïe 14.8 Apocalypse 12.3
4 Magari ya vita yanafanya mshindo njiani, Yanasongana-songana katika njia kuu; Kuonekana kwake ni kama mienge, Yanakwenda upesi kama umeme. Jérémie 4.13 Nahum 3.2-3.3 Ezéchiel 26.10 Esaïe 66.15 Daniel 11.40
5 Awakumbuka watu wake wenye heshima; Wanajikwaa katika mwendo wao; Wanafanya haraka waende ukutani; Nacho kitu cha kuwafunika kimewekwa tayari. Jérémie 46.12 Jérémie 51.27-51.28 Esaïe 21.5 Esaïe 5.27 Nahum 3.18
6 Malango ya mito yamefunguka, na jumba la mfalme limeyeyushwa. Esaïe 45.1-45.2 2 Pierre 3.10-3.11
7 Husabu naye amefunuliwa, anachukuliwa, na wajakazi wake wanalia kama kwa sauti ya hua, wakipiga-piga vifua vyao. Esaïe 59.11 Esaïe 38.14 Luc 23.27 Luc 23.48 Esaïe 32.12
8 Lakini Ninawi tokea zamani amekuwa kama ziwa la maji; ila hata sasa wanakimbia; Simameni! Simameni! Lakini hapana hata mmoja atazamaye nyuma. Esaïe 13.14 Genèse 10.11 Jérémie 46.5 Apocalypse 17.1 Apocalypse 17.15
9 Chukueni nyara za fedha; Chukueni nyara za dhahabu; Kwa maana ni akiba isiyoisha, Fahari ya vyombo vipendezavyo. Nahum 2.12-2.13 Esaïe 33.4 Jérémie 25.34 Ezéchiel 26.12 Daniel 11.8
10 Amekuwa utupu, na ukiwa, na uharibifu; hata moyo unayeyuka, na magoti yanagongana-gongana; viunoni mwote mna utungu, na nyuso za wote zimekuwa nyeupe kwa hofu. Psaumes 22.14 Joël 2.6 Sophonie 2.13-2.15 Esaïe 24.1 Esaïe 21.3
11 Kao la simba li wapi? Na mahali walishapo wana-simba pa wapi, mahali walipotembea simba mume na simba mke na mwana-simba, wala hapana aliyewatia hofu? Esaïe 5.29 Jérémie 2.15 Jérémie 4.7 Job 4.10-4.11 Sophonie 3.3
12 Simba alirarua vipande vipande chakula cha kuwatosha watoto wake, aliwasongea wake zake nyama, aliyajaza mapango yake mateka, na makao yake aliyajaza mawindo. Jérémie 51.34 Esaïe 10.6-10.14 Psaumes 17.12
13 Tazama, mimi ni juu yako, asema Bwana wa majeshi, nami nitayateketeza magari yako ya vita katika moshi, na upanga utawala wana-simba wako; nami nitayakatilia mbali mawindo yako katika nchi, na sauti za wajumbe wako hazitasikiwa tena kamwe. 2 Rois 19.23 Nahum 3.5 Psaumes 46.9 Jérémie 21.13 2 Rois 19.9

Cette Bible est dans le domaine public.