Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Romains 16
Bible en Swahili de l’est


1 Namkabidhi kwenu Fibi, ndugu yetu, aliye mhudumu wa kanisa lililoko Kenkrea; Actes 18.18 2 Corinthiens 3.1 1 Timothée 5.2 Marc 10.30 Matthieu 12.50
2 kwamba mmpokee katika Bwana, kama iwapasavyo watakatifu; mkamsaidie katika neno lo lote atakalohitaji kwenu; kwa sababu yeye naye amekuwa msaidizi wa watu wengi, akanisaidia mimi pia. Philippiens 2.29 2 Timothée 1.18 Actes 9.36 Romains 16.9 Romains 16.23
3 Nisalimieni Priska na Akila, watenda kazi pamoja nami katika Kristo Yesu; Actes 18.2-18.17 Actes 18.26 1 Corinthiens 16.16 Romains 16.9 2 Timothée 4.19
4 waliokuwa tayari hata kukatwa kichwa kwa ajili ya maisha yangu; ambao ninawashukuru, wala si mimi tu, ila na makanisa ya Mataifa yote pia; nisalimieni na kanisa lililomo katika nyumba yao. Actes 16.5 1 Corinthiens 7.17 1 Thessaloniciens 2.14 Apocalypse 1.4 Romains 5.7
5 Nisalimieni Epaineto, mpenzi wangu, aliye malimbuko ya Asia kwa Kristo. 1 Corinthiens 16.19 1 Corinthiens 16.15 Colossiens 4.15 Philémon 1.2 Apocalypse 14.4
6 Nisalimieni Mariamu, aliyejitaabisha sana kwa ajili yenu. Romains 16.12 Matthieu 27.55 1 Timothée 5.10
7 Nisalimieni Androniko na Yunia, jamaa zangu, waliofungwa pamoja nami, ambao ni maarufu miongoni mwa mitume; nao walikuwa katika Kristo kabla yangu. Romains 16.11 Romains 16.21 Philémon 1.23 Colossiens 4.10 2 Corinthiens 5.17
8 Nisalimieni Ampliato, mpenzi wangu katika Bwana. Romains 16.5 Philippiens 4.1 1 Jean 3.14
9 Nisalimieni Urbano, mtenda kazi pamoja nami katika Kristo, na Stakisi, mpenzi wangu. Romains 16.2-16.3 Romains 16.21
10 Nisalimieni Apele, mwenye kukubaliwa katika Kristo. Nisalimieni watu wa nyumbani mwa Aristobulo. 1 Timothée 3.10 2 Corinthiens 8.22 1 Pierre 1.7 Romains 14.18 Deutéronome 8.2
11 Nisalimieni Herodioni, jamaa yangu. Nisalimieni watu wa nyumbani mwa Narkiso, walio katika Bwana. Romains 16.7 Romains 16.21
12 Nisalimieni Trifaina na Trifosa, wenye bidii katika Bwana. Nisalimieni Persisi, mpenzi aliyejitahidi sana katika Bwana. 1 Timothée 5.17-5.18 1 Timothée 4.10 Hébreux 6.10-6.11 1 Thessaloniciens 5.12-5.13 1 Corinthiens 16.16
13 Nisalimieni Rufo, mteule katika Bwana, na mamaye, aliye mama yangu pia. Marc 15.21 Jean 15.16 Matthieu 12.49-12.50 2 Jean 1.1 1 Timothée 5.2
14 Nisalimieni Asinkrito, Flegoni, Herme, Patroba, Herma, na ndugu walio pamoja nao. Romains 8.29 1 Pierre 1.22-1.23 Colossiens 1.2 Hébreux 3.1
15 Nisalimieni Filologo na Yulia, Nerea na dada yake, na Olimpa, na watakatifu wote walio pamoja nao. Romains 16.2 Esaïe 60.21 Romains 16.14 1 Pierre 1.2 Ephésiens 1.1
16 Salimianeni kwa busu takatifu. Makanisa yote ya Kristo yawasalimu. 1 Corinthiens 16.20 1 Thessaloniciens 5.26 2 Corinthiens 13.12 1 Pierre 5.14 Actes 20.37
17 Ndugu zangu, nawasihi, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao. 2 Thessaloniciens 3.6 1 Timothée 6.3-6.5 2 Timothée 3.5 1 Timothée 1.3 Matthieu 18.7
18 Kwa sababu walio hivyo hawamtumikii Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wanyofu. Colossiens 2.4 Michée 3.5 Philippiens 3.19 2 Pierre 2.3 1 Timothée 6.5
19 Maana utii wenu umewafikilia watu wote; basi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya. Matthieu 10.16 1 Corinthiens 14.20 Romains 1.8 Jacques 3.13-3.18 Philippiens 2.15
20 Naye Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi. [Amina.] Genèse 3.15 Romains 15.33 Luc 10.19 1 Thessaloniciens 5.28 1 Jean 3.8
21 Timotheo, mtenda kazi pamoja nami, awasalimu, na Lukio, na Yasoni, na Sosipatro, jamaa zangu. Actes 20.4 Actes 13.1 Actes 17.5 Romains 16.11 Romains 16.7
22 Mimi Tertio, niliyeandika waraka huu, nawasalimu katika Bwana. Galates 6.11 1 Corinthiens 16.21 Romains 16.8 Colossiens 3.17
23 Gayo, mwenyeji wangu na wa Kanisa lote pia awasalimu. Erasto, wakili wa mji, awasalimu, na Kwarto, ndugu yetu. 1 Corinthiens 1.14 Actes 19.22 3 Jean 1.1-1.6 2 Timothée 4.20 Actes 19.29
24 Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi nyote. Amina.] 25 Sasa na atukuzwe yeye awezaye kuwafanya imara, sawasawa na injili yangu na kwa kuhubiriwa kwake Yesu Kristo, sawasawa na ufunuo wa ile siri iliyositirika tangu zamani za milele, 1 Corinthiens 2.7 Romains 2.16 Ephésiens 1.9 Amos 3.7 Ephésiens 3.3-3.5
26 ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulikana na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, ili waitii Imani. Romains 1.5 Romains 1.2 Colossiens 1.26 2 Timothée 1.10 1 Timothée 1.17
27 Ndiye Mungu mwenye hekima peke yake. Utukufu una yeye kwa Yesu Kristo, milele na milele. Amina. Romains 11.36 Apocalypse 7.10-7.12 1 Timothée 1.17 1 Pierre 5.10-5.11 Apocalypse 1.5-1.6

Cette Bible est dans le domaine public.