Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Apocalypse 5.11
Bible en Swahili de l’est


1 Kisha nikaona katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa muhuri saba.Ezéchiel 2.9-2.10 Esaïe 29.11 Apocalypse 5.7 Apocalypse 6.1 Daniel 12.4-12.9
2 Nikaona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kuu, N’nani astahiliye kukifungua kitabu, na kuzivunja muhuri zake?Esaïe 41.22-41.23 Esaïe 29.11-29.12 Apocalypse 18.21 Apocalypse 5.5 Psaumes 103.20
3 Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama.Apocalypse 5.13 Romains 11.34 Esaïe 40.13-40.14 Esaïe 41.28
4 Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama.Daniel 12.8-12.9 Apocalypse 4.1
5 Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba.Esaïe 11.1 Romains 15.12 Apocalypse 22.16 Esaïe 11.10 Romains 1.3
6 Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.Zacharie 4.10 Jean 1.29 Zacharie 3.9 Apocalypse 5.12 Apocalypse 13.8
7 Akaja, akakitwaa kile kitabu katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi.Apocalypse 5.1 Apocalypse 4.2-4.3
8 Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu.Apocalypse 5.14 Psaumes 141.2 Apocalypse 8.3-8.4 Apocalypse 14.2-14.3 Apocalypse 4.10
9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,Apocalypse 14.6 1 Pierre 1.18-1.19 Apocalypse 5.6 1 Corinthiens 6.20 Psaumes 33.3
10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.Apocalypse 1.6 Apocalypse 20.6 Apocalypse 22.5 Daniel 7.27 Exode 19.6
11 Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu,Daniel 7.10 Hébreux 12.22 Apocalypse 4.4 Apocalypse 19.6 Psaumes 68.17
12 wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka.Apocalypse 4.11 Matthieu 28.18 Apocalypse 5.9 Zacharie 13.7 Philippiens 2.9-2.11
13 Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele.Philippiens 2.10 Apocalypse 5.3 Apocalypse 5.12 Apocalypse 6.16 Romains 11.36
14 Na wale wenye uhai wanne wakasema, Amina. Na wale wazee wakaanguka, wakasujudu.Apocalypse 19.4 Apocalypse 5.8 Apocalypse 7.12 Apocalypse 4.9-4.11 Apocalypse 5.6

Cette Bible est dans le domaine public.