Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Genèse 16.15
Bible en Swahili de l’est


1 Basi Sarai mkewe Abramu hakumzalia mwana, naye alikuwa na mjakazi, Mmisri, jina lake Hajiri.Galates 4.24 Genèse 21.21 Genèse 12.16 Genèse 15.2-15.3 Luc 1.36
2 Sarai akamwambia Abramu, Basi sasa, Bwana amenifunga tumbo nisizae, umwingilie mjakazi wangu labda nitapata uzao kwa yeye. Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai.Genèse 30.9-30.10 Genèse 17.16 Genèse 20.18 Genèse 3.1-3.6 Genèse 30.22
3 Sarai mkewe Abramu akamtwaa Hajiri Mmisri mjakazi wake, baada ya kukaa Abramu katika nchi ya Kanaani miaka kumi, akampa Abramu mumewe, awe mkewe.Genèse 12.4-12.5 Genèse 16.5 Genèse 30.4 Genèse 35.22 Juges 19.1-19.4
4 Basi akamwingilia Hajiri, naye akapata mimba. Naye alipoona ya kwamba amepata mimba, bibi yake alikuwa duni machoni pake.1 Corinthiens 4.6 1 Samuel 1.6-1.8 1 Corinthiens 13.4-13.5 2 Samuel 6.16 Proverbes 30.23
5 Sarai akamwambia Abramu, Ubaya ulionipata na uwe juu yako; nimekupa mjakazi wangu kifuani mwako, naye alipoona kwamba amepata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake. Bwana na ahukumu kati ya mimi na wewe.Genèse 31.53 Exode 5.21 Luc 10.40-10.41 1 Samuel 24.12-24.15 2 Chroniques 24.22
6 Naye Abramu akamwambia Sarai, Tazama, mjakazi wako yu mkononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake.Proverbes 15.17-15.18 Psaumes 106.41-106.42 Job 2.6 Jérémie 38.5 Ecclésiaste 10.4
7 Malaika wa Bwana akamwona kwenye chemchemi ya maji katika jangwa, chemchemi iliyoko katika njia ya kuendea Shuri.Genèse 25.18 Exode 15.22 Genèse 31.11 Genèse 22.11 Proverbes 15.3
8 Akamwambia, Hajiri, wewe mjakazi wa Sarai, unatoka wapi, nawe unakwenda wapi? Akanena, Nakimbia mimi kutoka mbele ya bibi yangu Sarai.Genèse 3.9 Genèse 4.10 Ecclésiaste 10.4 1 Samuel 26.19 Ephésiens 6.5-6.8
9 Malaika wa Bwana akamwambia, Rudi kwa bibi yako, ukanyenyekee chini ya mikono yake.1 Pierre 5.5-5.6 Ephésiens 5.21 Tite 2.9 1 Pierre 2.18-2.25 Ecclésiaste 10.4
10 Malaika wa Bwana akamwambia, Hakika nitauzidisha uzao wako, wala hautahesabika kwa jinsi utakavyokuwa mwingi.Genèse 17.20 Genèse 21.13 Genèse 22.15-22.18 Genèse 25.12-25.18 Esaïe 63.9
11 Malaika wa Bwana akamwambia, Tazama! Wewe una mimba, utazaa mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Ishmaeli, maana Bwana amesikia kilio cha mateso yako.Exode 3.7 Exode 2.23-2.24 Exode 3.9 Luc 1.13 Esaïe 7.14
12 Naye atakuwa kama punda-mwitu kati ya watu, mkono wake utakuwa juu ya watu wote na mkono wa watu wote utakuwa juu yake, naye atakaa mbele yao ndugu zake wote.Genèse 25.18 Job 39.5-39.8 Genèse 21.20 Job 11.12 Genèse 27.40
13 Akaliita jina la Bwana aliyesema naye, Wewe U Mungu uonaye, kwani alisema, Hata hapa nimemwona yeye anionaye?Genèse 32.30 Psaumes 139.1-139.12 Proverbes 5.21 Proverbes 15.3 Genèse 16.7
14 Kwa hiyo kisima kile kiliitwa Beer-lahai-roi.Tazama,kiko kati ya kadeshi na beredi.Nombres 13.26 Genèse 24.62 Genèse 25.11 Genèse 21.31 Genèse 14.7
15 Hajiri akamzalia Abramu mwana wa kiume; Abramu akamwita jina lake Ishmaeli, yule mwanawe, ambaye Hajiri alimzaa.Genèse 25.12 1 Chroniques 1.28 Genèse 17.20 Genèse 17.25-17.26 Genèse 28.9
16 Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka themanini na sita, hapo Hajiri alipomzalia Abramu Ishmaeli.

Cette Bible est dans le domaine public.