Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

2 Samuel 8.2
Bible en Swahili de l’est


1 Ikawa baadaye, Daudi akawapiga Wafilisti, akawashinda; Daudi akautwaa Gathi na vijiji vyake mikononi mwa hao Wafilisti.1 Chroniques 18.1-18.17 2 Samuel 2.24 2 Samuel 21.15-21.22 2 Samuel 7.9
2 Akapiga Moabu, akawapima kwa kamba hali wamelazwa chini; akapima kamba mbili za kuuawa, na kamba moja nzima ya kuhifadhi hai. Wamoabi wakawa watumwa wa Daudi, wakaleta zawadi.Nombres 24.17 2 Samuel 8.6 1 Samuel 10.27 Psaumes 60.8 2 Samuel 8.12-8.14
3 Tena Daudi akampiga Hadadezeri mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba, alipokwenda kujipatia tena mamlaka yake huko Mtoni.1 Samuel 14.47 2 Samuel 10.19 2 Samuel 10.16 2 Samuel 10.6 1 Chroniques 18.3
4 Daudi akampokonya wapanda farasi elfu na mia saba na askari waliokwenda kwa miguu ishirini elfu; Daudi akawakata mshipa farasi wote wa magari, ila farasi wa magari mia akawasaza.Josué 11.6 Josué 11.9 Deutéronome 17.16 Psaumes 33.16-33.17 1 Rois 10.26
5 Na Washami wa Dameski walipokuja kumsaidia Hadadezeri, mfalme wa Soba, Daudi akawapiga wa Washami watu ishirini na mbili elfu.1 Rois 11.23-11.25 Job 9.13 2 Samuel 8.3 Psaumes 83.4-83.8 Esaïe 7.8
6 Daudi akaweka ngome katika Shamu ya Dameski, na hao Washami wakawa watumwa wa Daudi, wakaleta zawadi. Naye Bwana akampa Daudi kushinda kila alikokwenda.2 Samuel 8.14 2 Samuel 7.9 Psaumes 5.11-5.12 Psaumes 18.34-18.46 2 Samuel 23.14
7 Tena Daudi akazitwaa ngao za dhahabu zilizovaliwa na watumwa wa Hadadezeri, akazileta Yerusalemu.1 Chroniques 18.7 2 Chroniques 9.15-9.16 1 Rois 14.26-14.27 1 Rois 10.16-10.17
8 Tena toka Tebhathi na toka Berothai, miji ya Hadadezeri, Daudi akatwaa shaba nyingi mno.1 Chroniques 18.8 Ezéchiel 47.16 2 Chroniques 4.1-4.18 1 Chroniques 22.16 1 Chroniques 22.14
9 Na Tou, mfalme wa Hamathi, aliposikia ya kwamba Daudi amewapiga jeshi lote la Hadadezeri,1 Rois 8.65 1 Chroniques 18.9 Amos 6.2 2 Chroniques 8.4
10 Tou akamtuma kwa Daudi Hadoramu mwanawe kusalimia, na kumbarikia, kwa sababu amepigana na Hadadezeri, na kumpiga; kwa maana Hadadezeri alikuwa amepigana vita juu ya Tou. Na mkononi mwake akaleta vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na vyombo vya shaba;Psaumes 129.8 1 Chroniques 18.10 1 Samuel 13.10 1 Rois 1.47 Genèse 43.27
11 hivi pia mfalme Daudi akavifanya wakfu kwa Bwana, pamoja na hiyo fedha, na dhahabu alizofanya wakfu za mataifa yote aliowashinda;1 Rois 7.51 1 Chroniques 29.2 1 Chroniques 26.26-26.28 1 Chroniques 18.11 1 Chroniques 22.14-22.16
12 za Edomu, na za Moabu, na za wana wa Amoni, na za Wafilisti, na za Amaleki, na za nyara za Hadadezeri, mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba.2 Samuel 10.14 2 Samuel 8.2 1 Chroniques 18.11 2 Samuel 5.17-5.25 1 Samuel 27.8
13 Basi Daudi akajipatia jina, aliporudi kutoka kuwapiga Waedomi katika Bonde la Chumvi, watu kumi na nane elfu.2 Rois 14.7 2 Samuel 7.9 1 Chroniques 18.12 Psaumes 60.1 2 Chroniques 25.11
14 Akaweka askari wenye kulinda ngome katika Edomu; katikati ya Edomu yote akaweka ngome, na Waedomi wote wakawa watumwa wa Daudi. Naye Bwana akampa Daudi kushinda kila alikokwenda.Genèse 27.29 Genèse 25.23 2 Samuel 8.6 1 Chroniques 18.13 Psaumes 60.8-60.9
15 Daudi akatawala juu ya Israeli wote; naye Daudi akawafanyia hukumu na haki watu wake wote.2 Samuel 5.5 Jérémie 23.5-23.6 Jérémie 22.15-22.16 2 Samuel 3.12 2 Samuel 23.3-23.4
16 Huyo Yoabu, mwana wa Seruya alikuwa juu ya jeshi; na Yehoshafati, mwana wa Ahiludi, mwenye kuandika tarehe;1 Rois 4.3 1 Chroniques 11.6 2 Samuel 19.13 1 Chroniques 18.15-18.17 2 Samuel 20.23-20.24
17 na Sadoki, mwana wa Ahitubu, na Ahimeleki, mwana wa Abiathari walikuwa makuhani; na Shausha mwandishi;1 Chroniques 6.8 1 Chroniques 18.16 1 Chroniques 16.39 1 Chroniques 6.53 1 Chroniques 24.3-24.4
18 na Benaya, mwana wa Yehoyada, alikuwa juu ya Wakerethi na Wapelethi; nao wana wa Daudi wakawa makuhani.1 Samuel 30.14 2 Samuel 20.7 2 Samuel 15.18 1 Chroniques 18.17 2 Samuel 20.23

Cette Bible est dans le domaine public.