Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

2 Samuel 8.9
Bible en Swahili de l’est


1 Ikawa baadaye, Daudi akawapiga Wafilisti, akawashinda; Daudi akautwaa Gathi na vijiji vyake mikononi mwa hao Wafilisti.1 Chroniques 18.1-18.17 2 Samuel 2.24 2 Samuel 21.15-21.22 2 Samuel 7.9
2 Akapiga Moabu, akawapima kwa kamba hali wamelazwa chini; akapima kamba mbili za kuuawa, na kamba moja nzima ya kuhifadhi hai. Wamoabi wakawa watumwa wa Daudi, wakaleta zawadi.Nombres 24.17 2 Samuel 8.6 1 Samuel 10.27 Psaumes 60.8 1 Samuel 14.47
3 Tena Daudi akampiga Hadadezeri mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba, alipokwenda kujipatia tena mamlaka yake huko Mtoni.1 Samuel 14.47 2 Samuel 10.19 2 Samuel 10.16 2 Samuel 10.6 1 Chroniques 18.3
4 Daudi akampokonya wapanda farasi elfu na mia saba na askari waliokwenda kwa miguu ishirini elfu; Daudi akawakata mshipa farasi wote wa magari, ila farasi wa magari mia akawasaza.Josué 11.6 Josué 11.9 1 Rois 10.26 1 Chroniques 18.4 Psaumes 20.7
5 Na Washami wa Dameski walipokuja kumsaidia Hadadezeri, mfalme wa Soba, Daudi akawapiga wa Washami watu ishirini na mbili elfu.1 Rois 11.23-11.25 Esaïe 8.9-8.10 1 Chroniques 18.5-18.6 Job 9.13 2 Samuel 8.3
6 Daudi akaweka ngome katika Shamu ya Dameski, na hao Washami wakawa watumwa wa Daudi, wakaleta zawadi. Naye Bwana akampa Daudi kushinda kila alikokwenda.2 Samuel 8.14 2 Samuel 7.9 1 Samuel 14.6 1 Samuel 14.1 Psaumes 5.11-5.12
7 Tena Daudi akazitwaa ngao za dhahabu zilizovaliwa na watumwa wa Hadadezeri, akazileta Yerusalemu.1 Rois 10.16-10.17 1 Chroniques 18.7 2 Chroniques 9.15-9.16 1 Rois 14.26-14.27
8 Tena toka Tebhathi na toka Berothai, miji ya Hadadezeri, Daudi akatwaa shaba nyingi mno.1 Chroniques 18.8 1 Chroniques 22.14 1 Chroniques 29.7 Ezéchiel 47.16 2 Chroniques 4.1-4.18
9 Na Tou, mfalme wa Hamathi, aliposikia ya kwamba Daudi amewapiga jeshi lote la Hadadezeri,1 Rois 8.65 2 Chroniques 8.4 1 Chroniques 18.9 Amos 6.2
10 Tou akamtuma kwa Daudi Hadoramu mwanawe kusalimia, na kumbarikia, kwa sababu amepigana na Hadadezeri, na kumpiga; kwa maana Hadadezeri alikuwa amepigana vita juu ya Tou. Na mkononi mwake akaleta vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na vyombo vya shaba;1 Rois 1.47 Genèse 43.27 Esaïe 39.1 Psaumes 129.8 1 Chroniques 18.10
11 hivi pia mfalme Daudi akavifanya wakfu kwa Bwana, pamoja na hiyo fedha, na dhahabu alizofanya wakfu za mataifa yote aliowashinda;1 Rois 7.51 1 Chroniques 18.11 1 Chroniques 22.14-22.16 Michée 4.13 1 Chroniques 29.2
12 za Edomu, na za Moabu, na za wana wa Amoni, na za Wafilisti, na za Amaleki, na za nyara za Hadadezeri, mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba.2 Samuel 10.14 2 Samuel 8.2 1 Chroniques 18.11 1 Samuel 30.20 2 Samuel 10.11
13 Basi Daudi akajipatia jina, aliporudi kutoka kuwapiga Waedomi katika Bonde la Chumvi, watu kumi na nane elfu.2 Rois 14.7 2 Samuel 7.9 1 Chroniques 18.12 2 Chroniques 25.11 Psaumes 60.1
14 Akaweka askari wenye kulinda ngome katika Edomu; katikati ya Edomu yote akaweka ngome, na Waedomi wote wakawa watumwa wa Daudi. Naye Bwana akampa Daudi kushinda kila alikokwenda.Genèse 27.29 Genèse 25.23 2 Samuel 8.6 Genèse 27.37-27.40 1 Chroniques 18.13
15 Daudi akatawala juu ya Israeli wote; naye Daudi akawafanyia hukumu na haki watu wake wote.Amos 5.15 1 Chroniques 18.14 Psaumes 101.1-101.8 2 Samuel 5.5 Jérémie 23.5-23.6
16 Huyo Yoabu, mwana wa Seruya alikuwa juu ya jeshi; na Yehoshafati, mwana wa Ahiludi, mwenye kuandika tarehe;1 Rois 4.3 1 Chroniques 11.6 2 Samuel 19.13 2 Samuel 20.23-20.24 1 Chroniques 18.15-18.17
17 na Sadoki, mwana wa Ahitubu, na Ahimeleki, mwana wa Abiathari walikuwa makuhani; na Shausha mwandishi;1 Chroniques 18.16 1 Chroniques 6.8 1 Chroniques 24.3-24.4 1 Chroniques 16.39 1 Chroniques 6.53
18 na Benaya, mwana wa Yehoyada, alikuwa juu ya Wakerethi na Wapelethi; nao wana wa Daudi wakawa makuhani.1 Samuel 30.14 2 Samuel 20.23 2 Samuel 20.7 2 Samuel 15.18 1 Chroniques 18.17

Cette Bible est dans le domaine public.