Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

2 Chroniques 10.17
Bible en Swahili de l’est


1 Rehoboamu akaenda Shekemu; maana Israeli wote walikuwa wamekuja Shekemu, ili wamfanye mfalme.Genèse 37.12-37.13 1 Rois 4.1 1 Chroniques 12.38 Matthieu 1.7 Josué 20.7
2 Ikawa Yeroboamu mwana wa Nebati aliposikia, (maana alikuwako Misri, ambako amekimbilia mbele ya mfalme Sulemani), Yeroboamu akarudi kutoka Misri.1 Rois 11.40 1 Rois 11.26 1 Rois 12.2 1 Rois 11.28
3 Wakapeleka ujumbe, wakamwita, Yeroboamu akaja na Israeli wote, wakamwambia Rehoboamu, wakasema,1 Rois 12.3
4 Baba yako alilifanya zito kongwa letu; basi sasa upunguze utumwa mgumu wa baba yako, na kongwa lake zito alilotutwika, nasi tutakutumikia.1 Rois 9.22 1 Rois 12.4 Matthieu 23.4 Matthieu 11.29-11.30 1 Rois 4.20
5 Akawaambia, Mnirudie baada ya siku tatu. Watu wakaenda zao.Proverbes 3.28 1 Rois 12.5
6 Mfalme Rehoboamu akataka shauri kwa wazee, waliosimama mbele ya Sulemani baba yake, alipokuwa hai bado, akasema, Mwanipa shauri gani la kuwajibu watu hawa?Job 32.7 Job 12.12-12.13 Proverbes 27.10 Proverbes 12.15 2 Samuel 16.20
7 Wakamwambia, wakasema, Ukiwa mwema kwao watu hawa, na kuwapendeza, na kuwaambia maneno mazuri, ndipo watakapokuwa watumishi wako siku zote.Proverbes 15.1 1 Rois 12.7 2 Samuel 15.2-15.6 Genèse 49.21
8 Lakini akaliacha shauri lile la wazee walilompa, akataka shauri kwa wale vijana waliokua pamoja naye, waliosimama mbele yake.2 Samuel 17.14 Proverbes 19.20 Proverbes 1.25 Esaïe 30.1 Ecclésiaste 10.2-10.3
9 Akawaambia, Je! Mwanipa shauri gani la kuwajibu watu hawa, waliosema nami, wakisema, Utufanyie jepesi kongwa alilotutwika baba yako.2 Chroniques 10.6 1 Rois 22.6-22.8 2 Samuel 17.5-17.6
10 Na wale vijana waliokua pamoja naye wakamwambia, wakasema, Uwaambie hivi watu wale waliosema nawe, wakinena, Baba yako alilifanya zito kongwa letu, lakini wewe tufanyie jepesi; uwaambie hivi, Kidole changu cha mwisho ni kinene kuliko kiuno cha baba yangu.Proverbes 14.16 Proverbes 29.23 2 Samuel 17.7-17.13 Proverbes 10.14 Proverbes 18.6-18.7
11 Basi kama baba yangu aliwatwika kongwa zito, mimi nitaongeza kongwa lenu; baba yangu akiwapiga kwa mijeledi, lakini mimi nitawapiga kwa nge.1 Samuel 8.18 Esaïe 47.6 Jérémie 28.13-28.14 Luc 10.19 Esaïe 58.6
12 Basi Yeroboamu na watu wote wakamjia Rehoboamu siku ya tatu, kama mfalme alivyoamuru, akisema, Mnirudie siku ya tatu.1 Rois 12.12-12.15 2 Chroniques 10.5
13 Mfalme akawajibu kwa ukali; mfalme Rehoboamu akaliacha shauri la wazee, akasema nao kwa shauri la vijana,1 Samuel 25.10-25.11 2 Chroniques 10.8 1 Rois 20.6-20.11 Proverbes 19.27 Exode 10.28
14 akinena, Baba yangu aliwafanyia kongwa zito, nami nitawaongezea; baba yangu aliwapiga kwa mijeledi, lakini mimi nitawapiga kwa nge.2 Chroniques 22.4-22.5 Ecclésiaste 10.16 Jacques 3.14-4.2 Proverbes 17.14 Proverbes 12.5
15 Basi mfalme hakuwasikia wale watu; maana jambo hili lilitoka kwa Mungu, ili alithibitishe neno lake alilomwambia Yeroboamu mwana wa Nebati kwa mkono wa Ahiya Mshiloni.1 Samuel 2.25 1 Rois 11.29-11.39 2 Chroniques 25.16-25.20 Esaïe 19.14 Actes 2.23
16 Basi Israeli wote walipoona ya kuwa mfalme hawasikilizi, watu wakamjibu mfalme, wakasema, Tuna sehemu gani katika Daudi? Wala hatuna urithi katika mwana wa Yese; nendeni zenu hemani kwenu, enyi Israeli, kila mtu; sasa itunze nyumba yako mwenyewe, Daudi. Basi wakaenda zao Israeli wote hemani kwao.2 Samuel 20.1 2 Chroniques 10.19 Apocalypse 22.16 Psaumes 2.1-2.6 Psaumes 76.10
17 Lakini kwa habari za wana wa Israeli waliokaa katika miji ya Yuda, Rehoboamu alitawala juu yao.2 Chroniques 11.1 1 Rois 11.36 1 Rois 12.17
18 Ndipo mfalme Rehoboamu akamtuma Adoramu, msimamizi wa shokoa; nao wana wa Israeli wakamtupia mawe, hata akafa. Mfalme Rehoboamu akafanya haraka kupanda garini mwake, ili akimbilie Yerusalemu.1 Rois 5.14 1 Rois 4.6 2 Chroniques 24.21 Actes 7.57-7.58
19 Hivyo Israeli wakaasi juu ya nyumba ya Daudi, hata leo.2 Rois 17.21-17.23 Psaumes 89.30 Josué 4.9 2 Chroniques 10.16 2 Chroniques 13.5-13.7

Cette Bible est dans le domaine public.