Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

2 Chroniques 10.7
Bible en Swahili de l’est


1 Rehoboamu akaenda Shekemu; maana Israeli wote walikuwa wamekuja Shekemu, ili wamfanye mfalme.1 Chroniques 3.10 Genèse 12.6 1 Rois 12.1-12.20 Genèse 37.12-37.13 1 Rois 4.1
2 Ikawa Yeroboamu mwana wa Nebati aliposikia, (maana alikuwako Misri, ambako amekimbilia mbele ya mfalme Sulemani), Yeroboamu akarudi kutoka Misri.1 Rois 11.40 1 Rois 11.26 1 Rois 12.2 1 Rois 11.28
3 Wakapeleka ujumbe, wakamwita, Yeroboamu akaja na Israeli wote, wakamwambia Rehoboamu, wakasema,1 Rois 12.3
4 Baba yako alilifanya zito kongwa letu; basi sasa upunguze utumwa mgumu wa baba yako, na kongwa lake zito alilotutwika, nasi tutakutumikia.Exode 1.13-1.14 Exode 2.23 1 Jean 5.3 1 Rois 9.22 1 Rois 12.4
5 Akawaambia, Mnirudie baada ya siku tatu. Watu wakaenda zao.1 Rois 12.5 Proverbes 3.28
6 Mfalme Rehoboamu akataka shauri kwa wazee, waliosimama mbele ya Sulemani baba yake, alipokuwa hai bado, akasema, Mwanipa shauri gani la kuwajibu watu hawa?Job 32.7 Proverbes 19.20 Jérémie 42.20 Job 12.12-12.13 Proverbes 27.10
7 Wakamwambia, wakasema, Ukiwa mwema kwao watu hawa, na kuwapendeza, na kuwaambia maneno mazuri, ndipo watakapokuwa watumishi wako siku zote.Proverbes 15.1 1 Rois 12.7 Genèse 49.21 2 Samuel 15.2-15.6
8 Lakini akaliacha shauri lile la wazee walilompa, akataka shauri kwa wale vijana waliokua pamoja naye, waliosimama mbele yake.2 Samuel 17.14 Proverbes 9.9 Proverbes 13.20 Proverbes 19.20 Proverbes 1.25
9 Akawaambia, Je! Mwanipa shauri gani la kuwajibu watu hawa, waliosema nami, wakisema, Utufanyie jepesi kongwa alilotutwika baba yako.1 Rois 22.6-22.8 2 Samuel 17.5-17.6 2 Chroniques 10.6
10 Na wale vijana waliokua pamoja naye wakamwambia, wakasema, Uwaambie hivi watu wale waliosema nawe, wakinena, Baba yako alilifanya zito kongwa letu, lakini wewe tufanyie jepesi; uwaambie hivi, Kidole changu cha mwisho ni kinene kuliko kiuno cha baba yangu.Proverbes 28.25 Esaïe 19.11-19.13 1 Rois 12.10-12.11 Proverbes 14.16 Proverbes 29.23
11 Basi kama baba yangu aliwatwika kongwa zito, mimi nitaongeza kongwa lenu; baba yangu akiwapiga kwa mijeledi, lakini mimi nitawapiga kwa nge.Exode 1.13-1.14 Apocalypse 9.10 Exode 5.18 1 Samuel 8.18 Esaïe 47.6
12 Basi Yeroboamu na watu wote wakamjia Rehoboamu siku ya tatu, kama mfalme alivyoamuru, akisema, Mnirudie siku ya tatu.2 Chroniques 10.5 1 Rois 12.12-12.15
13 Mfalme akawajibu kwa ukali; mfalme Rehoboamu akaliacha shauri la wazee, akasema nao kwa shauri la vijana,Genèse 42.7 Genèse 42.30 Proverbes 15.1 1 Samuel 25.10-25.11 2 Chroniques 10.8
14 akinena, Baba yangu aliwafanyia kongwa zito, nami nitawaongezea; baba yangu aliwapiga kwa mijeledi, lakini mimi nitawapiga kwa nge.2 Chroniques 10.10-10.11 Ecclésiaste 7.8 Daniel 6.7 2 Chroniques 22.4-22.5 Ecclésiaste 10.16
15 Basi mfalme hakuwasikia wale watu; maana jambo hili lilitoka kwa Mungu, ili alithibitishe neno lake alilomwambia Yeroboamu mwana wa Nebati kwa mkono wa Ahiya Mshiloni.2 Chroniques 25.16-25.20 1 Samuel 2.25 1 Rois 11.29-11.39 Esaïe 19.14 Actes 2.23
16 Basi Israeli wote walipoona ya kuwa mfalme hawasikilizi, watu wakamjibu mfalme, wakasema, Tuna sehemu gani katika Daudi? Wala hatuna urithi katika mwana wa Yese; nendeni zenu hemani kwenu, enyi Israeli, kila mtu; sasa itunze nyumba yako mwenyewe, Daudi. Basi wakaenda zao Israeli wote hemani kwao.2 Samuel 20.1 2 Chroniques 10.19 Jean 6.66 Jérémie 33.25-33.26 Juges 8.35
17 Lakini kwa habari za wana wa Israeli waliokaa katika miji ya Yuda, Rehoboamu alitawala juu yao.1 Rois 11.36 1 Rois 12.17 2 Chroniques 11.1
18 Ndipo mfalme Rehoboamu akamtuma Adoramu, msimamizi wa shokoa; nao wana wa Israeli wakamtupia mawe, hata akafa. Mfalme Rehoboamu akafanya haraka kupanda garini mwake, ili akimbilie Yerusalemu.1 Rois 5.14 1 Rois 4.6 Actes 7.57-7.58 2 Chroniques 24.21
19 Hivyo Israeli wakaasi juu ya nyumba ya Daudi, hata leo.1 Rois 12.19-12.20 2 Chroniques 5.9 Esdras 9.7 2 Rois 17.21-17.23 Psaumes 89.30

Cette Bible est dans le domaine public.