Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Job 1.18 Bible en Swahili de l’est
Mise à l’épreuve de Job
Présentation de Job
1 Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu. Ezéchiel 14.14 Ezéchiel 14.20 Jacques 5.11 Genèse 17.1 Genèse 6.9 2 Kisha walizaliwa kwake wana saba, na binti watatu. Job 42.13 Psaumes 127.3-127.5 Job 13.13 Esther 5.11 Psaumes 128.3 3 Mali yake nayo yalikuwa ni kondoo elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng’ombe mia tano, na punda wake mia tano, na watu wa nyumbani wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote wa upande wa mashariki. Job 29.25 Job 42.12 Genèse 12.16 Juges 6.3 Genèse 34.23 4 Nao wanawe huenda na kufanya karamu katika nyumba ya kila mmoja wao kwa siku yake; nao wakatuma na kuwaita maumbu yao watatu ili waje kula na kunywa pamoja nao. Hébreux 13.1 Psaumes 133.1 5 Basi ilikuwa, hapo hizo siku za karamu zao zilipokuwa zimetimia, Ayubu hutuma kwao akawatakasa, kisha akaamka asubuhi na mapema, na kusongeza sadaka za kuteketezwa kama hesabu yao wote ilivyokuwa; kwani Ayubu alisema, Yumkini kwamba hawa wanangu wamefanya dhambi, na kumkufuru Mungu mioyoni mwao. Ndivyo alivyofanya Ayubu sikuzote. Genèse 8.20 Job 42.8 1 Samuel 16.5 1 Rois 21.10 1 Rois 21.13