Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Job 1.8
Bible en Swahili de l’est


1 Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu.Ezéchiel 14.14 Ezéchiel 14.20 Jacques 5.11 Genèse 17.1 Genèse 6.9
2 Kisha walizaliwa kwake wana saba, na binti watatu.Job 42.13 Psaumes 127.3-127.5 Job 13.13 Esther 5.11 Psaumes 128.3
3 Mali yake nayo yalikuwa ni kondoo elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng’ombe mia tano, na punda wake mia tano, na watu wa nyumbani wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote wa upande wa mashariki.Job 29.25 Genèse 12.16 Juges 6.3 Job 42.12 Genèse 12.5
4 Nao wanawe huenda na kufanya karamu katika nyumba ya kila mmoja wao kwa siku yake; nao wakatuma na kuwaita maumbu yao watatu ili waje kula na kunywa pamoja nao.Hébreux 13.1 Psaumes 133.1
5 Basi ilikuwa, hapo hizo siku za karamu zao zilipokuwa zimetimia, Ayubu hutuma kwao akawatakasa, kisha akaamka asubuhi na mapema, na kusongeza sadaka za kuteketezwa kama hesabu yao wote ilivyokuwa; kwani Ayubu alisema, Yumkini kwamba hawa wanangu wamefanya dhambi, na kumkufuru Mungu mioyoni mwao. Ndivyo alivyofanya Ayubu sikuzote.Genèse 8.20 Job 42.8 1 Samuel 16.5 1 Rois 21.10 1 Rois 21.13
6 Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao.Job 2.1 Job 38.7 Zacharie 3.1 1 Chroniques 21.1 1 Rois 22.19
7 Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.1 Pierre 5.8 Job 2.2 Zacharie 6.7 Zacharie 1.10-1.11 Apocalypse 20.8
8 Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu.Job 1.1 2 Rois 23.25 Job 2.3 Nombres 12.7-12.8 Esaïe 1.16
9 Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Je! Huyo Ayubu yuamcha Bwana bure?Matthieu 16.26 Job 21.14-21.15 Job 1.21 1 Timothée 6.6 Malachie 1.10
10 Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi.Psaumes 34.7 1 Pierre 1.5 Zacharie 2.5 Job 31.25 Psaumes 107.38
11 Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako.Job 2.5 Job 19.21 Job 1.5 Apocalypse 16.11 Esaïe 8.21
12 Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe. Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana.1 Rois 22.23 Genèse 16.6 2 Corinthiens 12.7 Luc 8.32-8.33 Jérémie 38.5
13 Ilitukia siku moja hao wanawe na binti zake walipokuwa wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa,Luc 17.27-17.29 Luc 21.34 Proverbes 27.1 Ecclésiaste 9.12 Luc 12.19-12.20
14 mjumbe akamfikilia Ayubu na kumwambia, Hao ng’ombe walikuwa wakilima, na punda walikuwa wakilisha karibu nao;Jérémie 51.31 1 Samuel 4.17 2 Samuel 15.13
15 mara Waseba wakawashambulia, wakawachukua wakaenda nao; naam, wamewaua hao watumishi kwa makali ya upanga, mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.Genèse 10.7 Job 6.19 Esaïe 45.14 Genèse 25.3 Joël 3.8
16 Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Moto wa Mungu umeanguka kutoka mbinguni na kuwateketeza kondoo, na wale watumishi, na kuwaangamiza; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.2 Rois 1.12 Genèse 19.24 Lévitique 10.2 Amos 7.4 2 Rois 1.10
17 Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wakaldayo walifanya vikosi vitatu, wakawaangukia ngamia, wakaenda nao, naam, wamewaua wale watumishi kwa makali ya upanga; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.Genèse 11.28 Habakuk 1.6 Genèse 11.31 2 Samuel 1.3 Job 1.15
18 Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wanao na binti zako walikuwa wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa;Job 1.4 Job 1.13 Amos 4.6-4.11 2 Samuel 13.28 Esaïe 28.19
19 mara, tazama, upepo wenye nguvu ukatoka pande za jangwani, ukaipiga hiyo nyumba pembe zake nne, nayo ikawaangukia hao vijana, nao wamekufa; na mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.Ephésiens 2.2 Genèse 42.36 Jérémie 4.11-4.12 Juges 16.30 2 Samuel 18.33
20 Ndipo Ayubu akainuka, akalirarua joho lake, kisha akanyoa kichwa chake, na kuanguka chini, na kusujudia;1 Pierre 5.6 Genèse 37.29 Esdras 9.3 Genèse 37.34 2 Samuel 12.16-12.20
21 akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana na libarikiwe.Ecclésiaste 5.15 1 Thessaloniciens 5.18 Ephésiens 5.20 1 Timothée 6.7 Job 2.10
22 Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa upumbavu.Job 2.10 Jacques 1.12 Romains 9.20 Jacques 1.4 1 Pierre 1.7

Cette Bible est dans le domaine public.