Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 10
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Bwana, kwa nini wasimama mbali? Kwani kujificha nyakati za shida? Psaumes 22.1 Job 34.29 Job 13.24 Job 23.9 Psaumes 27.9
2 Kwa kiburi chake asiye haki mnyonge anafuatiwa kwa ukali; Na wanaswe kwa hila zizo hizo walizoziwaza. Psaumes 7.16 Psaumes 119.5 Exode 9.17 Jérémie 43.2 Esaïe 14.16
3 Maana mdhalimu hujisifia tamaa ya nafsi yake, Na mwenye choyo humkana Bwana na kumdharau. Psaumes 94.4 Psaumes 49.6 Psaumes 49.18 Matthieu 26.15-26.16 Jérémie 22.17
4 Mdhalimu kwa kiburi cha uso wake Asema, Hatapatiliza. Jumla ya mawazo yake ni, Hakuna Mungu; Psaumes 53.1 Exode 5.2 Psaumes 36.1 Romains 1.28 Jérémie 2.31
5 Njia zake ni thabiti kila wakati. Hukumu zako ziko juu asizione, Adui zake wote awafyonya. Psaumes 12.5 Esaïe 26.11 Romains 3.16 Proverbes 15.24 Esaïe 42.25
6 Asema moyoni mwake, Sitaondoshwa, Kizazi baada ya kizazi sitakuwamo taabuni. Matthieu 24.48 Apocalypse 18.7 Ecclésiaste 8.11 Psaumes 30.6 Psaumes 15.5
7 Kinywa chake kimejaa laana, Na hila na dhuluma. Chini ya ulimi wake kuna madhara na uovu, Psaumes 7.14 Job 20.12 Psaumes 140.3 Psaumes 36.3 Proverbes 30.8
8 Hukaa katika maoteo ya vijiji. Mahali pa siri humwua asiye na hatia, Macho yake humvizia mtu duni. Habakuk 3.14 1 Samuel 23.23 Proverbes 6.12-6.13 Proverbes 1.11-1.12 Jérémie 22.17
9 Huotea faraghani kama simba pangoni, Huotea amkamate mtu mnyonge. Naam, humkamata mtu mnyonge, Akimkokota wavuni mwake. Psaumes 59.3 Psaumes 17.12 Michée 7.2 Nahum 2.11-2.12 Proverbes 22.16
10 Hujikunyata na kuinama; Watu duni huanguka kwa nguvu zake. 1 Samuel 2.36 1 Samuel 18.21-18.26 1 Samuel 23.21-23.22 2 Samuel 15.5
11 Asema moyoni mwake, Mungu amesahau, Auficha uso wake, haoni kamwe. Ezéchiel 8.12 Psaumes 94.7 Ezéchiel 9.9 Psaumes 73.11 Psaumes 10.6
12 Bwana, uondoke, Ee Mungu, uuinue mkono wako, Usiwasahau wanyonge. Psaumes 9.12 Michée 5.9 Psaumes 3.7 Psaumes 13.1 Psaumes 9.19
13 Kwani mdhalimu kumdharau Mungu. Akisema moyoni mwake, Hutapatiliza? Nombres 11.20 Genèse 9.5 Luc 10.16 2 Samuel 12.9-12.10 Luc 11.50-11.51
14 Umeona, maana unaangalia madhara na jeuri, Uyatwae mkononi mwako. Mtu duni hukuachia nafsi yake, Maana umekuwa msaidizi wa yatima. Psaumes 68.5 Psaumes 146.9 2 Timothée 1.12 1 Pierre 4.19 Osée 14.3
15 Uuvunje mkono wake mdhalimu, Na mbaya, uipatilize dhuluma yake, hata usiione. Psaumes 37.17 Psaumes 7.9 Ezéchiel 30.21-30.22 Sophonie 1.12 Job 38.15
16 Bwana ndiye Mfalme milele na milele; Mataifa wamepotea kutoka nchi yake. Psaumes 29.10 Deutéronome 8.20 1 Timothée 1.17 Psaumes 145.13 Lamentations 5.19
17 Bwana, umeisikia tamaa ya wanyonge, Utaitengeneza mioyo yao, utalitega sikio lako. 1 Chroniques 29.18 Psaumes 9.18 1 Pierre 3.12 2 Chroniques 34.27 Jacques 1.16-1.17
18 Ili kumhukumu yatima naye aliyeonewa, Binadamu aliye udongo asizidi kudhulumu. Psaumes 82.3 Psaumes 9.9 Psaumes 17.14 Esaïe 11.4 Psaumes 94.1-94.6

Cette Bible est dans le domaine public.