Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 10
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Bwana, kwa nini wasimama mbali? Kwani kujificha nyakati za shida? Psaumes 22.1 Jérémie 14.8 Psaumes 88.14 Job 34.29 Job 13.24
2 Kwa kiburi chake asiye haki mnyonge anafuatiwa kwa ukali; Na wanaswe kwa hila zizo hizo walizoziwaza. Psaumes 7.16 Esaïe 14.13 Psaumes 31.18 Psaumes 119.69 Psaumes 119.5
3 Maana mdhalimu hujisifia tamaa ya nafsi yake, Na mwenye choyo humkana Bwana na kumdharau. Psaumes 94.4 Psaumes 49.6 Proverbes 28.4 Luc 12.19 Deutéronome 29.19
4 Mdhalimu kwa kiburi cha uso wake Asema, Hatapatiliza. Jumla ya mawazo yake ni, Hakuna Mungu; Psaumes 53.1 Proverbes 21.4 Jérémie 4.14 Genèse 6.5 Esaïe 2.11
5 Njia zake ni thabiti kila wakati. Hukumu zako ziko juu asizione, Adui zake wote awafyonya. Esaïe 26.11 Psaumes 12.5 Osée 14.9 Proverbes 2.15 Esaïe 28.15
6 Asema moyoni mwake, Sitaondoshwa, Kizazi baada ya kizazi sitakuwamo taabuni. Matthieu 24.48 Apocalypse 18.7 Ecclésiaste 8.11 Esaïe 56.12 Nahum 1.10
7 Kinywa chake kimejaa laana, Na hila na dhuluma. Chini ya ulimi wake kuna madhara na uovu, Psaumes 7.14 Job 20.12 Psaumes 140.3 Psaumes 36.3 Psaumes 144.11
8 Hukaa katika maoteo ya vijiji. Mahali pa siri humwua asiye na hatia, Macho yake humvizia mtu duni. Habakuk 3.14 Psaumes 94.6 Luc 8.1 2 Rois 21.16 1 Samuel 23.23
9 Huotea faraghani kama simba pangoni, Huotea amkamate mtu mnyonge. Naam, humkamata mtu mnyonge, Akimkokota wavuni mwake. Psaumes 59.3 Psaumes 17.12 Michée 7.2 Esaïe 3.15 Zacharie 11.3
10 Hujikunyata na kuinama; Watu duni huanguka kwa nguvu zake. 1 Samuel 23.21-23.22 2 Samuel 15.5 1 Samuel 2.36 1 Samuel 18.21-18.26
11 Asema moyoni mwake, Mungu amesahau, Auficha uso wake, haoni kamwe. Ezéchiel 8.12 Psaumes 94.7 Ezéchiel 9.9 Psaumes 73.11 Psaumes 64.5
12 Bwana, uondoke, Ee Mungu, uuinue mkono wako, Usiwasahau wanyonge. Psaumes 9.12 Michée 5.9 Psaumes 3.7 Esaïe 33.10 Psaumes 94.2
13 Kwani mdhalimu kumdharau Mungu. Akisema moyoni mwake, Hutapatiliza? Genèse 42.22 1 Thessaloniciens 4.8 Psaumes 74.10 Nombres 11.20 Genèse 9.5
14 Umeona, maana unaangalia madhara na jeuri, Uyatwae mkononi mwako. Mtu duni hukuachia nafsi yake, Maana umekuwa msaidizi wa yatima. Psaumes 68.5 Psaumes 146.9 Psaumes 55.22 1 Pierre 5.7 2 Timothée 1.12
15 Uuvunje mkono wake mdhalimu, Na mbaya, uipatilize dhuluma yake, hata usiione. Psaumes 37.17 Job 38.15 Psaumes 7.9 Ezéchiel 30.21-30.22 Sophonie 1.12
16 Bwana ndiye Mfalme milele na milele; Mataifa wamepotea kutoka nchi yake. Psaumes 29.10 Jérémie 10.10 Deutéronome 8.20 1 Timothée 1.17 Psaumes 145.13
17 Bwana, umeisikia tamaa ya wanyonge, Utaitengeneza mioyo yao, utalitega sikio lako. Psaumes 9.18 1 Chroniques 29.18 Luc 18.13-18.14 Psaumes 34.15 1 Pierre 3.12
18 Ili kumhukumu yatima naye aliyeonewa, Binadamu aliye udongo asizidi kudhulumu. Psaumes 82.3 Esaïe 11.4 Psaumes 9.9 Psaumes 17.14 Psaumes 72.4

Cette Bible est dans le domaine public.