Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Psaumes 136.1 Bible en Swahili de l’est
La bonté éternelle de Dieu
1 Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 2 Mshukuruni Mungu wa miungu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 3 Mshukuruni Bwana wa mabwana; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 4 Yeye peke yake afanya maajabu makuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 5 Yeye aliyefanya mbingu kwa fahamu zake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 6 Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 7 Yeye aliyefanya mianga mikubwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 8 Jua litawale mchana; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 9 Mwezi na nyota zitawale usiku; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 10 Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wa kwanza wao; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 11 Akawatoa Waisraeli katikati yao; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 12 Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 13 Yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 14 Akawavusha Israeli katikati yake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 15 Akamwangusha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 16 Yeye aliyewaongoza watu wake jangwani; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 17 Yeye aliyewapiga wafalme wakuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 18 Akawaua wafalme mashuhuri; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 19 Sihoni, mfalme wa Waamori; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 20 Na Ogu, mfalme wa Bashani; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 21 Akaitoa nchi yao iwe urithi; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 22 Urithi wa Israeli mtumishi wake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 23 Aliyetukumbuka katika unyonge wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 24 Akatuokoa na watesi wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 25 Kila chenye mwili akipa chakula chake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. 26 Mshukuruni Mungu wa mbingu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.