Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 9
Bible en Swahili de l’est


1 Nitamshukuru Bwana kwa moyo wangu wote; Nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu; Psaumes 86.12 Psaumes 145.1-145.3 Psaumes 138.1 Psaumes 146.1-146.2 Psaumes 111.1
2 Nitafurahi na kukushangilia Wewe; Nitaliimbia jina lako, Wewe Uliye juu. Psaumes 83.18 Psaumes 5.11 Psaumes 92.1 Psaumes 7.17 Psaumes 28.7
3 Kwa sababu adui zangu hurudi nyuma; Hujikwaa na kuangamia mbele zako. Esaïe 64.3 Apocalypse 6.12-6.17 Apocalypse 20.11 Psaumes 68.1-68.2 2 Thessaloniciens 1.9
4 Kwa maana umenifanyia hukumu na haki Umeketi kitini pa enzi ukihukumu kwa haki. Psaumes 140.12 1 Pierre 2.23 Psaumes 47.8 Psaumes 45.6-45.7 Psaumes 96.13
5 Umewakemea mataifa; Na kumwangamiza mdhalimu; Umelifuta jina lao milele na milele; Proverbes 10.7 Deutéronome 9.14 Malachie 4.3 2 Samuel 8.1-8.15 1 Samuel 25.32
6 Adui wamekoma na kuachwa ukiwa milele. Nayo miji yao uliing’oa; Hata kumbukumbu lao limepotea. Exode 15.16 1 Corinthiens 15.54-15.57 Michée 7.10 Esaïe 10.6-10.7 Psaumes 8.2
7 Bali Bwana atakaa milele, Ameweka kiti chake tayari kwa hukumu. Psaumes 103.19 Psaumes 90.2 Psaumes 102.12 Hébreux 1.11-1.12 Psaumes 102.24-102.27
8 Naye atauhukumu ulimwengu kwa haki; Atawaamua watu kwa adili. Psaumes 96.13 Psaumes 98.9 Romains 2.16 Romains 2.5-2.6 Esaïe 11.4-11.5
9 Bwana atakuwa ngome kwake aliyeonewa, Naam, ngome kwa nyakati za shida. Psaumes 32.7 Proverbes 18.10 Psaumes 91.1-91.2 Hébreux 6.18 Psaumes 18.2
10 Nao wakujuao jina lako wakutumaini Wewe, Maana Wewe, Bwana hukuwaacha wakutafutao. Psaumes 91.14 2 Corinthiens 1.9-1.10 2 Timothée 1.12 Proverbes 18.10 Esaïe 26.3-26.4
11 Mwimbieni Bwana akaaye Sayuni, Yatangazeni kati ya watu matendo yake. Psaumes 107.22 Psaumes 76.2 Jean 17.26 Psaumes 96.10 Psaumes 132.13-132.14
12 Maana mlipiza kisasi cha damu awakumbuka, Hakukisahau kilio cha wanyonge. Genèse 9.5 Psaumes 34.6 Exode 3.7 Apocalypse 16.6 Apocalypse 6.9-6.10
13 Wewe, Bwana, unifadhili, Tazama mateso niteswayo na wanaonichukia; Wewe uniinuaye katika malango ya mauti, Psaumes 30.3 Psaumes 86.13 Psaumes 142.6 Esaïe 38.10 Lamentations 1.9
14 Ili nizisimulie sifa zako zote; Katika malango ya binti Sayuni Nitaufurahia wokovu wako. Psaumes 13.5 Psaumes 106.2 Psaumes 51.12 Psaumes 20.5 Psaumes 35.9
15 Mataifa wamezama katika shimo walilolifanya; Kwa wavu waliouficha imenaswa miguu yao. Psaumes 57.6 Psaumes 7.15-7.16 Psaumes 35.8 Psaumes 37.15 Psaumes 94.23
16 Bwana amejidhihirisha na kutekeleza hukumu; Amemnasa mdhalimu kwa kazi ya mikono yake. Exode 7.5 Proverbes 12.13 Exode 14.4 Esaïe 8.15 1 Samuel 17.46
17 Wadhalimu watarejea kuzimu, Naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu. Job 8.13 Psaumes 50.22 2 Thessaloniciens 1.7-1.9 Romains 2.8-2.9 Esaïe 5.14
18 Kwa maana mhitaji hatasahauliwa daima; Matumaini ya wanyonge hayatapotea milele. Proverbes 23.18 Psaumes 12.5 Psaumes 9.12 Proverbes 24.14 Psaumes 71.5
19 Bwana, usimame, mwanadamu asipate nguvu, Mataifa wahukumiwe mbele zako. Psaumes 3.7 2 Chroniques 14.11 Psaumes 44.26 Psaumes 10.12 Psaumes 76.8-76.9
20 Bwana, uwawekee kitisho, Mataifa na wajijue kuwa ni binadamu. Esaïe 31.3 Exode 15.16 Exode 23.27 Deutéronome 2.25 Actes 12.22-12.23

Cette Bible est dans le domaine public.