Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Proverbes 14.29
Bible en Swahili de l’est


1 Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.Proverbes 21.19 Proverbes 21.9 Proverbes 31.10-31.31 Proverbes 24.3-24.4 Ruth 4.11
2 Yeye aendaye kwa unyofu wake humcha Bwana; Bali aliye mkaidi katika njia zake humdharau.Proverbes 28.6 Actes 10.22 Proverbes 11.12 Psaumes 112.1 Malachie 2.5-2.6
3 Katika kinywa cha mpumbavu mna fimbo ya kiburi, Bali midomo ya wenye hekima huwahifadhi.Proverbes 12.6 2 Pierre 2.18 Proverbes 21.24 Psaumes 52.1-52.2 Psaumes 57.4
4 Zizi ni safi ambapo hapana ng’ombe; Bali nguvu za ng’ombe zaleta faida nyingi.1 Corinthiens 9.9-9.11 Proverbes 13.23 Amos 4.6
5 Shahidi mwaminifu hatasema uongo; Bali shahidi wa uongo, pumzi zake ni uongo.Proverbes 6.19 Exode 23.1 Proverbes 12.17 Proverbes 19.5 Exode 20.16
6 Mwenye dharau hutafuta hekima, asiipate; Bali maarifa huwa mepesi kwa mwenye ufahamu.Proverbes 17.24 Proverbes 8.9 Matthieu 13.11-13.12 Jacques 1.5 Matthieu 11.25-11.27
7 Toka mbele ya uso wa mpumbavu, Maana hutaona kwake midomo ya maarifa.Proverbes 13.20 Proverbes 9.6 Proverbes 19.27 Ephésiens 5.11 1 Corinthiens 5.11
8 Akili za mwenye busara ni kujua njia yake; Lakini upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu.Ephésiens 5.17 Colossiens 1.9-1.10 Psaumes 143.8 Jérémie 13.20 Proverbes 2.9
9 Wapumbavu huidharau hatia; Bali upo upendeleo kwa wenye haki.Proverbes 10.23 Proverbes 13.15 Proverbes 26.18-26.19 Proverbes 8.35 Jude 1.18
10 Moyo huujua uchungu wa nafsi yake, Wala mgeni haishiriki furaha yake.1 Samuel 1.10 Philippiens 4.7 Jean 14.18 Apocalypse 2.17 Job 10.1
11 Nyumba ya mtu mbaya itabomolewa; Bali hema ya mwenye haki itafanikiwa.Proverbes 3.33 Job 8.15 Job 21.28 Proverbes 12.7 Psaumes 128.3
12 Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti.Proverbes 16.25 Proverbes 12.15 Matthieu 7.13-7.14 Jacques 1.22 Galates 6.3
13 Hata wakati wa kucheka moyo huwa na huzuni; Na mwisho wa furaha ni uzito wa moyo.Ecclésiaste 2.2 Ecclésiaste 7.5-7.6 Jacques 4.9 Ecclésiaste 11.9 Apocalypse 18.7-18.8
14 Ageukaye moyoni hushiba njia zake mwenyewe; Na mtu mwema ataridhika nafsini mwake.Proverbes 12.14 Galates 6.8 Jérémie 8.5 Hébreux 3.12 Osée 4.16
15 Mjinga huamini kila neno; Bali mwenye busara huangalia sana aendavyo.Ephésiens 5.17 Romains 16.18-16.19 Proverbes 22.3 Proverbes 4.26 Proverbes 14.8
16 Mwenye hekima huogopa, akajitenga na uovu; Bali mpumbavu ana ufidhuli, na kujitumai.Proverbes 22.3 Proverbes 3.7 1 Thessaloniciens 5.22 Marc 6.17-6.19 Proverbes 16.6
17 Yeye aonaye hasira upesi atatenda kwa ujinga; Na mtu mwenye hila mbaya huzirwa.Proverbes 14.29 Proverbes 29.22 Jacques 1.19 Proverbes 15.18 Ecclésiaste 7.9
18 Wajinga hurithi upumbavu; Bali wenye busara huvikwa taji ya maarifa.1 Pierre 5.4 Daniel 12.3 1 Pierre 1.18 Matthieu 23.29-23.32 Jérémie 44.17
19 Wabaya huinama mbele ya wema, Na wasio haki malangoni mwao wenye haki.Genèse 42.6 Exode 9.27-9.28 Michée 7.16-7.17 2 Rois 3.12 Exode 11.8
20 Maskini huchukiwa hata na jirani yake; Bali tajiri ana rafiki wengi.Proverbes 19.4 Job 19.13-19.14 Esther 5.10-5.11 Proverbes 10.15 Job 6.21-6.23
21 Amdharauye mwenzake afanya dhambi; Bali amhurumiaye maskini ana heri.Proverbes 11.12 Proverbes 19.17 Jacques 2.5-2.6 Psaumes 112.9 Psaumes 22.24
22 Je! Hawakosi wawazao mabaya? Bali fadhili na kweli zina wao wawazao mema.Proverbes 12.2 Esaïe 32.7-32.8 Matthieu 5.7 Genèse 24.27 Proverbes 3.29
23 Katika kila kazi mna faida; Bali maneno ya midomo huleta hasara tu.Hébreux 6.10-6.11 Jean 6.27 Proverbes 28.19 Proverbes 12.24 2 Thessaloniciens 3.10-3.12
24 Taji ya wenye hekima ni mali zao; Bali upumbavu wa wajinga ni upumbavu tu.Esaïe 33.6 Luc 16.19-16.25 Psaumes 49.10-49.13 Luc 16.9 Proverbes 27.22
25 Shahidi wa kweli huponya nafsi za watu; Bali atoaye uongo hudanganya.Proverbes 14.5 Actes 26.16-26.20 Actes 20.21 2 Pierre 3.3 Actes 20.26-20.27
26 Kumcha Bwana ni tumaini imara; Watoto wake watakuwa na kimbilio.Proverbes 18.10 Proverbes 19.23 Jérémie 32.39-32.40 Esaïe 33.6 Psaumes 34.7-34.11
27 Kumcha Bwana ni chemchemi ya uzima, Ili kuepukana na tanzi za mauti.Proverbes 13.14 Proverbes 2.10-2.18 Ecclésiaste 7.26 Apocalypse 21.6 Proverbes 22.5
28 Utukufu wa mfalme ni wingi wa watu wake; Bali uchache wa watu ni uharibifu wa mkuu wao.2 Rois 13.7 2 Rois 10.32-10.33 1 Rois 20.27 1 Rois 4.20-4.21 Exode 1.12
29 Asiye mwepesi wa hasira ana fahamu nyingi; Bali mwenye roho ya hamaki hutukuza upumbavu.Jacques 1.19 Ecclésiaste 7.9 Proverbes 14.17 Proverbes 16.32 Proverbes 19.11
30 Moyo ulio mzima ni uhai wa mwili; Bali husuda ni ubovu wa mifupa.Proverbes 12.4 Proverbes 17.22 Job 5.2 Proverbes 4.23 Psaumes 112.10
31 Amwoneaye maskini humsuta Muumba wake; Bali yeye awahurumiaye wahitaji humheshimu.Proverbes 17.5 Proverbes 22.2 Job 31.13-31.16 Proverbes 22.16 Proverbes 19.17
32 Mtu mbaya husukumwa chini katika kutenda mabaya kwake; Bali mwenye haki ana matumaini katika kufa kwake.2 Timothée 4.18 Genèse 49.18 2 Corinthiens 1.9 2 Corinthiens 5.8 Job 19.25-19.27
33 Hekima hukaa katika moyo wake mwenye ufahamu; Bali yaliyo ndani ya wapumbavu hudhihirika.Proverbes 12.16 Proverbes 29.11 Proverbes 13.16 Ecclésiaste 10.3 Proverbes 15.28
34 Haki huinua taifa; Bali dhambi ni aibu ya watu wo wote.Psaumes 107.34 Deutéronome 28.1-28.68 Deutéronome 29.18-29.28 Deutéronome 4.6-4.8 Ezéchiel 16.1-16.63
35 Upendeleo wa mfalme humwelekea mtumwa atendaye kwa busara; Bali ghadhabu yake itakuwa juu yake aletaye aibu.Proverbes 22.11 Matthieu 24.45-24.51 Luc 12.42-12.48 Psaumes 101.4-101.8 Proverbes 25.5

Cette Bible est dans le domaine public.