Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Ecclésiaste 10.13
Bible en Swahili de l’est


1 Mainzi mafu huvundisha marhamu ya mwuza marashi; Kadhalika upumbavu haba ni mzito kuliko hekima na heshima.Matthieu 5.13-5.16 Galates 2.12-2.14 2 Chroniques 19.2 Exode 30.25 Exode 30.34-30.35
2 Moyo wake mwenye hekima upo upande wa kuume; Bali moyo wake mpumbavu upo mkono wa kushoto.Luc 12.18-12.20 Luc 14.28-14.32 Ecclésiaste 10.14 Proverbes 14.8 Ecclésiaste 10.10
3 Naam, huyo mpumbavu tena, aendapo njiani, hupungukiwa na fahamu zake; hata humwambia kila mtu ya kuwa yeye ni mpumbavu.Proverbes 18.2 Proverbes 13.16 1 Pierre 4.4 Ecclésiaste 5.3 Proverbes 18.6
4 Roho yake mtawala ikiinuka kinyume chako, Usiondoke mara mahali pako ulipo; Kwa maana roho ya upole hutuliza machukizo yaliyo makubwa.Ecclésiaste 8.3 Proverbes 25.15 1 Samuel 25.24-25.44
5 Liko baa nililoliona chini ya jua, nalo ni kama kosa litokalo kwake yeye atawalaye;Ecclésiaste 3.16 Ecclésiaste 5.13 Ecclésiaste 9.3 Ecclésiaste 4.7 Ecclésiaste 4.1
6 ya kuwa upumbavu huwekwa mahali pa juu sana, nao wakwasi hukaa mahali pa chini.Proverbes 28.12 Esther 3.1 Proverbes 29.2 1 Rois 12.13-12.14 Juges 9.14-9.20
7 Mimi nimeona watumwa wamepanda farasi, na wakuu wakienda kwa miguu juu ya nchi kama watumwa.Proverbes 19.10 Proverbes 30.22 Esther 6.8
8 Mwenye kuchimba shimo atatumbukia ndani yake; Na yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma.Amos 5.19 Proverbes 26.27 Juges 9.5 Amos 9.3 Psaumes 7.15-7.16
9 Mwenye kuchonga mawe ataumizwa kwayo; Naye apasuaye miti huona hatari katika hiyo. 10 Iwapo chuma hakipati, wala mtu hakinoi; Ndipo hana budi kutumia nguvu zaidi. Walakini yafaa kutumia hekima, na kufanikiwa.Jacques 1.5 Ephésiens 5.15-5.17 Exode 18.19-18.23 Ecclésiaste 10.15 Actes 6.1-6.9
11 Nyoka akiuma asijatumbuizwa, Basi hakuna faida ya mtumbuizi.Jérémie 8.17 Psaumes 58.4-58.5 Psaumes 52.2 Psaumes 64.3 Proverbes 18.21
12 Maneno ya kinywa chake mwenye hekima yana neema; Bali midomo ya mpumbavu itammeza nafsi yake.Proverbes 15.2 Luc 4.22 Colossiens 4.6 Ephésiens 4.29 Proverbes 22.17-22.18
13 Mwanzo wa maneno ya kinywa chake ni upuuzi; na mwisho wa usemi wake ni wazimu wenye hatari.Actes 19.24-19.28 1 Samuel 22.7-22.8 Actes 5.28-5.33 Matthieu 2.7-2.8 Luc 6.2
14 Tena, upumbavu huongeza maneno; lakini mwanadamu hajui yatakayokuwako; nayo yatakayokuwa baada yake, ni nani awezaye kumweleza?Proverbes 15.2 Ecclésiaste 8.7 Ecclésiaste 6.12 Ecclésiaste 5.3 Ecclésiaste 3.22
15 Kazi yao wapumbavu huwachosha kila mmoja, Maana hajui hata njia ya kuuendea mji.Matthieu 11.28-11.30 Ecclésiaste 10.10 Ecclésiaste 10.3 Esaïe 57.1 Jérémie 50.4-50.5
16 Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana, Na wakuu wako hula asubuhi!Esaïe 3.12 Esaïe 3.4-3.5 2 Chroniques 13.7 Esaïe 5.11-5.12 2 Chroniques 36.9
17 Heri kwako, nchi, mfalme wako akiwa mtoto wa watu, Na wakuu wako hula wakati ufaao, Ili makusudi wapate nguvu, wala si kwa ajili ya ulevi.Proverbes 31.4-31.5 Ecclésiaste 10.6-10.7 Jérémie 30.21 Proverbes 28.2-28.3 Esaïe 5.11
18 Kwa sababu ya uvivu paa hunepa; Na kwa utepetevu wa mikono nyumba huvuja.Proverbes 14.1 Proverbes 20.4 Proverbes 21.25 Proverbes 12.24 Hébreux 6.11
19 Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, Na divai huyafurahisha maisha; Na fedha huleta jawabu la mambo yote.Psaumes 104.15 Luc 12.19 Genèse 43.34 1 Timothée 6.17-6.19 Esaïe 24.11
20 Usimlaani mfalme, la, hata katika wazo lako; Wala usiwalaani wakwasi chumbani mwako; Kwa kuwa ndege wa anga ataichukua sauti, Na mwenye mabawa ataitoa habari.Exode 22.28 Actes 23.5 Luc 10.40 Luc 12.2-12.3 Ecclésiaste 7.21-7.22

Cette Bible est dans le domaine public.