Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Cantique 4
Bible en Swahili de l’est


1 Tazama, u mzuri, mpenzi wangu, U mzuri, macho yako ni kama ya hua, Nyuma ya barakoa yako. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi, Wakijilaza mbavuni pa mlima Gileadi. Cantique 1.15 Cantique 6.5 Cantique 6.7 Cantique 7.5 Michée 7.14
2 Meno yako ni kama kundi waliokatwa manyoya, Wakipanda kutoka kuoshwa, Ambao kila mmoja amezaa mapacha, Wala hakuna aliyefiwa kati yao. Cantique 6.6 Jérémie 15.16 1 Thessaloniciens 2.13 2 Pierre 1.5-1.8 Exode 23.26
3 Midomo yako ni kama uzi mwekundu, Na kinywa chako ni kizuri; Mashavu yako ni kama kipande cha komamanga, Nyuma ya barakoa yako. Cantique 6.7 Josué 2.18 Cantique 5.16 Lévitique 14.4 Luc 4.22
4 Shingo yako ni kama mnara wa Daudi, Uliojengwa pa kuwekea silaha; Ngao elfu zimetungikwa juu yake, Zote ni ngao za mashujaa. Cantique 7.4 Néhémie 3.19 Ezéchiel 27.10-27.11 1 Pierre 1.5 2 Chroniques 9.15-9.16
5 Maziwa yako mawili ni kama wana-paa wawili, Nyuma ya barakoa yako. Ambao ni mapacha ya paa; Wakilisha penye nyinyoro. Cantique 7.3 Cantique 6.3 Cantique 2.16 Cantique 8.10 Proverbes 5.19
6 Hata jua lipunge, na vivuli vikimbie, Nitakwenda kwenye mlima wa manemane, Na kwenye kilima cha ubani. Cantique 2.17 Cantique 4.14 Luc 1.78 Malachie 4.2 Exode 37.29
7 Mpenzi wangu, u mzuri pia pia, Wala ndani yako hamna ila. Cantique 1.15 Psaumes 45.13 Psaumes 45.11 Ephésiens 5.25-5.27 Cantique 4.1
8 Bibi arusi, njoo pamoja nami toka Lebanoni, Pamoja nami toka Lebanoni. Shuka kutoka kilele cha Amana, Kutoka vilele vya Seniri na Hermoni; Kutoka mapangoni mwa simba, Kutoka milimani mwa chui. Deutéronome 3.9 1 Chroniques 5.23 Psaumes 45.10 Proverbes 9.6 Deutéronome 3.25
9 Umenishangaza moyo, umbu langu, Bibi arusi, umenishangaza moyo, Kwa mtupo mmoja wa macho yako, Kwa mkufu mmoja wa shingo yako. Cantique 5.1-5.2 Cantique 4.12 Cantique 4.10 Cantique 7.10 Esaïe 62.5
10 Jinsi zilivyo nzuri pambaja zako, umbu langu, Bibi arusi, ni nzuri kupita divai; Na harufu ya marhamu yako Yapita manukato ya kila namna. Cantique 1.2-1.4 Galates 5.22 Cantique 5.5 2 Corinthiens 1.21-1.22 Philippiens 4.18
11 Bibi arusi, midomo yako yadondoza asali, Asali na maziwa vi chini ya ulimi wako; Na harufu ya mavazi yako Ni kama harufu ya Lebanoni. Genèse 27.27 Cantique 5.1 Cantique 4.10 Cantique 7.9 Proverbes 24.13-24.14
12 Bustani iliyofungwa ni umbu langu, bibi arusi, Kijito kilichofungwa, chemchemi iliyotiwa muhuri. Proverbes 5.15-5.18 Cantique 6.2 Apocalypse 7.3 Esaïe 61.10-61.11 Cantique 6.11
13 Machipuko yako ni bustani ya komamanga, Yenye matunda mazuri, hina na nardo, Cantique 1.14 Cantique 6.11 Ecclésiaste 2.5 Cantique 1.12 Jean 15.1-15.3
14 Nardo na zafarani, mchai na mdalasini, Na miti yote iletayo ubani, Manemane na udi, na kolezi kuu zote. Exode 30.23 Cantique 4.6 Ezéchiel 27.19 Cantique 3.6 Genèse 43.11
15 Wewe ndiwe chemchemi ya bustani yangu, Kisima cha maji yaliyo hai, Vijito vya Lebanoni viendavyo kasi. Jean 4.10 Jérémie 2.13 Jean 7.38 Jérémie 18.13-18.14 Jérémie 17.13
16 Amka, kaskazi; nawe uje, kusi; Vumeni juu ya bustani yangu, Manukato ya bustani yatokee. Mpendwa wangu na aingie bustanini mwake, Akayale matunda yake mazuri. Cantique 6.2 Cantique 5.1 Romains 15.28 Ezéchiel 37.9 Actes 4.31

Cette Bible est dans le domaine public.