Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 38.15
Bible en Swahili de l’est


1 Siku hizo Hezekia aliugua, akawa katika hatari ya kufa; na Isaya nabii, mwana wa Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, Bwana asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona.2 Samuel 17.23 2 Chroniques 32.24 2 Rois 20.1-20.11 Esaïe 38.1-38.8 Philippiens 2.27-2.30
2 Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana,1 Rois 8.30 Psaumes 91.15 Psaumes 50.15 Matthieu 6.6
3 akasema, Ee Bwana, kumbuka haya, nakusihi, kwamba nimekwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana.Néhémie 13.14 1 Chroniques 29.19 Psaumes 6.8 Psaumes 32.2 Jean 1.47
4 Ikawa, neno la Bwana likamjia Isaya, kusema, 5 Enenda ukamwambie Hezekia, Bwana, Mungu wa Daudi, baba yako, asema hivi, Mimi nimeyasikia maombi yako, nimeyaona machozi yako; tazama, nitaziongeza siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano.2 Rois 18.2 Actes 27.24 Psaumes 56.8 Esaïe 7.13-7.14 Psaumes 116.15
6 Nami nitakuokoa wewe, na mji huu, na mkono wa mfalme wa Ashuru, nami nitaulinda mji huu.Esaïe 37.35 Esaïe 12.6 2 Chroniques 32.22 2 Timothée 4.17 Esaïe 31.4-31.5
7 Jambo hili liwe ishara kwako, itokayo kwa Bwana, ya kuwa Bwana atalitimiza jambo hili alilolisema;Juges 6.37-6.39 Esaïe 37.30 Genèse 9.13 Juges 6.17-6.22 2 Rois 20.8-20.21
8 Tazama, nitakirudisha nyuma kivuli madaraja kumi, ambayo kilishuka juu ya duara ya Ahazi kwa sababu ya jua. Basi jua likarudi madaraja kumi katika hiyo duara, ambayo limekwisha kushuka.2 Chroniques 32.31 Josué 10.12-10.14 Matthieu 16.1 2 Chroniques 32.24 2 Rois 20.9-20.11
9 Haya ndiyo maandiko ya Hezekia, mfalme wa Yuda, alipokuwa hawezi, naye akapona ugonjwa wake.Psaumes 116.1-116.4 Psaumes 107.17-107.22 Exode 15.1-15.21 Osée 6.1-6.2 Juges 5.1-5.31
10 Nalisema, Katika usitawi wa siku zangu nitakwenda kuingia malango ya kuzimu; Nimenyimwa mabaki ya miaka yangu.2 Corinthiens 1.9 Psaumes 102.24 Job 6.11 Job 17.11-17.16 Esaïe 38.1
11 Nalisema, Sitamwona Bwana, yeye Bwana, katika nchi ya walio hai; Sitamwona mwanadamu tena pamoja na hao wakaao duniani.Psaumes 27.13 Job 35.14-35.15 Psaumes 31.22 Ecclésiaste 9.5-9.6 Psaumes 6.4-6.5
12 Kao langu limeondolewa kabisa, limechukuliwa kama hema ya mchungaji; Nimekunja maisha yangu kama mfumaji; atanikatilia mbali na kitanda cha mfumi; Tangu mchana hata usiku wanimaliza.Psaumes 73.14 2 Corinthiens 5.1 Hébreux 1.12 Esaïe 13.20 Psaumes 119.23
13 Nalijituliza hata asubuhi; kama simba, aivunja mifupa yangu yote; Tangu mchana hata usiku wanimaliza.Daniel 6.24 Psaumes 51.8 Osée 5.14 Psaumes 50.22 1 Rois 13.24-13.26
14 Kama mbayuwayu au korongo ndivyo nilivyolia; Naliomboleza kama hua; macho yangu yamedhoofu kwa kutazama juu; Ee Bwana, nimeonewa, na uwe mdhamini wangu.Esaïe 59.11 Ezéchiel 7.16 Psaumes 119.122-119.123 Job 30.29 Nahum 2.7
15 Niseme nini? Yeye amenena nami, na yeye mwenyewe ametenda hayo; Nitakwenda polepole miaka yangu yote, kwa sababu ya uchungu wa nafsi yangu.1 Rois 21.27 Job 7.11 Job 10.1 Jean 12.27 2 Rois 4.27
16 Ee Bwana, kwa mambo hayo watu huishi; Na uhai wa roho yangu u katika hayo yote; Kwa hiyo uniponye na kunihuisha.Deutéronome 8.3 Psaumes 119.25 2 Corinthiens 4.17 Esaïe 64.5 1 Corinthiens 11.32
17 Tazama; nalikuwa na uchungu mwingi kwa ajili ya amani yangu; Lakini kwa kunipenda umeniokoa na shimo la uharibifu; Kwa maana umezitupa dhambi zangu zote nyuma yako.Esaïe 43.25 Jérémie 31.34 Psaumes 30.3 Jonas 2.6 Psaumes 86.13
18 Kwa kuwa kuzimu hakuwezi kukusifu; mauti haiwezi kukuadhimisha; Wale washukao shimoni hawawezi kuitarajia kweli yako.Ecclésiaste 9.10 Psaumes 30.9 Psaumes 6.5 Nombres 16.33 Psaumes 115.17-115.18
19 Aliye hai, naam, aliye hai, ndiye atakayekusifu, kama mimi leo; Baba atawajulisha watoto kweli yako.Deutéronome 6.7 Deutéronome 4.9 Psaumes 78.3-78.6 Joël 1.3 Josué 4.21-4.22
20 Bwana yu tayari kunipa wokovu. Basi, kwa vinubi tutaziimba nyimbo zangu, Siku zote za maisha yetu nyumbani mwa Bwana.Psaumes 33.2 Psaumes 145.2 Psaumes 30.11-30.12 Psaumes 51.15 Psaumes 68.25
21 Maana Isaya amesema, Na watwae mkate wa tini, wakauweke juu ya jipu, naye atapona.Jean 9.6 Marc 7.33 2 Rois 20.7-20.8
22 Tena Hezekia alikuwa amesema, Iko ishara gani ya kunionyesha ya kuwa nitapanda niingie nyumbani mwa Bwana?Jean 5.14 Psaumes 118.18-118.19 Psaumes 122.1 2 Rois 20.8 Psaumes 42.1-42.2

Cette Bible est dans le domaine public.