Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Lamentations 5.13
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Bwana, kumbuka yaliyotupata; Utazame na kuiona aibu yetu.Psaumes 44.13-44.16 Lamentations 3.61 Luc 23.42 Habakuk 3.2 Lamentations 1.20
2 Urithi wetu umegeuka kuwa mali ya wageni; Na nyumba zetu kuwa mali ya makafiri.Sophonie 1.13 Esaïe 1.7 Ezéchiel 7.21 Jérémie 6.12 Psaumes 79.1-79.2
3 Tumekuwa yatima waliofiwa na baba; Mama zetu wamekuwa kama wajane.Jérémie 18.21 Exode 22.24 Osée 14.3 Jérémie 15.8
4 Tumekunywa maji yetu kwa fedha; Kuni zetu twauziwa.Esaïe 3.1 Ezéchiel 4.9-4.17 Deutéronome 28.48
5 Watufuatiao wa juu ya shingo zetu; Tumechoka tusipate raha yo yote.Néhémie 9.36-9.37 Jérémie 28.14 Lamentations 4.19 Lamentations 1.14 Jérémie 27.11-27.12
6 Tumewapa hao Wamisri mkono; Na Waashuri nao, ili tushibe chakula.Osée 12.1 Osée 9.3 Esaïe 31.1-31.3 Esaïe 30.1-30.6 Osée 7.11
7 Baba zetu walitenda dhambi hata hawako; Na sisi tumeyachukua maovu yao.Jérémie 16.12 Ezéchiel 18.2 Jérémie 31.29 Jérémie 14.20 Exode 20.5
8 Watumwa wanatutawala; Hakuna mtu wa kutuokoa na mikono yao.Zacharie 11.6 Néhémie 5.15 Proverbes 30.22 Psaumes 7.2 Esaïe 43.13
9 Twapata chakula kwa kujihatarisha nafsi zetu; Kwa sababu ya upanga wa nyikani.Jérémie 40.9-40.12 Juges 6.11 Jérémie 42.16 Ezéchiel 12.18-12.19 2 Samuel 23.17
10 Ngozi yetu ni nyeusi kama tanuu; Kwa sababu ya hari ya njaa ituteketezayo.Lamentations 4.8 Job 30.30 Lamentations 3.4 Psaumes 119.83
11 Huwatia jeuri wanawake katika Sayuni; Na mabikira katika miji ya Yuda.Zacharie 14.2 Esaïe 13.16 Deutéronome 28.30
12 Wakuu hutungikwa kwa mikono yao; Nyuso za wazee hazipewi heshima.Lamentations 4.16 Esaïe 47.6 Jérémie 39.6-39.7 Jérémie 52.10-52.11 Jérémie 52.25-52.27
13 Vijana huyachukua mawe ya kusagia; Na watoto hujikwaa chini ya kuni.Juges 16.21 Exode 11.5 Exode 23.5 Exode 1.11 Esaïe 58.6
14 Wazee wameacha kwenda langoni; Na vijana kwenda ngomani.Jérémie 7.34 Deutéronome 16.18 Job 30.31 Lamentations 2.10 Jérémie 16.9
15 Furaha ya mioyo yetu imekoma; Machezo yetu yamegeuka maombolezo.Amos 8.10 Psaumes 30.11 Jacques 4.9-4.10 Jérémie 25.10 Amos 6.4-6.7
16 Taji ya kichwa chetu imeanguka; Ole wetu! Kwa kuwa tumetenda dhambi.Psaumes 89.39 Esaïe 3.9-3.11 Jérémie 13.18 Lamentations 1.1 Job 19.9
17 Kwa sababu hiyo mioyo yetu imezimia; Kwa ajili ya hayo macho yetu hayaoni vema.Esaïe 1.5 Lamentations 2.11 Job 17.7 Psaumes 6.7 Esaïe 38.14
18 Kwa ajili ya mlima Sayuni ulio ukiwa, Mbweha hutembea juu yake.Michée 3.12 Jérémie 17.3 Jérémie 26.9 1 Rois 9.7-9.8 Jérémie 9.11
19 Wewe, Bwana, unadumu milele; Kiti chako cha enzi ni tangu kizazi hata kizazi.Psaumes 102.12 Psaumes 45.6 Psaumes 102.25-102.27 Psaumes 9.7 Psaumes 145.13
20 Mbona watusahau sikuzote; Na kutuacha muda huu mwingi?Psaumes 13.1 Psaumes 44.24 Psaumes 85.5 Esaïe 64.9-64.12 Psaumes 79.5
21 Ee Bwana, utugeuze kwako, nasi tutageuka; Zifanye mpya siku zetu kama siku za kale.Psaumes 80.3 Jérémie 31.18 Psaumes 80.7 Psaumes 80.19 Jérémie 33.13
22 Isipokuwa wewe umetukataa kabisa; Nawe una hasira nyingi sana juu yetu.Psaumes 60.1-60.2 Osée 1.6 Psaumes 44.9 Jérémie 15.1-15.5 Esaïe 64.9

Cette Bible est dans le domaine public.