Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Lamentations 5
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Bwana, kumbuka yaliyotupata; Utazame na kuiona aibu yetu. Psaumes 44.13-44.16 Lamentations 3.61 Psaumes 79.12 Lamentations 3.19 Lamentations 2.15
2 Urithi wetu umegeuka kuwa mali ya wageni; Na nyumba zetu kuwa mali ya makafiri. Sophonie 1.13 Esaïe 1.7 Esaïe 5.17 Esaïe 63.18 Deutéronome 28.30-28.68
3 Tumekuwa yatima waliofiwa na baba; Mama zetu wamekuwa kama wajane. Jérémie 18.21 Exode 22.24 Jérémie 15.8 Osée 14.3
4 Tumekunywa maji yetu kwa fedha; Kuni zetu twauziwa. Esaïe 3.1 Ezéchiel 4.9-4.17 Deutéronome 28.48
5 Watufuatiao wa juu ya shingo zetu; Tumechoka tusipate raha yo yote. Néhémie 9.36-9.37 Jérémie 27.2 Actes 15.10 Jérémie 27.8 Deutéronome 28.65-28.66
6 Tumewapa hao Wamisri mkono; Na Waashuri nao, ili tushibe chakula. Osée 9.3 Osée 12.1 Osée 5.13 Genèse 24.2 Jérémie 44.12-44.14
7 Baba zetu walitenda dhambi hata hawako; Na sisi tumeyachukua maovu yao. Jérémie 16.12 Ezéchiel 18.2 Jérémie 31.29 Zacharie 1.5 Jérémie 14.20
8 Watumwa wanatutawala; Hakuna mtu wa kutuokoa na mikono yao. Zacharie 11.6 Néhémie 5.15 Proverbes 30.22 Psaumes 7.2 Psaumes 50.22
9 Twapata chakula kwa kujihatarisha nafsi zetu; Kwa sababu ya upanga wa nyikani. Jérémie 40.9-40.12 2 Samuel 23.17 Jérémie 41.18 Jérémie 42.14 Ezéchiel 4.16-4.17
10 Ngozi yetu ni nyeusi kama tanuu; Kwa sababu ya hari ya njaa ituteketezayo. Lamentations 4.8 Job 30.30 Lamentations 3.4 Psaumes 119.83
11 Huwatia jeuri wanawake katika Sayuni; Na mabikira katika miji ya Yuda. Zacharie 14.2 Esaïe 13.16 Deutéronome 28.30
12 Wakuu hutungikwa kwa mikono yao; Nyuso za wazee hazipewi heshima. Lamentations 4.16 Esaïe 47.6 Jérémie 52.10-52.11 Jérémie 52.25-52.27 Lamentations 2.10
13 Vijana huyachukua mawe ya kusagia; Na watoto hujikwaa chini ya kuni. Juges 16.21 Néhémie 5.1-5.5 Esaïe 47.2 Exode 2.11 Matthieu 23.4
14 Wazee wameacha kwenda langoni; Na vijana kwenda ngomani. Jérémie 7.34 Lamentations 1.4 Ezéchiel 26.13 Job 29.7-29.17 Esaïe 3.2-3.3
15 Furaha ya mioyo yetu imekoma; Machezo yetu yamegeuka maombolezo. Amos 8.10 Jacques 4.9-4.10 Jérémie 25.10 Amos 6.4-6.7 Psaumes 30.11
16 Taji ya kichwa chetu imeanguka; Ole wetu! Kwa kuwa tumetenda dhambi. Psaumes 89.39 Jérémie 13.18 Esaïe 3.9-3.11 Lamentations 1.1 Job 19.9
17 Kwa sababu hiyo mioyo yetu imezimia; Kwa ajili ya hayo macho yetu hayaoni vema. Esaïe 1.5 Lamentations 2.11 Job 17.7 Psaumes 6.7 Lamentations 1.22
18 Kwa ajili ya mlima Sayuni ulio ukiwa, Mbweha hutembea juu yake. Michée 3.12 Jérémie 9.11 Jérémie 52.13 Psaumes 74.2-74.3 Lamentations 2.8-2.9
19 Wewe, Bwana, unadumu milele; Kiti chako cha enzi ni tangu kizazi hata kizazi. Psaumes 102.12 Psaumes 45.6 Psaumes 102.25-102.27 Psaumes 145.13 Psaumes 9.7
20 Mbona watusahau sikuzote; Na kutuacha muda huu mwingi? Psaumes 13.1 Psaumes 44.24 Psaumes 89.46 Psaumes 77.7-77.10 Psaumes 94.3-94.4
21 Ee Bwana, utugeuze kwako, nasi tutageuka; Zifanye mpya siku zetu kama siku za kale. Psaumes 80.3 Jérémie 31.18 Psaumes 80.19 Psaumes 80.7 Zacharie 8.3-8.6
22 Isipokuwa wewe umetukataa kabisa; Nawe una hasira nyingi sana juu yetu. Psaumes 60.1-60.2 Psaumes 44.9 Jérémie 15.1-15.5 Esaïe 64.9 Ezéchiel 37.11

Cette Bible est dans le domaine public.