Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Ezéchiel 28.23
Bible en Swahili de l’est


1 Neno la Bwana likanijia tena, kusema, 2 Mwanadamu, mwambie mkuu wa Tiro, Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa moyo wako umeinuka, nawe umesema, Mimi ni Mungu, nami nimeketi katika kiti cha Mungu, kati ya bahari; lakini u mwanadamu wala si Mungu, ujapokuwa umeweka moyo wako kama moyo wa Mungu.Ezéchiel 28.9 2 Thessaloniciens 2.4 Esaïe 31.3 Esaïe 14.13-14.14 Psaumes 9.20
3 Tazama, una hekima kuliko Danieli; hapana neno la siri watu wawezalo kukuficha;Daniel 5.11-5.12 Daniel 1.20 Daniel 2.22 Job 15.8 Psaumes 25.14
4 kwa hekima yako na kwa fahamu zako umejipatia utajiri, nawe umepata dhahabu na fedha katika hazina zako;Ecclésiaste 9.11 Ezéchiel 29.3 Proverbes 18.11 Deutéronome 8.17-8.18 Zacharie 9.2-9.4
5 kwa hekima yako nyingi, na kwa biashara yako, umeongeza utajiri wako, na moyo wako umeinuka kwa sababu ya utajiri wako;Psaumes 62.10 Psaumes 52.7 Ezéchiel 28.2 Osée 13.6 Job 31.24-31.25
6 basi, kwa hiyo, Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa umeweka moyo wako kama moyo wa Mungu;Ezéchiel 28.2 Exode 9.17 2 Thessaloniciens 2.4 Job 40.9-40.12 1 Corinthiens 10.22
7 basi, tazama, nitaleta wageni juu yako, watu wa mataifa wenye kutisha; nao watafuta panga zao juu ya uzuri wa hekima yako, nao watautia uchafu mwangaza wako.Ezéchiel 31.12 Ezéchiel 32.12 Ezéchiel 30.11 Habakuk 1.6-1.8 Amos 3.6
8 Watakushusha hata shimoni; nawe utakufa kifo chao waliouawa kati ya bahari.Ezéchiel 27.26-27.27 Ezéchiel 27.34 Psaumes 28.1 Job 33.18 Ezéchiel 32.18-32.30
9 Je! Utazidi kusema mbele yake huyo akuuaye, Mimi ni Mungu? Lakini u mwanadamu, wala si Mungu, mkononi mwake akutiaye jeraha.Ezéchiel 28.2 Psaumes 82.7 Esaïe 31.3 Actes 12.22-12.23 Daniel 4.31-4.32
10 Utakufa kifo cha hao wasiotahiriwa, kwa mikono ya wageni; kwa maana mimi nimenena neno hili, asema Bwana MUNGU.Ezéchiel 31.18 Ezéchiel 32.19 Ezéchiel 32.21 1 Samuel 17.26 1 Samuel 17.36
11 Tena neno la Bwana likanijia, kusema, 12 Mwanadamu, umfanyie maombolezo mfalme wa Tiro, umwambie, Bwana MUNGU asema hivi; Wewe wakitia muhuri kipimo, umejaa hekima, na ukamilifu wa uzuri.Ezéchiel 19.1 Ezéchiel 26.17 Ezéchiel 27.2-27.4 Jacques 3.13-3.18 Ezéchiel 19.14
13 Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari.Ezéchiel 31.8-31.9 Genèse 2.8 Ezéchiel 27.16 Esaïe 30.32 Esaïe 51.3
14 Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto.Exode 40.9 Exode 30.26 Ezéchiel 20.40 Exode 25.17-25.20 Apocalypse 18.16
15 Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako.Ezéchiel 27.3-27.4 Genèse 1.26-1.27 Ezéchiel 28.17-28.18 Ezéchiel 28.3-28.6 Ezéchiel 28.12
16 Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto.Habakuk 2.17 Habakuk 2.8 Ezéchiel 8.17 Genèse 3.24 Michée 2.2
17 Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama.Ezéchiel 28.2 Ezéchiel 28.5 Ezéchiel 31.10 1 Corinthiens 1.19-1.21 Job 40.11-40.12
18 Kwa wingi wa maovu yako, katika uovu wa uchuuzi wako, umepatia unajisi patakatifu pako; basi nimetokeza moto kutoka ndani yako, nao umekuteketeza, nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu wote wakutazamao.Malachie 4.3 Amos 1.9-1.10 Apocalypse 18.8 Ezéchiel 5.4 2 Pierre 2.6
19 Wote wakujuao kati ya kabila za watu watakustaajabia; umekuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwapo tena hata milele.Ezéchiel 26.21 Ezéchiel 26.14 Apocalypse 18.15-18.19 Apocalypse 18.21 Esaïe 14.16-14.19
20 Neno la Bwana likanijia, kusema, 21 Mwanadamu, uuelekezee Sidoni uso wako, ukatabiri juu yake,Ezéchiel 6.2 Genèse 10.15 Ezéchiel 27.8 Ezéchiel 25.2 Jérémie 25.22
22 useme, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu yako, Ee Sidoni, nami natukuzwa kati yako; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapokuwa nimetekeleza hukumu zangu ndani yake, na kutakasika ndani yake.Ezéchiel 39.13 Exode 14.4 Exode 14.17 Ezéchiel 20.41 Apocalypse 19.1-19.2
23 Maana nitampelekea tauni, na damu, katika njia kuu zake, na hao waliotiwa jeraha wataanguka kati yake, kwa upanga juu yake pande zote; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.Ezéchiel 38.22 Ezéchiel 5.12 Jérémie 15.2 Ezéchiel 25.7 Ezéchiel 26.6
24 Wala hautakuwapo mchongoma uchomao kwa nyumba ya Israeli; wala mwiba uumizao miongoni mwa wote wamzungukao, waliowatenda mambo ya jeuri; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana MUNGU.Josué 23.13 Nombres 33.55 2 Corinthiens 12.7 Esaïe 55.13 Jérémie 12.14
25 Bwana MUNGU asema hivi; Nitakapokuwa nimewakusanya nyumba ya Israeli, na kuwatoa katika watu ambao wametawanyika kati yao, na kutakasika kati yao machoni pa mataifa, ndipo watakapokaa katika nchi yao wenyewe, niliyompa mtumishi wangu, Yakobo.Ezéchiel 20.41 Jérémie 23.8 Ezéchiel 11.17 Ezéchiel 37.25 Psaumes 106.47
26 Nao watakaa humo salama; naam, watajenga nyumba, na kupanda mashamba ya mizabibu, na kukaa salama; nitakapokuwa nimetekeleza hukumu zangu juu ya watu wote, wanaowatenda mambo ya jeuri pande zote; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wao.Ezéchiel 28.22 Ezéchiel 28.24 Ezéchiel 38.8 Jérémie 32.15 Ezéchiel 34.25-34.28

Cette Bible est dans le domaine public.