Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Osée 5.6
Bible en Swahili de l’est


1 Sikieni haya, enyi makuhani, sikilizeni, enyi nyumba ya Israeli, tegeni masikio yenu, enyi wa nyumba ya mfalme, kwa kuwa hukumu hii yawahusu ninyi; maana mmekuwa mtego huko Mizpa, na wavu uliotandwa juu ya Tabori.Osée 9.8 Osée 6.9 Osée 4.1 Juges 4.6 1 Rois 21.18-21.22
2 Nao walioasi wameongeza sana ufisadi wao; lakini mimi ndiye awakaripiaye wote pia.Osée 9.15 Esaïe 29.15 Osée 6.9 Jérémie 18.18 Osée 4.2
3 Mimi namjua Efraimu, wala Israeli hakufichwa nisimwone; maana sasa, Ee Efraimu, umefanya uzinzi; Israeli ametiwa unajisi.Amos 3.2 1 Rois 14.14-14.16 Osée 4.17-4.18 Osée 12.1 Ezéchiel 23.5-23.21
4 Matendo yao hayatawaacha kumgeukia Mungu wao; maana roho ya uzinzi imo ndani yao, wala hawamjui Bwana.Osée 4.12 1 Jean 2.3-2.4 Jean 8.55 Psaumes 9.10 Jérémie 22.15-22.16
5 Na kiburi cha Israeli chamshuhudia mbele ya uso wake; kwa sababu hiyo, Israeli na Efraimu watajikwaa katika uovu wao. Yuda naye atajikwaa pamoja nao.Osée 7.10 Ezéchiel 23.31-23.35 Amos 5.2 Luc 19.22 Esaïe 9.9-9.10
6 Watakwenda na makundi yao ya kondoo na ng’ombe wamtafute Bwana; lakini hawatamwona; amejitenga nao.Michée 6.6-6.7 Proverbes 1.28 Jean 7.34 Ezéchiel 8.6 Proverbes 15.8
7 Wametenda kwa hila juu ya Bwana; maana wamezaa wana wageni; sasa mwezi huu uandamao utawala pamoja na mashamba yao.Osée 6.7 Jérémie 3.20 Esaïe 48.8 Ezéchiel 12.28 Zacharie 11.8
8 Pigeni tarumbeta katika Gibea, na baragumu katika Rama; pazeni sauti ya hofu katika Beth-Aveni; nyuma yako, Ee Benyamini!Osée 9.9 Osée 4.15 Joël 2.1 Jérémie 4.5 1 Samuel 15.34
9 Efraimu atakuwa ukiwa siku ya kukemewa; katika kabila za Israeli nimetangaza habari itakayotokea halafu bila shaka.Esaïe 46.10 Osée 9.11-9.17 Zacharie 1.6 Esaïe 28.1-28.4 Osée 11.5-11.6
10 Wakuu wa Yuda ni kama watu waondoao alama ya mpaka; nitawamwagia ghadhabu yangu kama maji.Deutéronome 19.14 Deutéronome 27.17 Psaumes 32.6 Psaumes 93.3-93.4 Ezéchiel 7.8
11 Efraimu ameonewa, amesetwa katika hukumu, kwa sababu alikuwa radhi kufuata ubatili.Deutéronome 28.33 Michée 6.16 1 Rois 12.26-12.33 Amos 5.11-5.12 2 Rois 15.29
12 Kwa sababu hiyo mimi nimekuwa kama nondo kwa Efraimu, nimekuwa kama ubovu kwa nyumba ya Yuda.Esaïe 51.8 Job 13.28 Marc 9.43-9.48 Jonas 4.7 Esaïe 50.9
13 Efraimu alipouona ugonjwa wake, na Yuda jeraha yake, ndipo Efraimu alipokwenda kwa Ashuru, akatuma watu kwa mfalme Yarebu; lakini yeye hawezi kuwapoza, wala hatawaponya jeraha yenu.Osée 7.11 Osée 12.1 Osée 10.6 Jérémie 30.12 2 Rois 15.19
14 Maana mimi nitakuwa kama simba kwa Efraimu, na kama mwana-simba kwa nyumba ya Yuda; mimi, naam, mimi nitararua, kisha nitakwenda zangu; nitachukulia mbali, wala hapatakuwa na mtu wa kupokonya.Michée 5.8 Psaumes 7.2 Osée 13.7-13.8 Esaïe 5.29 Psaumes 50.22
15 Nitakwenda zangu niparudie mahali pangu, hata watakapoungama makosa yao na kunitafuta uso wangu; katika taabu yao watanitafuta kwa bidii.Esaïe 26.16 Psaumes 78.34 Psaumes 50.15 Jérémie 29.12-29.14 Jérémie 2.27

Cette Bible est dans le domaine public.