Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Zacharie 11.16
Bible en Swahili de l’est


1 Ifungue milango yako, Ee Lebanoni, Ili moto uiteketeze mierezi yako.Jérémie 22.6-22.7 Jérémie 22.23 Luc 21.23-21.24 Deutéronome 32.22 Habakuk 2.8
2 Piga yowe, msunobari, maana mwerezi umeanguka, Kwa sababu miti iliyo mizuri imeharibika; Pigeni yowe, enyi mialoni ya Bashani, Kwa maana msitu wenye nguvu umeangamia.Ezéchiel 20.46 Nahum 3.8-3.19 Esaïe 32.15-32.19 Esaïe 10.33-10.34 Ezéchiel 31.2-31.3
3 Sauti ya wachungaji, ya uchungu mwingi! Kwa maana utukufu wao umeharibika; Sauti ya ngurumo ya wana-simba! Kwa maana kiburi cha Yordani kimeharibika.Jérémie 50.44 Jérémie 25.34-25.36 Actes 22.21-22.22 1 Samuel 4.21-4.22 Matthieu 15.14
4 Bwana, Mungu wangu, alisema hivi, Lilishe kundi la machinjo,Zacharie 11.7 Zacharie 14.5 Romains 15.8 Jean 20.17 Esaïe 49.4-49.5
5 ambalo wenye kundi hilo huwachinja, kisha hujiona kuwa hawana hatia; na hao wawauzao husema, Na ahimidiwe Bwana, kwa maana mimi ni tajiri; na wachungaji wao wenyewe hawawahurumii.Jérémie 50.7 Osée 12.8 1 Timothée 6.5-6.10 Ezéchiel 34.2-34.4 Jérémie 23.1-23.2
6 Maana mimi sitawahurumia tena wenyeji wa nchi hii, asema Bwana; bali, tazama, nitawatia, kila mmoja wao, mikononi mwa mwenzake, na mikononi mwa mfalme; nao wataipiga hiyo nchi, wala mimi sitawaokoa mikononi mwao.Jérémie 13.14 Esaïe 9.19-9.21 Matthieu 22.7 Michée 5.8 Hébreux 10.26-10.31
7 Basi nikalilisha kundi la machinjo, kweli kondoo waliokuwa wanyonge kabisa.Zacharie 11.4 Zacharie 11.14 Esaïe 11.4 Sophonie 3.12 Esaïe 61.1
8 Nami nikawakatilia mbali wachungaji watatu katika mwezi mmoja; maana nafsi yangu ilikuwa imechoka kwa ajili yao, na nafsi zao pia walinichukia.Esaïe 49.7 Osée 5.7 Jean 7.7 Matthieu 23.34-23.36 Hébreux 10.38
9 Ndipo nikasema, Sitawalisheni; afaye na afe; atakayekatiliwa mbali na akatiliwe mbali; nao waliosalia, kila mmoja na ale nyama ya mwili wa mwenziwe.Jérémie 43.11 Jean 12.35 Jean 8.24 Actes 13.46-13.47 Matthieu 21.19
10 Nikaitwaa hiyo fimbo yangu, iitwayo Neema, nikaikata vipande viwili, ili nipate kulivunja agano langu nililolifanya na watu wa kabila zote.Zacharie 11.7 Jérémie 14.21 Psaumes 89.39 Jérémie 31.31-31.32 Ezéchiel 7.20-7.22
11 Nayo ikavunjwa siku ile; na hivyo wale kondoo wanyonge walionisikiliza wakajua ya kuwa neno hili ndilo neno la Bwana.Sophonie 3.12 Esaïe 26.8-26.9 Luc 2.25 Lamentations 3.25-3.26 Deutéronome 31.29
12 Nikawaambia, Mkiona vema, nipeni ujira wangu; kama sivyo, msinipe. Basi wakanipimia vipande thelathini vya fedha, kuwa ndio ujira wangu.Matthieu 26.15 Exode 21.32 Luc 22.3-22.6 Genèse 37.28 Marc 14.10-14.11
13 Kisha Bwana akaniambia, Mtupie mfinyanzi kima kizuri, hicho nilichotiwa kima na watu hao. Basi nikavitwaa vile vipande thelathini vya fedha, nikamtupia huyo mfinyanzi ndani ya nyumba ya Bwana.Actes 1.18-1.19 Matthieu 27.3-27.10 Matthieu 27.12 Esaïe 53.2-53.3 Actes 4.11
14 Ndipo nikaikata vipande viwili fimbo yangu ya pili, iitwayo Vifungo, ili nipate kuuvunja udugu uliokuwa kati ya Yuda na Israeli.Esaïe 9.21 Jacques 3.16 Ezéchiel 37.16-37.20 Esaïe 11.13 Matthieu 24.10
15 Bwana akaniambia, Jitwalie tena vyombo vya mchungaji mpumbavu.Esaïe 6.10-6.12 Ezéchiel 13.3 Jérémie 2.26-2.27 Luc 11.40 Matthieu 15.14
16 Kwa maana, tazama, mimi nitainua katika nchi hii mchungaji, ambaye hatawaangalia waliopotea, wala hatawatafuta waliotawanyika, wala hatamganga aliyevunjika, wala hatamlisha aliye mzima; bali atakula nyama ya wanono, na kuzirarua-rarua kwato zao.Jérémie 23.2 Ezéchiel 34.2-34.6 Esaïe 40.11 Ezéchiel 34.10 1 Samuel 17.34-17.35
17 Ole wake mchungaji asiyefaa, aliachaye kundi! Upanga utakuwa juu ya mkono wake, na juu ya jicho lake la kuume; mkono wake utakuwa umekauka kabisa, na jicho lake la kuume litakuwa limepofuka.Jérémie 23.1 Jérémie 23.32 Ezéchiel 13.3 Ezéchiel 34.2 Jérémie 50.35-50.37

Cette Bible est dans le domaine public.