Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Matthieu 1.22
Bible en Swahili de l’est


1 Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu.Genèse 22.18 Apocalypse 22.16 Galates 3.16 Romains 1.3 Psaumes 132.11
2 Ibrahimu alimzaa Isaka; Isaka akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake;Actes 7.8 Genèse 25.26 Josué 24.2-24.4 Genèse 46.8-46.27 Genèse 30.5-30.20
3 Yuda akamzaa Peresi na Zera kwa Tamari; Peresi akamzaa Esromu; Esromu akamzaa Aramu;Genèse 46.12 Genèse 38.29-38.30 1 Chroniques 2.1-2.15 Luc 3.33 1 Chroniques 4.1
4 Aramu akamzaa Aminadabu; Aminadabu akamzaa Nashoni; Nashoni akamzaa Salmoni;Luc 3.32 Ruth 4.19-4.20 1 Chroniques 2.10-2.12 Nombres 10.14 Nombres 7.12
5 Salmoni akamzaa Boazi kwa Rahabu; Boazi akamzaa Obedi kwa Ruthu; Obedi akamzaa Yese;Hébreux 11.31 Jacques 2.25 Ruth 1.16-1.17 Josué 6.22-6.25 Josué 2.1-2.22
6 Yese akamzaa mfalme Daudi; Daudi akamzaa Suleimani kwa yule mke wa uria;1 Samuel 17.12 1 Samuel 16.1 2 Samuel 12.24-12.25 1 Samuel 17.58 1 Chroniques 11.41
7 Sulemani akamzaa Rehoboamu; Rehoboamu akamzaa Abiya; Abiya akamzaa Asa;1 Chroniques 3.10-3.14 1 Rois 15.8-15.23 2 Chroniques 13.7 1 Rois 11.43-12.24 2 Chroniques 14.1-14.15
8 Asa akamzaa Yehoshafati; Yehoshafati akamzaa Yoramu; Yoramu akamzaa Uzia;1 Chroniques 3.11 2 Rois 3.1 2 Chroniques 17.1-17.19 2 Chroniques 21.1 2 Rois 8.16
9 Uzia akamzaa Yothamu; Yothamu akamzaa Ahazi; Ahazi akamzaa Hezekia;Esaïe 36.1-36.22 2 Rois 18.1-18.20 2 Rois 15.32-16.20 2 Chroniques 27.1-29.32 Esaïe 7.1-7.13
10 Hezekia akamzaa Manase; Manase akamzaa Amoni; Amoni akamzaa Yosia;2 Rois 24.3-24.4 Jérémie 1.2-1.3 1 Chroniques 3.13-3.15 2 Chroniques 32.33-35.27 2 Rois 20.21-23.30
11 Yosia akamzaa Yekonia na ndugu zake, wakati wa ule uhamisho wa Babeli.Jérémie 27.20 Daniel 1.2 Jérémie 52.28-52.30 2 Rois 25.11 Jérémie 39.9
12 Na baada ya ule uhamisho wa Babeli, Yekonia akamzaa Shealtieli; Shealtieli akamzaa Zerubabeli;1 Chroniques 3.17 Esdras 3.2 Luc 3.27 Esdras 5.2 Aggée 1.1
13 Zerubabeli akamzaa Abihudi; Abihudi akamzaa Eliakimu; Eliakimu akamzaa Azori; 14 Azori akamzaa Sadoki; Sadoki akamzaa Akimu; Akimu akamzaa Eliudi; 15 Eliudi akamzaa Eleazari; Eleazari akamzaa Matani; Matani akamzaa Yakobo; 16 Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo.Matthieu 27.17 Luc 3.23 Matthieu 27.22 Jean 4.25 Luc 1.27
17 Basi vizazi vyote tangu Ibrahimu hata Daudi ni vizazi kumi na vinne; na tangu Daudi hata ule uhamisho wa Babeli ni vizazi kumi na vinne; na tangu ule uhamisho wa Babeli hata Kristo ni vizazi kumi na vinne.Jérémie 27.20 Matthieu 11.2 Matthieu 1.11-1.12 Jean 1.41 2 Rois 24.14
18 Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.Job 14.4 Matthieu 1.1 Genèse 3.15 Job 15.14 Luc 1.25
19 Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri.Deutéronome 22.21-22.24 Deutéronome 24.1-24.4 Jean 8.4-8.5 Lévitique 19.20 Marc 6.20
20 Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.Matthieu 1.18 Joël 2.28 Nombres 12.6 Job 4.13-4.16 Luc 2.4
21 Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.Actes 13.23 Luc 2.21 Actes 4.12 Actes 5.31 Jean 1.29
22 Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema,Luc 24.44 Matthieu 2.23 Matthieu 2.15 Jean 12.38-12.40 Jean 10.35
23 Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.Esaïe 7.14 Esaïe 9.6-9.7 Psaumes 46.11 1 Timothée 3.16 Jean 1.14
24 Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe;Jean 15.14 2 Rois 5.11-5.14 Genèse 6.22 Genèse 22.2-22.3 Genèse 7.5
25 asimjue kamwe hata alipomzaa mwanawe; akamwita jina lake YESU.Matthieu 1.21 Luc 2.21 Luc 2.7 Exode 13.2 Exode 22.29

Cette Bible est dans le domaine public.