Les bêtes
1 Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.
Apocalypse 12.3 Apocalypse 17.3 Apocalypse 11.7 Daniel 11.36 Daniel 7.23-7.25
2 Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.
Apocalypse 16.10 Apocalypse 20.2 Apocalypse 17.12 Esaïe 5.29 Apocalypse 12.13
3 Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.
Apocalypse 17.8 Apocalypse 13.14 Apocalypse 17.13 Apocalypse 17.10 Jean 12.19
4 Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye?
Apocalypse 18.18 Apocalypse 13.2 Daniel 11.36-11.37 1 Samuel 17.24 Apocalypse 9.20
5 Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.
Daniel 11.36 Daniel 7.8 Daniel 7.11 Daniel 7.25 Apocalypse 12.6
6 Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni.
Apocalypse 12.12 Apocalypse 4.4 Apocalypse 4.1 Matthieu 15.19 Apocalypse 19.1-19.6
7 Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa.
Apocalypse 11.7 Daniel 7.21 Daniel 7.25 Apocalypse 12.17 Daniel 12.1
8 Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.
1 Pierre 1.19-1.20 Ephésiens 1.4 Matthieu 25.34 Apocalypse 17.8 Apocalypse 3.5
9 Mtu akiwa na sikio na asikie.
Apocalypse 2.7 Apocalypse 2.17 Apocalypse 2.29 Apocalypse 2.11
10 Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hapa ndipo penye subira na imani ya watakatifu.
Hébreux 6.12 Esaïe 33.1 Apocalypse 14.12 Jacques 5.7-5.8 Jacques 1.2-1.4
11 Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka.
Matthieu 7.15 Apocalypse 17.6 Daniel 7.8 Daniel 7.24-7.25 2 Corinthiens 11.13-11.15
12 Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona.
Apocalypse 13.14-13.17 Apocalypse 17.10-17.11 2 Thessaloniciens 2.4 Apocalypse 19.20 Apocalypse 14.11
13 Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu.
Apocalypse 20.9 Apocalypse 19.20 1 Rois 18.38 Matthieu 24.24 Apocalypse 16.14
14 Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi.
Apocalypse 19.20 Apocalypse 12.9 Apocalypse 13.8 2 Rois 20.7 Job 12.16
15 Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe.
Apocalypse 16.2 Apocalypse 20.4 Apocalypse 19.20 Genèse 2.7 Apocalypse 16.5
16 Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao;
Apocalypse 19.18 Apocalypse 20.4 Apocalypse 7.3 Apocalypse 19.5 Apocalypse 19.20
17 tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.
Apocalypse 14.11 Apocalypse 15.2 Apocalypse 13.18 Apocalypse 13.16 Apocalypse 22.4
18 Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.Apocalypse 15.2 Apocalypse 17.9 Apocalypse 21.17 Daniel 12.10 Apocalypse 1.3