Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
1 Samuel 9.2 Bible en Swahili de l’est
Saül auprès de Samuel à Rama
1 Basi, kulikuwa na mtu mmoja wa Benyamini, jina lake akiitwa Kishi, mwana wa Abieli, mwana wa Serori, mwana wa Bekorathi, mwana wa Afia, mwana wa Mbenyamini, mtu shujaa, mwenye nguvu. 1 Samuel 14.51 1 Chroniques 9.36-9.39 1 Samuel 25.2 1 Chroniques 8.30-8.33 2 Samuel 19.32 2 Naye alikuwa na mwana, aliyeitwa jina lake Sauli, kijana, tena mzuri; wala katika wana wa Israeli hakuwako mtu mzuri kuliko yeye; tangu mabega yake kwenda juu alikuwa mrefu kuliko watu wote. 1 Samuel 17.4 1 Samuel 16.7 2 Samuel 14.25-14.26 Genèse 6.2 1 Samuel 10.23-10.24 3 Na punda za Kishi, baba yake Sauli, walikuwa wamepotea. Kishi akamwambia Sauli mwanawe, Haya basi, twaa mtumishi mmoja pamoja nawe, uondoke, uende ukawatafute punda hao. 1 Samuel 10.2 Juges 10.4 Juges 5.10 4 Naye akapita kati ya nchi ya milima milima ya Efraimu, akapita na kati ya nchi ya Shalisha, lakini hawakuwaona; kisha wakapita kati ya nchi ya Shaalimu, wala huko hawakuwako; wakapita kati ya nchi ya Wabenyamini, lakini hawakuwapata. 2 Rois 4.42 Josué 24.33 Genèse 33.18 Jean 3.23 Juges 17.1 5 Hata walipofika nchi ya Sufu, Sauli akamwambia yule mtumishi aliyefuatana naye, Haya, na turudi, baba yangu asije akaacha kufikiri habari za punda akatufikiri sisi. 1 Samuel 10.2 1 Samuel 1.1 Luc 12.11 Luc 12.22 Matthieu 6.34 6 Naye akamwambia, Tazama, katika mji huu mna mtu wa Mungu, naye ni mtu mwenye kuheshimiwa; yote asemayo hutukia kweli kweli; basi, twende huko; labda yeye aweza kutuambia habari ya safari yetu tunayoiendea. Deutéronome 33.1 1 Rois 13.1 2 Rois 6.6 1 Samuel 3.19-3.20 Esaïe 44.26 7 Ndipo Sauli akamwambia mtumishi wake, Lakini angalia, kama tukienda, tumpelekee mtu huyo kitu gani? Maana chakula kimekwisha vyomboni mwetu, wala hapana zawadi ya kumpelekea mtu wa Mungu; tuna nini sisi? 1 Rois 14.3 2 Rois 8.8 2 Rois 5.5 2 Rois 4.42 Juges 6.18 8 Yule mtumishi akamjibu Sauli, akasema, Tazama, mkononi mwangu nina robo ya shekeli ya fedha; nitampa huyo mtu wa Mungu fedha hiyo, atuambie njia yetu. 9 (Hapo zamani katika Israeli, mtu alipokwenda kuuliza neno kwa Mungu, husema hivi, Haya! Twende kwa mwonaji; maana mtu aitwaye sasa Nabii hapo zamani aliitwa Mwonaji.) Esaïe 30.10 2 Rois 17.13 1 Chroniques 26.28 2 Samuel 24.11 Amos 7.12 10 Basi Sauli akamwambia mtumishi wake, Umesema vema; haya! Twende. Wakaenda mpaka mji ule aliokuwamo mtu wa Mungu. 2 Rois 5.13-5.14 11 Hata walipokwea kwenda mjini, wakakutana na wasichana, wanatoka kwenda kuteka maji; wakawaambia, Je! Mwonaji yuko? Genèse 24.11 Exode 2.16 Juges 5.11 Genèse 24.18-24.20 12 Nao wakawajibu, wakasema, Yuko; tazama, yuko huko mbele yako; fanyeni haraka sasa, maana hivi leo amekuja mjini; kwa sababu watu wana dhabihu leo katika mahali pa juu; Genèse 31.54 1 Samuel 16.2 1 Rois 3.2-3.4 1 Samuel 10.5 1 Corinthiens 5.7-5.8 13 mkiingia mjini tu, mara mtamwona, kabla hajakwea kwenda mahali pa juu ale chakula; maana, watu hawatakula hata yeye atakapokuja; kwa sababu yeye ndiye anayeibarikia dhabihu; kisha hao watu walioalikwa hula. Basi, kweeni sasa; maana wakati huu ndio mtakapomwona. Jean 6.11 Jean 6.23 Marc 6.41 1 Timothée 4.4 Luc 24.30 14 Nao wakakwea kwenda mjini; nao walipokuwa wakiingia mjini, tazama, Samweli akawatokea, kwenda mahali pa juu. 15 Basi Bwana alikuwa amemfunulia Samweli, siku moja kabla Sauli hajamwendea, akisema, Actes 13.21 1 Samuel 15.1 1 Samuel 9.17 Marc 14.13-14.16 Actes 27.23 16 Kesho, wakati kama huu, nitakuletea mtu kutoka nchi ya Benyamini, nawe mtie mafuta ili awe mkuu juu ya watu wangu Israeli, naye atawaokoa watu wangu na mikono ya Wafilisti; maana nimewaangalia watu wangu, kwa sababu kilio chao kimenifikilia. 1 Samuel 10.1 Exode 3.7-3.9 2 Rois 9.3-9.6 1 Samuel 15.1 1 Rois 19.15-19.16 17 Hata Samweli alipomwona Sauli, Bwana akamwambia, Huyu ndiye niliyekuambia habari zake; huyu ndiye atakayewamiliki watu wangu. Néhémie 13.25 2 Samuel 23.6-23.7 Romains 13.3-13.4 Osée 13.11 Néhémie 13.19 18 Ndipo Sauli akamkaribia Samweli langoni, akasema, Tafadhali, uniambie, nyumba ya mwonaji iko wapi? 19 Samweli akamjibu Sauli, akasema, Mimi ndimi mwonaji; tangulia mbele yangu ukwee mpaka mahali pa juu, kwa maana mtakula pamoja nami leo; kisha, asubuhi nitakuacha uende zako, nami nitakuambia yote uliyo nayo moyoni mwako. Jean 4.29 1 Corinthiens 14.25 20 Na wale punda zako waliopotea siku hizi tatu, usijiudhi kwa ajili yao; maana wameonekana. Na yote yaliyotamanika katika Israeli amewekewa nani? Si wewe, na nyumba yote ya baba yako? 1 Samuel 12.13 1 Samuel 8.5 1 Samuel 9.3 Colossiens 3.2 Psaumes 62.10 21 Basi Sauli akajibu, akasema, Je! Mimi si Mbenyamini, mtu wa kabila iliyo ndogo kuliko kabila zote za Israeli? Na jamaa yangu nayo si ndogo kuliko jamaa zote za kabila ya Benyamini? Kwa nini basi, kuniambia hivyo? 1 Samuel 15.17 Juges 20.46-20.48 Psaumes 68.27 1 Samuel 18.23 Luc 14.11 22 Naye Samweli akamtwaa Sauli na mtumishi wake, akawaleta ndani sebuleni, akawaketisha mahali pa heshima kati ya watu walioalikwa, nao jumla yao walikuwa kama watu thelathini. Genèse 43.32 Luc 14.10 23 Samweli akamwambia mpishi, Lete ile sehemu niliyokupa, hiyo niliyokuambia, Iweke akiba. 1 Samuel 1.5 Genèse 43.34 24 Basi mpishi akatwaa paja, na nyama iliyokuwa juu yake, akaiweka mbele ya Sauli. Samweli akasema, Iliyowekwa akiba ndiyo hiyo! Iweke mbele yako ule, kwa sababu umewekewa hiyo wewe hata wakati uliokusudiwa, maana nalisema, Nimewaalika watu. Basi Sauli akala pamoja na Samweli siku hiyo. Lévitique 7.32-7.33 Ezéchiel 24.4 Exode 29.22 Exode 29.27 Nombres 18.18 25 Hata waliposhuka kutoka mahali pa juu na kufika mjini, akaongea na Sauli darini. Deutéronome 22.8 Actes 10.9 Néhémie 8.16 2 Samuel 11.2 Jérémie 19.13 26 Nao wakaamka alfajiri; kisha ikawa, kulipopambazuka, Samweli akamwita Sauli darini, akisema, Inuka, nikupeleke kwenu. Basi Sauli akainuka, nao wakatoka wote wawili, yeye na Samweli. Genèse 44.4 Juges 19.28 Josué 7.13 Genèse 19.14 27 Hata walipokuwa wakishuka mwisho wa mji, Samweli akamwambia Sauli, Mwambie mtumishi atangulie, (naye akatangulia), bali wewe simama hapa sasa, ili nikuambie neno la Mungu. 2 Rois 9.5-9.6 1 Samuel 15.16 1 Samuel 20.38-20.39 Jean 15.14-15.15