Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

1 Chroniques 5.4
Bible en Swahili de l’est


Descendance de Ruben, Gad et Manassé

1 Na wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli; (kwa maana ndiye aliyekuwa mzaliwa wa kwanza, lakini, kwa kuwa alikinajisi kitanda cha babaye, haki yake ya mzaliwa wa kwanza walipewa wana wa Yusufu, mwana wa Israeli; tena nasaba isihesabiwe kwa kuifuata hiyo haki ya mzaliwa wa kwanza.
Genèse 29.32 Genèse 35.22 Genèse 48.15-48.22 1 Chroniques 26.10 1 Chroniques 2.1
2 Kwani Yuda ndiye aliyeshinda miongoni mwa nduguze, na kwake ndiko alikotoka mtawala; bali haki ile ya mzaliwa wa kwanza alipewa Yusufu);
Michée 5.2 Matthieu 2.6 Hébreux 7.14 Genèse 49.8-49.10 Psaumes 60.7
3 wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli; Hanoki, na Palu, na Hesroni, na Karmi.
Genèse 46.9 Exode 6.14 Nombres 26.5-26.9
4 Wana wa Yoeli; mwanawe huyo ni Shemaya, na mwanawe huyo ni Gogu, na mwanawe huyo ni Shimei;
5 na mwanawe huyo ni Mika, na mwanawe huyo ni Reaya, na mwanawe huyo ni Baali;
6 na mwanawe huyo ni Beera, ambaye Tiglath-Pileseri, mfalme wa Ashuru, alimchukua mateka; ndiye aliyekuwa mkuu wa Wareubeni.
1 Chroniques 5.26 2 Rois 16.7 2 Chroniques 28.20 2 Rois 15.29
7 Na nduguze kwa jamaa zao, hapo ilipohesabiwa nasaba ya vizazi vyao; mkuu wao, Yeieli, na Zekaria,
1 Chroniques 5.17
8 na Bela, mwana wa Azazi, mwana wa Shemaya, mwana wa Yoeli, aliyekaa huko Aroeri, hata kufika Nebo na Baal-meoni;
Nombres 32.34 1 Chroniques 5.4 Nombres 32.38 Josué 13.17 Deutéronome 34.1
9 na upande wa mashariki akakaa hata kufika maingilio ya jangwa litokalo mto wa Frati; kwa sababu ng’ombe zao walikuwa wameongezeka sana katika nchi ya Gileadi.
Josué 22.8-22.9
10 Na katika siku za Sauli wakapigana vita na Wahajiri, ambao waliangushwa kwa mikono yao; nao wakakaa katika hema zao katika nchi yote upande wa mashariki wa Gileadi.
1 Chroniques 5.18-5.21 Genèse 25.12 Genèse 21.9 Psaumes 83.6
11 Na wana wa Gadi walikuwa wakikaa kwa kuwaelekea, katika nchi ya Bashani mpaka Saleka;
Josué 13.11 Josué 13.24-13.28 Nombres 32.34-32.36 Deutéronome 3.10-3.17
12 Yoeli, alikuwa mkuu wao, na wa pili Shafamu, na Yanai, na Shafati, katika Bashani;
13 na ndugu zao wa mbari za baba zao; Mikaeli, na Meshulamu, na Sheba, na Yorai, na Yakani, na Zia, na Eberi, watu saba.
14 Hao ndio wana wa Abihaili, mwana wa Huri, mwana wa Yaroa, mwana wa Gileadi, mwana wa Mikaeli, mwana wa Yehishai, mwana wa Yado, mwana wa Buzi;
15 Ahi, mwana wa Abdieli, mwana wa Guni, alikuwa mkuu wa mbari za baba zao.
16 Nao wakakaa huko Gileadi, katika Bashani, na katika miji yake, na katika viunga vyote vya Sharoni, hata kufika mipakani mwake.
1 Chroniques 27.29 Cantique 2.1 Esaïe 35.2
17 Hao wote walihesabiwa kwa nasaba, katika siku za Yothamu, mfalme wa Yuda, na siku za Yeroboamu, mfalme wa Israeli.
2 Rois 14.28 2 Rois 14.16 2 Rois 15.32 2 Rois 15.5 2 Chroniques 27.1
18 Wana wa Reubeni, na Wagadi, na nusu-kabila ya Manase, watu mashujaa, wawezao kuchukua ngao na upanga, na kupiga upinde, wenye ustadi katika kupigana vita, walikuwa watu arobaini na nne elfu mia saba na sitini, walioweza kwenda vitani.
Nombres 1.3 Josué 4.12-4.13
19 Nao wakapigana vita na Wahajiri; na Yeturi, na Nafishi, na Nodabu.
1 Chroniques 1.31 Genèse 25.15 1 Chroniques 5.10
20 Wakapata msaada juu yao, nao Wahajiri walitiwa mikononi mwao, na wote waliokuwa pamoja nao; kwa kuwa walimlingana Mungu pale vitani; naye akayatakabali maombi yao, kwa sababu walimtumaini yeye.
Psaumes 22.4-22.5 2 Chroniques 18.31 Psaumes 9.10 Psaumes 20.7-20.8 Josué 10.42
21 Wakateka nyara ng’ombe zao, na ngamia zao hamsini elfu, na kondoo zao mia mbili na hamsini elfu, na punda zao elfu mbili; na watu mia elfu.
Nombres 31.35 Apocalypse 18.13
22 Kwani wengi walianguka waliouawa, kwa sababu vita vile vilikuwa vya Mungu. Nao wakakaa badala yao hata wakati wa ule uhamisho.
2 Rois 15.29 2 Rois 17.6 2 Chroniques 32.8 Romains 8.31 Josué 23.10
23 Na wana wa nusu-kabila ya Manase walikaa katika nchi; nao wakaongezeka kutoka Bashani mpaka Baal-hermoni, na Seniri, na mlima Hermoni.
Deutéronome 3.8-3.9 Cantique 4.8 Josué 13.29-13.31 Josué 13.11 Psaumes 133.3
24 Na hawa ndio wakuu wa mbari za baba zao; Eferi, na Ishi, na Elieli, na Azrieli, na Yeremia, na Hodavia, na Yadieli; watu hodari wa vita, watu mashuhuri, wakuu wa mbari za baba zao.
1 Chroniques 4.38
25 Nao wakamwasi Mungu wa baba zao, wakaenda kufanya uasherati na miungu ya watu wa nchi, ambao Mungu alikuwa amewaangamiza mbele yao.
Exode 34.15 Psaumes 106.34-106.39 Deutéronome 32.15-32.18 Juges 2.17 Osée 1.2
26 Naye Mungu wa Israeli akamwamsha roho Pulu, mfalme wa Ashuru na roho ya Tiglath-Pileseri, mfalme wa Ashuru, naye akawachukua mateka hao Wareubeni, na Wagadi, na nusu-kabila ya Wamanase; akawaleta mpaka Hala, na Habori, na Hara, na mpaka mto wa Gozani, hata siku hii ya leo.
2 Rois 15.19 2 Rois 17.6 2 Rois 18.11 2 Rois 15.29 1 Chroniques 5.6

Cette Bible est dans le domaine public.