Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

2 Chroniques 15.4
Bible en Swahili de l’est


1 Ndipo roho ya Mungu ikamjia Azaria mwana wa Odedi;2 Chroniques 20.14 2 Chroniques 24.20 Nombres 24.2 Juges 3.10 2 Samuel 23.2
2 naye akatoka ili amlaki Asa, akamwambia, Nisikieni, Ee Asa, na Yuda wote na Benyamini; Bwana yu pamoja nanyi, mkiwa pamoja naye; nanyi mkimtafuta ataonekana kwenu; lakini mkimwacha atawaacha ninyi.2 Chroniques 24.20 2 Chroniques 15.4 1 Chroniques 28.9 Jacques 4.8 2 Chroniques 15.15
3 Basi tangu siku nyingi Israeli wamekuwa hawana Mungu wa kweli, wala hawana kuhani afundishaye, wala hawana torati;Lévitique 10.11 Osée 3.4 1 Rois 12.28-12.33 Michée 3.11 1 Jean 5.20
4 lakini walipomgeukia Bwana, Mungu wa Israeli, katika msiba wao, na kumtafuta, akaonekana kwao.Esaïe 55.6 Esaïe 65.1-65.2 2 Chroniques 15.15 Deutéronome 4.29-4.30 Psaumes 106.44
5 Hata na zamani zile hakukuwa na amani kwake atokaye, wala kwake aingiaye, ila fadhaa kubwa juu yao wote wakaao katika nchi.Juges 5.6 Psaumes 121.8 Matthieu 24.6-24.7 1 Samuel 13.6 Luc 21.25
6 Wakavunjika-vunjika, taifa juu ya taifa, na mji juu ya mji; kwani Mungu aliwafadhaisha kwa shida zote.Esaïe 10.6 Matthieu 24.7 Marc 13.8 2 Chroniques 36.17 2 Chroniques 12.15
7 Nanyi jipeni nguvu, wala mikono yenu isilegee; kwa maana kazi yenu itakuwa na ijara.Josué 1.9 Josué 1.7 1 Chroniques 28.20 Hébreux 10.35 Psaumes 58.11
8 Naye Asa alipoyasikia maneno hayo, yaani, unabii wa mwana wa Odedi nabii, akatiwa nguvu, akayaondolea mbali machukizo yote katika nchi ya Yuda na Benyamini, na katika miji aliyoitwaa milimani mwa Efraimu; akaifanyiza tena madhabahu ya Bwana, iliyokuwako mbele ya ukumbi wa Bwana.2 Chroniques 8.12 2 Chroniques 13.19 2 Chroniques 4.1 Esaïe 44.14 2 Chroniques 29.18
9 Akakusanya Yuda wote na Benyamini, na hao wageni waliokaa kwao, wa Efraimu, na wa Manase, na wa Simeoni; kwa kuwa walimwangukia wengi katika Israeli, walipoona kwamba Bwana, Mungu wake, alikuwa pamoja naye.2 Chroniques 11.16 Genèse 39.3 1 Rois 12.19 1 Samuel 18.28 2 Chroniques 30.25
10 Basi wakakusanyika huko Yerusalemu mwezi wa tatu, katika mwaka wa kumi na tano wa kumiliki kwake Asa.Esther 8.9
11 Wakamchinjia Bwana siku ile, katika nyara walizozileta, dhabihu za ng’ombe mia saba, na kondoo elfu saba.2 Chroniques 14.13-14.15 2 Chroniques 1.6 2 Chroniques 7.5 Nombres 31.28-31.29 1 Samuel 15.21
12 Wakafanya agano, ya kuwa watamtafuta Bwana, Mungu wa baba zao, kwa mioyo yao yote, na kwa roho zao zote;2 Chroniques 23.16 2 Chroniques 29.10 Néhémie 10.29 2 Rois 23.3 Néhémie 9.38
13 na ya kwamba ye yote asiyemtafuta Bwana, Mungu wa Israeli, atauawa, akiwa mdogo au mkubwa, kwamba ni mwanamume au mwanamke.Exode 22.20 Deutéronome 17.2-17.5 Apocalypse 20.12 Psaumes 115.13 Deutéronome 13.5-13.15
14 Wakamwapia Bwana kwa sauti kuu, na kwa kelele, na kwa mapanda, na kwa baragumu.Néhémie 10.29 Psaumes 81.1-81.4 Néhémie 5.13
15 Na Yuda wote wakakifurahia kile kiapo; kwani wameapa kwa moyo wao wote, na kumtafuta kwa mapenzi yao pia; naye ameonekana kwao; naye Bwana akawastarehesha pande zote.2 Chroniques 14.7 2 Chroniques 15.12 2 Chroniques 15.4 2 Corinthiens 1.12 2 Chroniques 29.36
16 Hata na Maaka mamaye Asa, mfalme akamwondolea daraja yake asiwe malkia, kwa kuwa amefanya sanamu ya kuchukiza kwa Ashera; basi Asa akaikata sanamu yake, akaiponda, akaiteketeza penye kijito cha Kidroni.1 Rois 15.13-15.24 1 Rois 15.2 2 Rois 23.15 Exode 34.13 1 Rois 15.10
17 Lakini mahali pa juu hapakuondolewa katika Israeli; ila moyo wake Asa ulikuwa mkamilifu siku zake zote.2 Rois 12.3 1 Rois 22.43 2 Rois 14.4 2 Chroniques 14.3-14.5 2 Chroniques 16.7-16.12
18 Akavileta nyumbani mwa Mungu vitu alivyovitakasa babaye, na vile alivyovitakasa mwenyewe, fedha, na dhahabu, na vyombo.1 Rois 15.14-15.15 1 Chroniques 26.20-26.26 1 Rois 7.51
19 Wala hapakuwa na vita tena hata mwaka wa thelathini na tano wa kutawala kwake Asa.1 Rois 15.16-15.17 1 Rois 15.33 2 Chroniques 16.1 1 Rois 15.31

Cette Bible est dans le domaine public.