Un clic sur un verset envoie vers le comparateur de versions.
Job 17.10 Bible en Swahili de l’est
1 Roho yangu imezimika, siku zangu zimekoma, Kaburi i tayari kunipokea. 2 Ni kweli wako kwangu wenye kufanya dhihaka, Jicho langu hukaa katika kunifanyia uchungu kwao. 3 Nipe rehani basi, uwe dhamana kwa ajili yangu kwako wewe mwenyewe; Kuna nani atakayeniwekea dhamana? 4 Kwani mioyo yao imeificha ufahamu; Kwa hiyo hutawakuza. 5 Awafitiniye rafiki zake wawe mawindo, Hata macho ya watoto wake yataingia kiwi. 6 Amenifanya niwe simo kwa watu; Nimekuwa mwenye kuchukiwa kwa wazi. 7 Jicho langu nalo limekuwa giza kwa sababu ya majonzi, Na via vyangu vyote vimekuwa kama kivuli. 8 Walekevu watayastaajabia hayo, Na asiye na hatia atajiamsha juu ya mpotovu. 9 Lakini mwenye haki ataishika njia yake, Naye mwenye mikono safi atazidi kupata nguvu. 10 Lakini rudini; ninyi nyote, njoni sasa; Wala sitampata mtu mwenye hekima kati yenu. 11 Siku zangu zimepita, makusudi yangu yamevunjika, Hata hayo niliyo nayo moyoni mwangu. 12 Wabadili usiku kuwa mchana; Wasema, Mwanga u karibu kwa sababu ya giza. 13 Nikitazamia kuzimu kuwa nyumba yangu; Nikitandika malazi yangu gizani; 14 Ikiwa nimeuita uharibifu, Wewe u baba yangu; Na kuliambia buu, Wewe u mama yangu, na umbu langu; 15 Basi, tumaini langu li wapi? Na tumaini langu, ni nani atakayeliona? 16 Litashuka kwenye makomeo ya kuzimu, Itakapokuwapo raha mavumbini.