Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 25.20
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Bwana, nakuinulia nafsi yangu,Psaumes 143.8 Psaumes 86.4 Lamentations 3.41 Psaumes 24.4 1 Samuel 1.15
2 Ee Mungu wangu, Nimekutumaini Wewe, nisiaibike, Adui zangu wasifurahi kwa kunishinda.Psaumes 31.1 Psaumes 41.11 Esaïe 49.23 Psaumes 71.1 Esaïe 26.3
3 Naam, wakungojao hawataaibika hata mmoja; Wataaibika watendao uhaini bila sababu.Lamentations 3.25 Esaïe 49.23 Psaumes 62.5 Esaïe 40.31 Michée 7.7
4 Ee Bwana, unijulishe njia zako, Unifundishe mapito yako,Exode 33.13 Psaumes 27.11 Psaumes 5.8 Psaumes 86.11 Psaumes 143.8
5 Uniongoze katika kweli yako, Na kunifundisha. Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu, Nakungoja Wewe mchana kutwa.Psaumes 79.9 Psaumes 88.1 Apocalypse 7.17 Proverbes 8.34 Esaïe 30.18
6 Ee Bwana, kumbuka rehema zako na fadhili zako, Maana zimekuwako tokea zamani.Psaumes 103.17 Psaumes 69.16 Esaïe 63.15 Psaumes 98.3 Psaumes 106.45
7 Usiyakumbuke makosa ya ujana wangu, Wala maasi yangu. Unikumbuke kwa kadiri ya fadhili zako, Ee Bwana kwa ajili ya wema wako.Job 13.26 Psaumes 51.1 Job 20.11 Jérémie 3.25 Ephésiens 1.6-1.7
8 Bwana yu mwema, mwenye adili, Kwa hiyo atawafundisha wenye dhambi njia.Psaumes 92.15 Psaumes 32.8 Jacques 1.5 Matthieu 9.13 Proverbes 9.4-9.6
9 Wenye upole atawaongoza katika hukumu, Wenye upole atawafundisha njia yake.Jean 14.6 Matthieu 5.5 Psaumes 143.10 Psaumes 22.26 Sophonie 2.3
10 Njia zote za Bwana ni fadhili na kweli, Kwao walishikao agano lake na shuhuda zake.Jean 1.17 Hébreux 12.14 Hébreux 8.8-8.12 Psaumes 28.4-28.6 Jean 1.14
11 Ee Bwana, kwa ajili ya jina lako, Unisamehe uovu wangu, maana ni mwingi.Psaumes 79.9 Psaumes 31.3 Esaïe 43.25 Psaumes 109.21 Romains 5.15
12 Ni nani amchaye Bwana? Atamfundisha katika njia anayoichagua.Psaumes 37.23 2 Thessaloniciens 2.10-2.12 Psaumes 111.10 Proverbes 1.7 Proverbes 2.5
13 Nafsi yake itakaa hali ya kufanikiwa; Wazao wake watairithi nchi.Proverbes 19.23 Psaumes 37.11 Proverbes 1.33 Psaumes 112.2 Esaïe 65.23
14 Siri ya Bwana iko kwao wamchao, Naye atawajulisha agano lake.Jean 7.17 Proverbes 3.32 1 Corinthiens 2.14 Matthieu 13.11-13.12 Genèse 18.17-18.19
15 Macho yangu humwelekea Bwana daima, Naye atanitoa miguu yangu katika wavu.Psaumes 141.8 Psaumes 31.4 Psaumes 123.2 2 Timothée 2.25-2.26 Psaumes 121.1-121.2
16 Uniangalie na kunifadhili, Maana mimi ni mkiwa na mteswa.Psaumes 143.4 Psaumes 86.16 Daniel 9.17 Michée 7.19 Psaumes 60.1
17 Katika shida za moyo wangu unifanyie nafasi, Na kunitoa katika dhiki zangu.1 Corinthiens 4.11-4.13 Psaumes 107.6 Habakuk 3.17-3.19 Psaumes 77.2-77.4 2 Corinthiens 4.8-4.9
18 Utazame teso langu na taabu yangu; Unisamehe dhambi zangu zote.2 Samuel 16.12 1 Samuel 1.11 Matthieu 9.2 Psaumes 32.1-32.5 Psaumes 119.153
19 Uwatazame adui zangu, maana ni wengi, Wananichukia kwa machukio ya ukali.Psaumes 86.14 Psaumes 38.19 Psaumes 11.5 Psaumes 18.48 Luc 22.2
20 Unilinde nafsi yangu na kuniponya, Nisiaibike, maana nakukimbilia Wewe.Joël 2.26-2.27 Psaumes 17.8 Psaumes 86.2 Actes 7.59 Psaumes 121.7
21 Ukamilifu na unyofu zinihifadhi, Maana nakungoja Wewe.Psaumes 41.12 Proverbes 20.7 Proverbes 11.3 Psaumes 26.1 Psaumes 18.20-18.24
22 Ee Mungu, umkomboe Israeli, Katika taabu zake zote.Psaumes 130.8 Psaumes 122.6 Psaumes 14.7 Psaumes 51.18-51.19

Cette Bible est dans le domaine public.