Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Exode 34
Bible en Swahili de l’est


1 Kisha Bwana akamwambia Musa, Chonga mbao mbili za mawe mfano wa zile za kwanza; nami nitaandika juu ya mbao hizo maneno hayo yaliyokuwa juu ya mbao za kwanza, hizo ulizozivunja. Exode 32.19 Exode 31.18 Exode 34.28 Deutéronome 10.1-10.4 Deutéronome 9.15-9.17
2 Nawe uwe tayari asubuhi, na asubuhi ukwee juu katika mlima wa Sinai, nawe hudhurisha nafsi yako kwangu huko katika kilele cha mlima. Exode 19.20 Exode 19.24 Exode 19.11 Exode 24.12 Deutéronome 9.25
3 Asikwee mtu pamoja nawe, wala asionekane mtu awaye yote katika huo mlima; wala kondoo na ng’ombe wasilishe mbele ya huo mlima. Exode 19.12-19.13 Exode 19.21 Hébreux 12.20 1 Timothée 2.5 Lévitique 16.17
4 Naye akachonga mbao mbili za mawe mfano wa zile za kwanza; na Musa akainuka na mapema asubuhi, naye akakwea katika mlima wa Sinai, kama Bwana alivyomwamuru, akazichukua hizo mbao mbili za mawe mkononi mwake. 5 Bwana akashuka ndani ya lile wingu, akasimama pamoja naye huko, akalitangaza jina la Bwana. Exode 33.19 Luc 9.34-9.35 Nombres 11.25 Exode 33.9 Proverbes 18.10
6 Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli; Joël 2.13 Psaumes 86.15 Néhémie 9.17 Psaumes 103.8-103.13 Psaumes 145.8
7 mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne. Exode 20.5-20.6 Exode 23.7 Psaumes 103.3 Psaumes 130.4 Jérémie 32.18
8 Musa akafanya haraka, akainamisha kichwa chake hata nchi, akasujudu. Exode 4.31 Genèse 17.3 2 Chroniques 20.18
9 Akasema, Ikiwa sasa nimepata neema mbele zako, Bwana, nakuomba, Bwana, uende kati yetu, maana ni watu wenye shingo ngumu; ukasamehe uovu wetu na dhambi yetu, ukatutwae tuwe urithi wako. Psaumes 33.12 Exode 32.9 Deutéronome 32.9 Psaumes 78.62 Psaumes 28.9
10 Akasema, Tazama, nafanya agano; mbele ya watu wangu wote nitatenda miujiza, ya namna isiyotendeka katika dunia yote, wala katika taifa lo lote; na watu wote ambao unakaa kati yao wataona kazi ya Bwana, kwa maana ni neno la kutisha nikutendalo. Josué 6.20 Psaumes 78.12 2 Samuel 7.23 Esaïe 64.3 Psaumes 77.14
11 Liangalie neno hili ninalokuamuru leo; tazama, mbele yako namtoa Mwamori, na Mkanaani, na Mhiti, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi. Exode 33.2 Exode 3.17 Deutéronome 12.32 Deutéronome 6.25-7.1 Jean 14.21
12 Ujihadhari nafsi yako, usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi ile unayoiendea, lisiwe mtego katikati yako. Exode 23.32-23.33 Josué 23.12-23.13 Deutéronome 7.2 Juges 2.2-2.3 Psaumes 106.36
13 Bali utabomoa madhabahu zao, na kuvunja-vunja nguzo zao, na kuyakata-kata maashera yao. Exode 23.24 2 Rois 18.4 Juges 6.25 Juges 2.2 2 Chroniques 34.3-34.4
14 Maana hutamwabudu mungu mwingine, kwa kuwa Bwana, ambaye jina lake ni mwenye wivu, ni Mungu mwenye wivu. Deutéronome 6.15 Exode 20.3-20.5 Deutéronome 32.21 Deutéronome 29.20 Deutéronome 4.24
15 Usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi, watu wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, na kuitolea sadaka miungu yao; mtu mmoja akakuita, ukaila sadaka yake. Nombres 25.2 1 Corinthiens 8.4 Juges 2.17 Deutéronome 31.16 Lévitique 17.7
16 Ukawaoza wana wako binti zao, nao binti zao wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, wakawavuta wana wenu wafanye uzinzi na miungu yao. Esdras 9.2 1 Rois 11.2-11.4 Néhémie 13.25 Deutéronome 7.3-7.4 2 Corinthiens 6.14-6.17
17 Usijifanyizie miungu ya kuyeyusha. Lévitique 19.4 Exode 32.8 Jérémie 10.14 Esaïe 46.6-46.7 Actes 17.29
18 Hiyo sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu utaitunza. Utakula mikate isiyotiwa chachu muda wa siku saba, kama nilivyokuagiza, kwa majira yaliyoaganwa katika mwezi wa Abibu; kwa kuwa ulitoka Misri katika mwezi huo wa Abibu. Exode 13.4 Lévitique 23.6 Exode 12.15-12.20 Deutéronome 16.1-16.4 Marc 14.1
19 Kila kifunguacho mimba ni changu mimi; na wanyama wako wote walio waume, wazaliwa wa kwanza wa ng’ombe na wa kondoo. Exode 13.2 Exode 22.29 Exode 13.12 Luc 2.23 Nombres 18.15-18.17
20 Na mzaliwa wa kwanza wa punda utamkomboa kwa mwana-kondoo; tena kwamba hutaki kumkomboa, ndipo utamvunja shingo. Wazaliwa wa kwanza wote wa wanao utawakomboa. Wala hapana atakayehudhuria mbele zangu mikono mitupu. Exode 23.15 Deutéronome 16.16 Exode 13.15 Nombres 18.15 Exode 13.13
21 Utafanya kazi siku sita, lakini katika siku ya saba utapumzika; wakati wa kulima mashamba, na wakati wa kuvuna pia, utapumzika. Exode 23.12 Luc 13.14 Deutéronome 21.4 Exode 35.2 Esaïe 30.24
22 Nawe utaitunza sikukuu ya majuma, nayo ni ya malimbuko ya mavuno ya ngano, na sikukuu ya kukusanya vitu mwisho wa mwaka. Exode 23.16 Deutéronome 16.10-16.15 Nombres 28.16-28.31 Actes 2.1 Jean 7.2
23 Mara tatu kila mwaka watu waume wako wote watahudhuria mbele za Bwana MUNGU, Mungu wa Israeli. Exode 23.14 Deutéronome 16.16 Exode 23.17 Psaumes 84.7 Genèse 32.28
24 Kwa kuwa mimi nitazitupa nje taifa za watu mbele yako, na kuipanua mipaka yako; wala hapana mtu ye yote atakayeitamani nchi yako, hapo utakapokwea kwenda kuhudhuria mbele za Bwana Mungu wako mara tatu kila mwaka. Exode 33.2 Psaumes 78.55 Exode 23.27-23.31 Proverbes 16.7 Deutéronome 12.20
25 Usisongeze damu ya sadaka yangu pamoja na mkate uliotiwa chachu; wala hiyo sadaka ya sikukuu ya pasaka haitasazwa hata asubuhi. Exode 23.18 Exode 12.10 Exode 12.20 Lévitique 7.15 Deutéronome 16.3
26 Vitu vya kwanza vya malimbuko ya nchi yako utavileta na kuvitia ndani ya nyumba ya Bwana Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake. Exode 23.19 Deutéronome 14.21 Deutéronome 26.2 Matthieu 6.33 Jacques 1.18
27 Bwana akamwambia Musa, Andika maneno haya; kwa kuwa mimi nimefanya agano nawe, na pamoja na Israeli, kwa mujibu wa maneno haya. Exode 17.14 Deutéronome 31.9 Exode 34.10 Exode 24.4 Deutéronome 4.13
28 Naye alikuwa huko pamoja na Bwana siku arobaini na masiku yake; hakula chakula, wala hakunywa maji. Naye akaandika katika hizo mbao, hayo maneno ya maagano, hizo amri kumi. Deutéronome 4.13 Exode 34.1 Exode 24.18 Exode 31.18 Exode 32.16
29 Hata ikawa, Musa aliposhuka katika mlima Sinai, na zile mbao mbili za ushuhuda zilikuwa mkononi mwa Musa, hapo aliposhuka katika mlima, Musa hakujua ya kuwa ngozi ya uso wake iling’aa kwa sababu amesema naye. Matthieu 17.2 Exode 32.15 2 Corinthiens 3.13 Actes 12.9 Josué 2.4
30 Basi Haruni na wana wote wa Israeli walipomwona Musa, tazama, ngozi ya uso wake iling’aa; nao wakaogopa kumkaribia. Luc 5.8 Marc 9.3 Nombres 12.8 Marc 9.15
31 Musa akawaita; Haruni na wakuu wote wa kusanyiko wakarudi kwake; Musa akasema nao. Genèse 45.3 Exode 24.1-24.3 Exode 3.15 Genèse 45.15
32 Baadaye wana wa Israeli wote wakakaribia; akawausia maneno yote ambayo Bwana amemwambia katika mlima Sinai. Exode 21.1 Exode 24.3 1 Rois 22.14 Matthieu 28.20 Nombres 15.40
33 Na Musa alipokuwa amekwisha kusema nao, akatia utaji juu ya uso wake. 2 Corinthiens 4.4-4.6 2 Corinthiens 3.13-3.18 Romains 10.4
34 Lakini desturi ya Musa ilikuwa alipoingia mbele za Bwana kusema naye, kuuvua huo utaji mpaka atoke; akatoka akawaambia wana wa Israeli maneno yote aliyoambiwa. 2 Corinthiens 3.16 Hébreux 10.19-10.22 Hébreux 4.16
35 Wana wa Israeli wakauona uso wa Musa ya kuwa ngozi ya uso wake Musa iling’aa; naye Musa akautia utaji juu ya uso wake tena, hata alipoingia kusema naye. Ecclésiaste 8.1 Matthieu 5.16 Exode 34.29-34.30 Matthieu 13.43 Philippiens 2.15

Cette Bible est dans le domaine public.