Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Osée 10.12
Bible en Swahili de l’est


1 Israeli ni mzabibu, utoao matunda yake; kwa kadiri ya wingi wa matunda yake, kwa kadiri iyo hiyo ameongeza madhabahu zake; kwa kadiri ya wema wa nchi yake, kwa kadiri iyo hiyo wamefanya nguzo nzuri.Osée 8.11 Esaïe 5.1-5.7 Osée 12.11 1 Rois 14.23 Ezéchiel 15.1-15.5
2 Moyo wao umegawanyika; sasa wataonekana kuwa na hatia; yeye atazipiga madhabahu zao, ataziharibu nguzo zao.Michée 5.13 1 Rois 18.21 Sophonie 1.5 Matthieu 6.24 Zacharie 13.2
3 Yakini sasa watasema, Hatuna mfalme; kwa maana hatumchi Bwana; na mfalme huyu je! Aweza kututendea nini?Osée 10.15 Osée 13.11 Osée 10.7 Osée 11.5 Jean 19.15
4 Hunena maneno yasiyo na maana; huapa kwa uongo wafanyapo maagano; basi ndipo hukumu huchipuka kama mbaruti katika matuta ya shamba.Amos 6.12 Amos 5.7 Osée 4.2 Ezéchiel 17.13-17.19 2 Rois 17.3-17.4
5 Wakaao Samaria wataona hofu kwa ajili ya ndama za Beth-Aveni; kwa maana watu wa mji huo wataulilia, na makuhani wake walioufurahia, kwa sababu ya utukufu wake; kwa maana umetoweka.Osée 8.5-8.6 Osée 9.11 Osée 4.15 Osée 5.8 2 Rois 23.5
6 Nayo itachukuliwa Ashuru, iwe zawadi kwa mfalme Yarebu; Efraimu atapata aibu, na Israeli atalionea haya shauri lake mwenyewe.Osée 5.13 Esaïe 30.3 Jérémie 7.24 Daniel 11.8 Osée 11.5-11.6
7 Katika habari za Samaria, mfalme wake amekatiliwa mbali, kama povu usoni pa maji.Osée 10.3 2 Rois 1.3 Osée 10.15 2 Rois 15.30 1 Rois 21.1
8 Mahali pa Aveni palipoinuka, yaani, dhambi ya Israeli, pataharibika; mwiba na mbigili itamea juu ya madhabahu zake; nao wataiambia milima, Tusitirini; na vilima, Tuangukieni.Apocalypse 6.16 Luc 23.30 Osée 9.6 1 Rois 12.28-12.30 Esaïe 32.13
9 Ee Israeli, umefanya dhambi tangu siku za Gibea; huko ndiko walikosimama; ili vita vilivyokuwa juu ya wana wa uovu visiwapate katika Gibea.Osée 9.9 Genèse 6.5 Juges 20.13-20.14 Sophonie 3.6-3.7 Genèse 8.21
10 Wakati nitakapopenda nitawaadhibu; na hao mataifa watakusanyika juu yao, watakapofungwa kwa sababu ya makosa yao mawili.Ezéchiel 5.13 Jérémie 16.16 Osée 4.9 Esaïe 1.24 Zacharie 14.2-14.3
11 Naye Efraimu ni ndama aliyefundishwa, apendaye kupura; lakini nimepitisha kongwa juu ya shingo yake nzuri; nitampandisha mwenye kupanda juu ya Efraimu; Yuda atalima, na Yakobo atavunja madongoa yake.Osée 4.16 Deutéronome 25.4 Jérémie 50.11 2 Chroniques 28.5-28.8 Esaïe 28.24
12 Jipandieni katika haki, vuneni kwa fadhili; uchimbueni udongo wa mashamba yenu, kwa maana wakati umewadia wa kumtafuta Bwana, hata atakapokuja na kuwanyeshea haki.Jérémie 4.3-4.4 Osée 6.3 Proverbes 11.18 Esaïe 45.8 Jacques 3.18
13 Mmelima dhuluma, mmevuna uovu; mmekula matunda ya uongo; kwa maana uliitumainia njia yako, na wingi wa mashujaa wako.Job 4.8 Psaumes 33.16 Galates 6.7-6.8 Osée 8.7 Proverbes 22.8
14 Kwa sababu hiyo fitina itatokea kati ya watu wako, na ngome zako zote zitaharibiwa, kama vile Shalmani alivyoharibu Betharbeli, katika siku ya vita; mama akavunjika-vunjika pamoja na watoto wake.Osée 13.16 Nahum 3.10 Amos 3.8 Esaïe 22.1-22.4 2 Rois 19.11-19.13
15 Hivyo ndivyo Betheli atakavyowatenda ninyi, kwa sababu ya ubaya wenu mwingi; wakati wa mapambazuko mfalme wa Israeli atakatiliwa mbali kabisa.Osée 10.5 Osée 10.7 Osée 10.3 Esaïe 16.14 Romains 7.13

Cette Bible est dans le domaine public.