Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Matthieu 28
Bible en Swahili de l’est


1 Hata sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi. Matthieu 27.61 Matthieu 27.56 Luc 23.56-24.10 Marc 16.1-16.8 Luc 24.22
2 Na tazama, palikuwa na tetemeko kubwa la nchi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaja akalivingirisha lile jiwe akalikalia. Jean 20.12-20.13 Actes 16.26 Marc 16.3-16.5 1 Pierre 1.12 Jean 20.1
3 Na sura yake ilikuwa kama umeme, na mavazi yake meupe kama theluji. Marc 9.3 Actes 1.10 Marc 16.5 Jean 20.12 Ezéchiel 1.4-1.14
4 Na kwa kumwogopa, wale walinzi wakatetemeka, wakawa kama wafu. Apocalypse 1.17 Job 4.14 Daniel 10.7 Actes 9.3-9.7 Psaumes 48.6
5 Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulibiwa. Hébreux 1.14 Esaïe 41.14 Apocalypse 1.17-1.18 Daniel 10.19 Jean 20.13-20.15
6 Hayupo hapa; kwani amefufuka kama alivyosema. Njoni, mpatazame mahali alipolazwa. Matthieu 27.63 Matthieu 16.21 Marc 8.31 Matthieu 12.40 Marc 16.6
7 Nanyi nendeni upesi, mkawaambie wanafunzi wake, Amefufuka katika wafu. Tazama, awatangulia kwenda Galilaya; ndiko mtakakomwona. Haya, nimekwisha waambia. Matthieu 26.32 Matthieu 28.10 Jean 20.17-20.18 Esaïe 44.8 1 Corinthiens 15.6
8 Wakaondoka upesi kutoka kaburini, kwa hofu na furaha nyingi, wakaenda mbio kuwapasha wanafunzi wake habari. Psaumes 2.11 Jean 16.20 Jean 16.22 Esdras 3.12-3.13 Jean 20.20-20.21
9 Na tazama, Yesu akakutana nao, akisema, Salamu! Wakakaribia wakamshika miguu, wakamsujudia. Matthieu 28.17 Luc 24.52 Jean 20.28 Jean 20.14-20.17 Marc 16.9-16.10
10 Kisha Yesu akawaambia, Msiogope; enendeni, mkawaambie ndugu zangu waende Galilaya, ndiko watakakoniona. Romains 8.29 Jean 20.17 Matthieu 28.5 Matthieu 14.27 Matthieu 28.7
11 Nao wale walipokuwa wakienda, tazama, baadhi ya askari waliingia mjini, wakawapasha wakuu wa makuhani habari za mambo yote yaliyotendeka. Matthieu 27.65-27.66 Matthieu 28.4
12 Wakakusanyika pamoja na wazee, wakafanya shauri, wakawapa askari fedha nyingi, Matthieu 27.62-27.64 Psaumes 2.1-2.7 Matthieu 27.1-27.2 Actes 4.5-4.22 Matthieu 26.3-26.4
13 wakisema, Semeni, ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala. Matthieu 26.64
14 Na neno hili likisikilikana kwa liwali, sisi tutasema naye, nanyi tutawaondolea wasiwasi. Matthieu 27.2 Actes 12.19
15 Basi wakazitwaa zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Na neno hilo likaenea kati ya Wayahudi hata leo. Matthieu 27.8 1 Timothée 6.10 Matthieu 26.15
16 Na wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya mpaka mlima ule aliowaagiza Yesu. Matthieu 26.32 Matthieu 28.10 Matthieu 28.7 Marc 16.14 Actes 1.13-1.26
17 Nao walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao waliona shaka. Matthieu 28.9 1 Corinthiens 15.6 Jean 5.23 Psaumes 45.11 Psaumes 2.12
18 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. 1 Pierre 3.22 Ephésiens 1.20-1.22 Jean 3.35 Matthieu 11.27 1 Corinthiens 15.27
19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; Marc 16.15-16.16 Actes 1.8 Actes 13.46-13.47 Actes 2.38-2.39 Actes 2.41
20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. Esaïe 41.10 Actes 18.9-18.10 Josué 1.5 Psaumes 46.7 Genèse 39.2-39.3

Cette Bible est dans le domaine public.